Job 27 – HTB & NEN

Het Boek

Job 27:1-23

12Zo waar God leeft, die mij gerechtigheid weigert, De Almachtige, die mijn leven verbittert: 3Zolang er nog een zucht in mij is, En Gods adem in mijn neus 4Zullen mijn lippen geen valsheid spreken, En zint mijn tong geen bedrog! 5Ik denk er niet aan, u gelijk te geven, Tot mijn laatste snik houd ik mijn onschuld vol; 6Ik houd vast aan mijn vroomheid, en geef ze niet op, Mijn hart schaamt zich over geen van mijn dagen! 7Moge het mijn vijand vergaan als den boze, Mijn hater als den goddeloze! 8Wat hoopt de boze, als hij bidt, Als hij zijn ziel tot de Godheid verheft? 9Zal God zijn schreien horen, Wanneer de rampspoed hem treft; 10Kan hij zich in den Almachtige verlustigen, Ten allen tijde roepen tot God? 11Daarna nam Sofar van Naäma het woord, en sprak: Ik zal u Gods werken leren kennen, De plannen van den Almachtige u niet verzwijgen: 12Zie, gij hebt het allen zelf aanschouwd: Waarom zo’n ijdele raad gegeven? 13Dit is, naar Gods bestel, het lot van den boze, Het deel der tyrannen, door den Almachtige hun toegewezen. 14Krijgt hij veel zonen, ze zijn bestemd voor het zwaard, En zijn kroost lijdt gebrek; 15Die hem overblijven, worden door de pest ten grave gesleept, En zijn weduwen bedrijven geen rouw. 16Al hoopt hij zilver op als stof, En stapelt kleren op als slijk, 17Hij stapelt ze op, maar de vrome bekleedt er zich mee, En de onschuldige erft zijn geld. 18Hij trekt zijn woning op als een spin, Aan de hut gelijk, die wachters bouwen; 19Rijk legt hij zich neer: het is de laatste maal, Hij opent zijn ogen: hij is er niet meer. 20Verschrikkingen grijpen hem aan overdag, En ‘s nachts sleurt een stormwind hem weg; 21De oostenwind neemt hem op: daar gaat hij heen, Hij vaagt hem weg van zijn plaats. 22Zonder erbarmen slingert God zijn pijlen op hem af, Zodat hij voor zijn slagen moet vluchten; 23Men klapt over hem in de handen, En fluit hem uit zijn woonplaats na.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ayubu 27:1-23

Hotuba Ya Mwisho Ya Ayubu

Ayubu Anadumisha Uadilifu Wake

127:1 Ay 29:1Ndipo Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:

227:2 Ay 9:18; 34:5; Isa 45:9; 1Sam 1:10“Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu,

Mwenyezi ambaye amenifanya

nionje uchungu wa nafsi,

327:3 Mwa 2:7; Za 144:4kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu,

nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu,

427:4 Ay 6:28; 12:16; 16:17midomo yangu haitanena uovu,

wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.

527:5 Ay 2:9; 10:7; 32:2Sitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi;

hadi nife, sitakana uadilifu wangu.

627:6 Ay 29:14; Za 119:121; Isa 59:17; 61:10; Rum 2:15Nitadumisha haki yangu wala sitaiacha;

dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi.

7“Watesi wangu wawe kama waovu,

nao adui zangu wawe kama wasio haki!

827:8 Ay 8:13; Hes 16:22; Lk 12:20; Mt 16:26Kwa maana mtu asiyemcha Mungu

analo tegemeo gani anapokatiliwa mbali,

Mungu anapouondoa uhai wake?

927:9 Zek 7:13; Mik 3:4; 1Sam 8:18Je, Mungu husikiliza kilio chake,

shida zimjiapo?

1027:10 Ay 22:26Je, anaweza kumfurahia Mwenyezi?

Je, atamwita Mungu nyakati zote?

1127:11 Ay 36:23; 27:13“Nitawafundisha juu ya uweza wa Mungu;

njia za Mwenyezi sitazificha.

12Ninyi nyote mmeona hili wenyewe.

Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana?

1327:13 Ay 15:20; 16:19“Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu,

urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi:

1427:14 Mao 2:22; Es 9:10; Hos 9:13; Ay 20:10; 2Fal 10:6-10Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani,

fungu lao ni kuuawa kwa upanga;

wazao wake hawatakuwa kamwe

na chakula cha kuwatosha.

1527:15 Za 78:64Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao,

nao wajane wao hawatawaombolezea.

1627:16 Zek 9:3Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi,

na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,

1727:17 Mit 13:22; Mhu 2:26yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa,

naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.

1827:18 Ay 8:14; Isa 1:8; 24:20; Mao 2:6Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui,

kama kibanda alichotengeneza mlinzi.

1927:19 Ay 3:13; Hes 20:26Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho;

afunguapo macho yake, yote yametoweka.

2027:20 Ay 15:21; 20:8Vitisho humjia kama mafuriko;

dhoruba humkumba ghafula usiku.

2127:21 Ay 38:24; Yer 13:24; Ay 30:22; 7:10; Yer 22:22Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka;

humzoa kutoka mahali pake.

2227:22 Yer 13:14; Eze 5:11; Ay 11:20Humvurumisha bila huruma,

huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake.

2327:23 Ay 7:10; 18:18Upepo humpigia makofi kwa dharau,

na kumfukuza atoke mahali pake.