马太福音 22 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

马太福音 22:1-46

王宴客的比喻

1耶稣又用比喻对他们说: 2“天国就像一个王为儿子筹备婚宴。 3他派奴仆去请受邀的客人,可是客人都不肯来。 4王再派其他奴仆去,说,‘去告诉被邀请的人,我的宴席已经备好,公牛和肥畜都宰了,一切都预备妥当,来赴婚宴吧!’ 5那些人却毫不理会地走了,一个去种田,一个去做买卖, 6其余的竟然抓住王的奴仆,把他们羞辱一番后杀了。 7王大怒,派军队去剿灭凶手,烧毁他们的城。

8“然后,他对奴仆说,‘婚宴已预备好了,只是被邀请的人不配。 9所以你们到街头巷尾,把所有见到的人都请到宴席上来。’ 10奴仆到街上把遇到的人都请了来,好人坏人都有,婚宴大厅里满了客人。

11“王出来会见在座的客人,发现有一个人没有穿礼服, 12就问他,‘朋友,你来这里怎么不穿婚宴的礼服呢?’那人无言以对。 13王便吩咐侍从,‘把他手脚绑起来丢到外面的黑暗里,让他在那里哀哭切齿。’

14“因为被邀请的人多,选上的人少。”

以纳税问题刁难耶稣

15那时,法利赛人出去策划怎样从耶稣的话里找把柄陷害祂。 16他们派了自己的门徒跟希律党人一同去问耶稣:“老师,我们知道你诚实无伪,按真理传上帝的道,不徇情面,因为你不以貌取人。 17那么请告诉我们,你认为向凯撒纳税对不对呢?”

18耶稣看出了他们的恶意,就说:“你们这些伪君子,为什么试探我呢? 19拿一个纳税用的钱币来给我看。”他们就拿给祂一个银币。

20耶稣问他们:“上面刻的是谁的像和名号?”

21他们说:“凯撒的。”

耶稣说:“那么,属于凯撒的东西应该给凯撒,属于上帝的东西应该给上帝。” 22他们听了很惊奇,只好离开祂走了。

论复活

23同一天,不相信死人会复活的撒都该人也来问耶稣, 24说:“老师,摩西说,‘如果一个人死了,没有儿女,只留下妻子,他的兄弟就当娶嫂嫂,替哥哥传宗接代。’ 25从前,我们这里有弟兄七人,老大结了婚,没有孩子就死了,把妻子留给了弟弟。 26二弟、三弟一直到七弟都相继娶了嫂嫂。 27最后,那女人也死了。 28那么,到复活的时候,她将是谁的妻子呢?因为他们都娶过她。”

29耶稣说:“你们弄错了。你们不明白圣经,也不知道上帝的能力。 30因为到复活的时候,人不娶也不嫁,就像天上的天使一样。

31“关于死人复活的事,你们没有读过上帝对你们说过的话吗? 32祂说,‘我是亚伯拉罕的上帝,以撒的上帝,雅各的上帝。’22:32 出埃及记3:6上帝不是死人的上帝,而是活人的上帝。” 33众人听到祂的教导都很惊奇。

最大的诫命

34法利赛人听见耶稣使撒都该人无言以对,就聚集在一起。 35其中有位律法专家试探耶稣说: 36“老师,请问律法中哪一条诫命最重要呢?”

37耶稣回答说:“‘你要全心、全情、全意爱主你的上帝’22:37 申命记6:538这是第一条也是最重要的诫命。 39第二条也相似,就是‘要爱邻如己’22:39 利未记19:1840律法和先知的全部教导都以这两条诫命为基础。”

基督的身份

41耶稣趁着法利赛人聚在那里,就问他们: 42“你们对基督有何看法?祂是谁的后裔?”他们答道:“大卫的后裔。”

43耶稣说:“那么,为什么大卫受圣灵感动,称祂为主呢?大卫曾说,

44“‘主对我主说,

你坐在我的右边,

等我把你的仇敌放在你脚下。’22:44 诗篇110:1

45既然大卫称基督为主,基督又怎么会是大卫的后裔呢?” 46没人能回答耶稣的问题。此后,再没人敢用问题刁难耶稣。

Kiswahili Contemporary Version

Mathayo 22:1-46

Mfano Wa Karamu Ya Arusi

(Luka 14:15-24)

122:1 Lk 14:16; Ufu 19:7-9Yesu akasema nao tena kwa mifano, akawaambia, 222:2 Mt 13:24; Yn 3:29“Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi. 322:3 Mt 21:34Akawatuma watumishi wake kuwaita wale waliokuwa wamealikwa karamuni, lakini wakakataa kuja.

422:4 Mt 21:36“Kisha akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa kwamba nimeandaa chakula. Nimekwisha kuchinja mafahali wangu na vinono, karamu iko tayari. Karibuni kwa karamu ya arusi.’

5“Lakini hawakuzingatia, wakaenda zao: huyu shambani mwake na mwingine kwenye biashara zake. 6Wengine wao wakawakamata wale watumishi wake, wakawatesa na kuwaua. 722:7 Lk 19:27Yule mfalme akakasirika sana, akapeleka jeshi lake likawaangamiza wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.

822:8 Mt 10:11-13“Kisha akawaambia watumishi wake, ‘Karamu ya arusi imeshakuwa tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja. 922:9 Eze 21:21; Mt 13:47; 21:43Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkamwalike karamuni yeyote mtakayemwona.’ 1022:10 Mt 13:47-48Wale watumishi wakaenda barabarani, wakawakusanya watu wote waliowaona, wema na wabaya. Ukumbi wa arusi ukajaa wageni.

1122:11 2Kor 5:3; Efe 4:24; Kol 3:10, 12; Ufu 3:4; 16:15; 19:8“Lakini mfalme alipoingia ndani ili kuwaona wageni, akamwona mle mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la arusi. 1222:12 Mt 20:12; 26:50Mfalme akamuuliza, ‘Rafiki, uliingiaje humu bila vazi la arusi?’ Yule mtu hakuwa na la kusema.

1322:13 Mt 8:12“Ndipo mfalme akawaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mikono na miguu mkamtupe nje, kwenye giza. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.’

1422:14 Ufu 17:14; Mt 20:16“Kwa maana walioitwa ni wengi, lakini walioteuliwa ni wachache.”

Kulipa Kodi Kwa Kaisari

(Marko 12:13-17; Luka 20:20-26)

1522:15 Mk 12:13; Lk 20:20Ndipo Mafarisayo wakatoka nje wakaandaa mpango wa kumtega Yesu katika maneno yake. 1622:16 Mk 3:6Wakatuma wanafunzi wao kwake pamoja na Maherode. Nao wakasema, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu na unafundisha njia ya Mungu katika kweli bila kuyumbishwa na mtu wala kuonyesha upendeleo. 1722:17 Mt 17:25Tuambie basi, wewe unaonaje? Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”

18Lakini Yesu, akijua makusudi yao mabaya, akawaambia, “Enyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? 19Nionyesheni hiyo sarafu inayotumika kwa kulipia kodi.” Wakamletea dinari. 20Naye akawauliza, “Sura hii ni ya nani? Na maandishi haya ni ya nani?”

2122:21 Rum 13:7Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.”

Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”

2222:22 Mk 12:12Waliposikia hili, wakashangaa. Hivyo wakamwacha, wakaenda zao.

Ndoa Na Ufufuo

(Marko 12:18-27; Luka 20:27-40)

2322:23 Mdo 4:1; 23:8; 1Kor 15:12Siku hiyo hiyo Masadukayo, wale wasemao kwamba hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Yesu na kumuuliza swali, wakisema, 2422:24 Kum 25:5-6“Mwalimu, Mose alisema, ‘Kama mtu akifa bila kuwa na watoto, ndugu yake inampasa amwoe huyo mjane ili ampatie watoto huyo nduguye aliyekufa.’ 25Basi palikuwa na ndugu saba miongoni mwetu. Yule wa kwanza akaoa mke, naye akafa, na kwa kuwa hakuwa na watoto, akamwachia nduguye yule mjane. 26Ikatokea vivyo hivyo kwa yule ndugu wa pili, na wa tatu, hadi wote saba. 27Hatimaye, yule mwanamke naye akafa. 28Sasa basi, siku ya ufufuo, yeye atakuwa mke wa nani miongoni mwa wale ndugu saba, kwa kuwa wote walikuwa wamemwoa huyo mwanamke?”

2922:29 Yn 20:9Yesu akawajibu, “Mwapotoka kwa sababu hamjui Maandiko wala uweza wa Mungu. 3022:30 Mt 24:38Wakati wa ufufuo, watu hawataoa wala kuolewa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni. 31Lakini kuhusu ufufuo wa wafu, hamjasoma kile Mungu alichowaambia, kwamba, 3222:32 Kut 3:6; Mdo 7:32‘Mimi ni Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo’? Yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.”

3322:33 Mt 7:28Ule umati wa watu uliposikia hayo, ulishangaa sana kwa mafundisho yake.

Amri Kuu Kuliko Zote

(Marko 12:28-34; Luka 10:25-28)

3422:34 Mdo 4:1Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, Mafarisayo wakakusanyika pamoja. 3522:35 Lk 11:45; 14:3Mmoja wao, mtaalamu wa sheria, akamuuliza swali ili kumjaribu, akisema, 36“Mwalimu, ni amri ipi katika Sheria iliyo kuu kuliko zote?”

3722:37 Kum 6:5Yesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ 38Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 3922:39 Law 19:18; Gal 5:14Nayo ya pili ni kama hiyo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ 4022:40 Mt 7:12; Lk 10:25-28Amri hizi mbili ndizo msingi wa Sheria na Manabii.”

Swali Kuhusu Mwana Wa Daudi

(Marko 12:35-37; Luka 20:41-44)

4122:41 Mk 12:35; Lk 20:41Wakati Mafarisayo walikuwa wamekusanyika pamoja, Yesu akawauliza, 4222:42 Mt 9:27“Mnaonaje kuhusu Kristo?22:42 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Yeye ni mwana wa nani?”

Wakamjibu, “Yeye ni mwana wa Daudi.”

43Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi, akinena kwa kuongozwa na Roho, anamwita Kristo ‘Bwana’? Kwa maana asema,

4422:44 1Fal 5:3; Ebr 1:13“ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:

“Keti mkono wangu wa kuume,

hadi nitakapowaweka adui zako

chini ya miguu yako.” ’

45Kama basi Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ awezaje kuwa mwanawe?” 4622:46 Mk 12:34; Lk 20:40Hakuna mtu aliyeweza kumjibu Yesu neno. Tena tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu kumuuliza tena maswali.