马太福音 14 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

马太福音 14:1-36

施洗者约翰之死

1那时,分封王希律听见耶稣的名声, 2就对臣仆说:“这个人是施洗者约翰!他从死里复活了,所以能行这些神迹。”

3原来希律为他兄弟腓力的妻子希罗底的缘故,拘捕了约翰,把他捆绑起来关在监牢。 4因为约翰曾多次对他说:“你娶这个妇人不合法。” 5他想杀掉约翰,但怕触怒百姓,因为他们都认为约翰是先知。

6希律的生日那天,希罗底的女儿在众人面前跳舞。希律非常高兴, 7就起誓答应她无论要什么都可以。 8她受了母亲的指使,说:“请把施洗者约翰的头放在盘子里送给我。” 9希律感到为难,但既然在众宾客面前起了誓,只好下令给她。 10他派人进监牢砍了约翰的头, 11放在盘子里送给女孩,她又转送给她母亲。 12约翰的门徒把尸体领回安葬后,就去告诉耶稣。

耶稣使五千人吃饱

13耶稣听见这个消息,就独自坐船退到一处荒僻的地方。众人得知后,就从各城步行来跟随祂。 14耶稣上了岸,看见一大群人,心里怜悯他们,就治好了他们当中的病人。 15黄昏时,门徒过来对耶稣说:“这里是荒郊野外,天又晚了,请遣散众人,好让他们到村庄去自己买些吃的。”

16耶稣回答说:“他们不用离开,你们给他们吃的吧。”

17门徒答道:“我们这里只有五个饼和两条鱼。”

18耶稣说:“拿来给我。”

19于是,祂叫众人坐在草地上,然后拿起那五个饼和两条鱼,举目望着天祝谢后,掰开饼递给门徒,让他们分给众人。 20大家都吃饱了,把剩下的零碎收拾起来,装满了十二个篮子。 21当时吃饭的,除了妇女和小孩,约有五千男人。

耶稣在水上行走

22随后,耶稣催门徒上船,叫他们先渡到湖对岸,祂则遣散众人。 23等众人都离开了,祂就独自上山去祷告,在那里一直待到晚上。

24那时,门徒的船离岸已远,遇到逆风,船身被波浪撞击得摇摆不定。 25天将破晓的时候,耶稣从水面上朝门徒走去。 26门徒看见祂在湖面上走,都吓坏了,说:“是幽灵!”他们害怕得又喊又叫。

27耶稣立刻对他们说:“放心吧!是我,不要怕。”

28彼得说:“主啊!如果真的是你,就叫我从水面上走到你那里。”

29耶稣说:“你来吧!”

于是,彼得就从船上下去,走在湖面上,要去耶稣那里。 30他看到风浪很大,就害怕起来,身体开始往下沉,便大喊:“主啊,救我!”

31耶稣马上伸手拉住他,说:“你信心太小了!为什么怀疑呢?”

32他们上了船,风浪就平静了。 33船上的人都敬拜祂,说:“你真是上帝的儿子。”

34他们渡到湖对岸,来到革尼撒勒35当地的人认出是耶稣,就派人去把附近所有的病人都带到祂面前, 36求耶稣让他们只摸一摸祂衣服的穗子,所有摸过的病人都好了。

Kiswahili Contemporary Version

Mathayo 14:1-36

Yohana Mbatizaji Akatwa Kichwa

(Marko 6:14-29; Luka 9:7-9)

114:1 Lk 13:31; 9:7-9; Mdo 12:1Wakati huo, Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za Yesu, 214:2 Mt 3:1akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji; amefufuka kutoka kwa wafu! Hii ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”

314:3 Mt 4:12; 11:2; Lk 3:19-20Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga na kumweka gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, 414:4 Law 18:16; 20:21kwa kuwa Yohana alikuwa amemwambia Herode: “Si halali kwako kuwa na huyo mwanamke.” 514:5 Mt 11:19; 21:26; Lk 20:26Herode alitaka sana kumuua Yohana, lakini akaogopa watu, kwa maana walimtambua kuwa ni nabii.

6Katika siku ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti wa Herodia alicheza mbele ya watu waliohudhuria, akamfurahisha sana Herode, 7kiasi kwamba aliahidi kwa kiapo kumpa huyo binti chochote angeomba. 8Huyo binti, akiwa amechochewa na mama yake, akasema, “Nipe kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.” 9Mfalme akasikitika, lakini kwa sababu ya viapo alivyoapa mbele ya wageni, akaamuru kwamba apatiwe ombi lake. 1014:10 Mt 17:12Hivyo akaagiza Yohana Mbatizaji akatwe kichwa mle gerezani. 11Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake. 1214:12 Mt 8:2Wanafunzi wa Yohana wakaja na kuuchukua mwili wake kwenda kuuzika. Kisha wakaenda wakamwambia Yesu.

Yesu Alisha Wanaume 5,000

(Marko 6:30-44; Luka 9:10-17; Yohana 6:1-14)

1314:13 Mk 6:31-44; Mt 10:23; Mk 6:32; Lk 9:19; Yn 6:13Yesu aliposikia yaliyokuwa yametukia, aliondoka kwa chombo akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu walipopata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu kutoka miji. 1414:14 Mt 9:36; 4:23Yesu alipofika kando ya bahari, aliona makutano makubwa ya watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao.

1514:15 Mk 6:35; Lk 9:12; Yn 6:5Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makutano ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.”

16Yesu akawaambia, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.”

1714:17 Mt 16:9; 1Sam 9:13; 1Kor 10:16Wakamjibu, “Tuna mikate mitano na samaki wawili tu.”

18Akawaambia, “Nileteeni hivyo vitu hapa.” 1914:19 Mt 15:36; 1Sam 9:13; Mt 26:26; Mk 8:6; Lk 9:16; 24:30; Mdo 2:42; 20:7Yesu akaagiza makutano wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia makutano. 2014:20 2Fal 4:44Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili. 21Idadi ya watu waliokula walikuwa wanaume wapatao 5,000, bila kuhesabu wanawake na watoto.

Yesu Atembea Juu Ya Maji

(Marko 6:45-52; Yohana 6:15-21)

2214:22 Mk 6:45-46Mara Yesu akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda ngʼambo ya bahari, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano. 2314:23 Lk 3:21; 6:12; 9:18Baada ya kuwaaga, akaenda zake mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Yesu alikuwa huko peke yake. 24Wakati huo ile mashua ilikuwa mbali kutoka nchi kavu ikisukwasukwa na mawimbi, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.

25Wakati wa zamu ya nne ya usiku,14:25 Zamu ya nne ya usiku ni kati ya saa tisa na saa kumi na mbili asubuhi. Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. 2614:26 Lk 24:37; Ay 9:8Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga yowe kwa kuogopa.

2714:27 Mt 9:2; Mdo 23:11; Dan 10:12; Mdo 18:9Lakini mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope.”

28Petro akamjibu, “Bwana, ikiwa ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.”

29Yesu akamwambia, “Njoo.”

Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Yesu. 30Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!”

3114:31 Mt 6:30Mara Yesu akaunyoosha mkono wake na kumshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?”

32Nao walipoingia ndani ya mashua, upepo ukakoma. 3314:33 Za 2:7; Mt 4:3Ndipo wote waliokuwa ndani ya ile mashua wakamwabudu Yesu, wakisema, “Hakika, wewe ndiwe Mwana wa Mungu.”

Yesu Awaponya Wagonjwa Genesareti

(Marko 6:53-56)

34Walipokwisha kuvuka, wakafika nchi ya Genesareti. 35Watu wa eneo lile walipomtambua Yesu, walipeleka habari sehemu zote za jirani. Watu wakamletea wagonjwa wao wote, 3614:36 Mt 9:20-21wakamsihi awaruhusu wagonjwa waguse tu pindo la vazi lake, nao wote waliomgusa, wakaponywa.