1 Thessalonians 1 – KJV & NEN

King James Version

1 Thessalonians 1:1-10

1Paul, and Silvanus, and Timotheus, unto the church of the Thessalonians which is in God the Father and in the Lord Jesus Christ: Grace be unto you, and peace, from God our Father, and the Lord Jesus Christ. 2We give thanks to God always for you all, making mention of you in our prayers; 3Remembering without ceasing your work of faith, and labour of love, and patience of hope in our Lord Jesus Christ, in the sight of God and our Father; 4Knowing, brethren beloved, your election of God. 5For our gospel came not unto you in word only, but also in power, and in the Holy Ghost, and in much assurance; as ye know what manner of men we were among you for your sake. 6And ye became followers of us, and of the Lord, having received the word in much affliction, with joy of the Holy Ghost: 7So that ye were ensamples to all that believe in Macedonia and Achaia. 8For from you sounded out the word of the Lord not only in Macedonia and Achaia, but also in every place your faith to God-ward is spread abroad; so that we need not to speak any thing. 9For they themselves shew of us what manner of entering in we had unto you, and how ye turned to God from idols to serve the living and true God; 10And to wait for his Son from heaven, whom he raised from the dead, even Jesus, which delivered us from the wrath to come.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wathesalonike 1:1-10

Salamu

11:1 Mdo 16:1; 17:1; Rum 1:7Paulo, Silvano1:1 Yaani Sila. na Timotheo:

Kwa kanisa la Wathesalonike, ninyi mlio ndani ya Mungu Baba yetu na ndani ya Bwana Yesu Kristo:

Neema iwe kwenu na amani.

Shukrani Kwa Ajili Ya Imani Ya Wathesalonike

21:2 Rum 1:8; 2The 1:11; Efe 1:16; Flm 4Siku zote tunamshukuru Mungu kwa ajili yenu ninyi nyote, tukiwataja kwenye maombi yetu daima. 31:3 2The 1:11; 1The 2:13; Yn 6:29; Gal 5:6; 1The 3:6; Yak 2:17; Rum 16:6Tunaikumbuka daima kazi yenu ya imani mbele za Mungu aliye Baba yetu, taabu yenu katika upendo na saburi yenu ya tumaini katika Bwana wetu Yesu Kristo.

41:4 Kol 3:12; 2The 2:13Ndugu zetu mpendwao na Mungu, kwa kuwa tunajua kwamba Mungu amewachagua, 51:5 2The 2:14; Mk 16:20; 1Kor 6:6; Kol 2:2kwa sababu ujumbe wetu wa Injili haukuja kwenu kwa maneno matupu bali pia ulidhihirishwa katika nguvu na katika Roho Mtakatifu, tena ukiwa na uthibitisho kamili, kama vile ninyi wenyewe mnavyojua jinsi tulivyoenenda katikati yenu kwa ajili yenu. 61:6 1Kor 4:16; Mdo 17:5-10; 13:52Nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana, ingawa mlipata mateso mengi, mlilipokea lile Neno kwa furaha katika Roho Mtakatifu. 71:7 1The 4:10; Flp 3:7; 1Pet 5:3; 1Tim 4:12Hivyo ninyi mkawa kielelezo kwa waumini wote katika Makedonia na Akaya. 81:8 Rum 1:8; 10:18Kwa maana kutoka kwenu neno la Bwana limesikika, si katika Makedonia na Akaya tu, bali pia imani yenu katika Mungu imejulikana kila mahali kiasi kwamba hatuna haja ya kusema lolote kwa habari yake. 91:9 1Kor 12:2; Gal 4:8Kwa maana watu wa maeneo hayo wenyewe wanaeleza jinsi mlivyotupokea na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli 101:10 Mdo 2:24; Rum 5:9na ili kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu: yaani, Yesu, yeye aliyetuokoa kutoka ghadhabu inayokuja.