马太福音 11 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

马太福音 11:1-30

耶稣和施洗者约翰

1耶稣嘱咐完十二个门徒,就离开那里,到附近的城镇传道和教导人。

2约翰在监狱中听到基督所做的事,就差门徒去问祂: 3“你就是我们所等候的那位吗?还是我们要等别人呢?”

4耶稣回答说:“你们回去把所见所闻告诉约翰5就是瞎眼的看见,瘸腿的走路,麻风病人得洁净,耳聋的听见,死人复活,穷人听到福音。 6凡对我笃信不疑的人有福了!”

7他们离开后,耶稣对众人谈论约翰,说:“你们从前去旷野要看什么呢?看随风摇动的芦苇吗? 8如果不是,你们出去到底想看什么?是看穿绫罗绸缎的人吗?那些穿绫罗绸缎的人在王宫里。 9你们出去究竟想看什么?看先知吗?是的,我告诉你们,他不只是先知。 10圣经上说,‘看啊,我要差遣我的使者在你前面为你预备道路’11:10 玛拉基书3:1,这里所指的就是约翰11我实在告诉你们,凡妇人所生的,没有一个兴起来比施洗者约翰大,然而天国里最微不足道的也比他大。

12“从施洗者约翰到现在,天国在强劲地扩展着,暴力之徒一直在攻击它。 13因为到约翰为止,所有的先知和律法都在预言天国的事。 14如果你们愿意接受,约翰就是那要来的以利亚15有耳朵的,都应当听。

16“我用什么来比拟这个世代的人呢?他们好像一群在街上玩耍的儿童对别的孩子说,

17“‘我们吹娶亲的乐曲,

你们不跳舞;

我们唱送葬的哀歌,

你们不捶胸。’

18约翰来了,也不吃也不喝,他们就说他被鬼附身。 19人子来了,又吃又喝,他们就说祂是贪吃好酒之徒,与税吏和罪人为友。然而智慧通过她的作为显明为义。”

不肯悔改的城

20那时,耶稣开始责备一些城镇,因为祂在那里行了许多神迹,当地的居民仍不肯悔改。 21祂说:“哥拉汛啊,你有祸了!伯赛大啊,你有祸了!因为如果把在你们当中所行的神迹行在泰尔西顿,那里的人早就身披着麻衣、头蒙着灰尘悔改了。 22所以我告诉你们,在审判之日,你们将比泰尔西顿受更重的刑罚!

23迦百农啊,你将被提升到天上吗?不!你将被打落到阴间。因为如果把在你那里所行的神迹行在所多玛,它肯定会存留到今天。 24所以我告诉你们,在审判之日,你们将比所多玛受更重的刑罚!”

劳苦者得安息

25那时,耶稣说:“父啊,天地的主,我颂赞你,因为你把这些事向聪明、有学问的人隐藏起来,却启示给像孩童一般的人。 26父啊,是的,这正是你的美意。 27我父将一切交给了我。除了父,没有人认识子;除了子和受子启示的人,没有人认识父。

28“所有劳苦困乏、背负重担的人啊,到我这里来吧!我要赐给你们安息。 29我心柔和谦卑,你们要负我的轭,向我学习,这样你们的心灵必得享安息。 30因为我的轭容易负,我的担子很轻省。”

Kiswahili Contemporary Version

Mathayo 11:1-30

Yesu Na Yohana Mbatizaji

(Luka 7:18-35)

111:1 Mt 7:28; 26:1Baada ya Yesu kumaliza kutoa maagizo kwa wanafunzi wake kumi na wawili, aliondoka hapo akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.

211:2 Mt 14:3Yohana aliposikia akiwa gerezani mambo ambayo Kristo11:2 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. alikuwa akiyafanya, aliwatuma wanafunzi wake 311:3 Za 118:26; Ebr 10:37ili wakamuulize, “Wewe ndiye yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?”

4Yesu akajibu, “Rudini mkamwambie Yohana yale mnayosikia na kuyaona: 511:5 Lk 4:18-19; Isa 61:1-2Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema. 611:6 Mt 13:21; 26:31Amebarikiwa mtu yule asiyechukizwa na mimi.”

711:7 Mt 3:1-5Wale wanafunzi wa Yohana walipokuwa wanaondoka, Yesu akaanza kusema na makutano kuhusu Yohana Mbatizaji. Akawauliza, “Mlipokwenda kule nyikani, mlikwenda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo? 8Kama sivyo, mlikwenda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya kifahari? La hasha, watu wanaovaa mavazi ya kifahari wako katika majumba ya wafalme. 911:9 Lk 1:76; 7:26Basi mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona nabii? Naam, nawaambia, yeye ni zaidi ya nabii. 1011:10 Mal 3:1; Lk 7:27Huyu ndiye ambaye habari zake zimeandikwa:

“ ‘Tazama nitamtuma mjumbe wangu mbele yako,

atakayetengeneza njia mbele yako.’

1111:11 Mt 13:17Amin, nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake, hajatokea mtu aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni ni mkuu kuliko Yohana. 1211:12 Lk 16:16; 13:24Tangu siku za Yohana Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wanauteka. 1311:13 Lk 16:16Kwa maana manabii wote na Sheria walitabiri mpaka wakati wa Yohana. 1411:14 Mal 4:5; Yn 1:21Ikiwa mko tayari kukubali hilo, yeye ndiye yule Eliya ambaye manabii walikuwa wamesema angekuja. 1511:15 Lk 14:35; Ufu 2:7Yeye aliye na masikio, na asikie.

1611:16 Lk 7:31“Lakini kizazi hiki nikifananishe na nini? Kinafanana na watoto waliokaa sokoni wakiwaita wenzao na kuwaambia,

1711:17 Mit 29:9“ ‘Tuliwapigia filimbi,

lakini hamkucheza;

tuliwaimbia nyimbo za maombolezo,

lakini hamkuomboleza.’

1811:18 Mt 3:4; Lk 1:15Kwa maana Yohana Mbatizaji alikuja, alikuwa hali wala hanywi, nao wanasema, ‘Yeye ana pepo mchafu.’ 1911:19 Mt 9:11Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, nao wanasema, ‘Tazameni huyu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na “wenye dhambi.” ’ Lakini hekima huthibitishwa kuwa kweli kwa matendo yake.”

Onyo Kwa Miji Isiyotubu

(Luka 10:13-15)

2011:20 Lk 10:11Ndipo Yesu akaanza kushutumu miji ambamo alifanya miujiza yake mingi kuliko kwingine, kwa maana watu wake hawakutubu. 2111:21 Mk 8:22; Yn 1:44; Yoe 3:4; Mk 3:8; Yn 3:5-9“Ole wako, Korazini! Ole wako Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu, ingefanyika Tiro na Sidoni, miji hiyo ingekuwa imetubu zamani kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu. 2211:22 Mt 11:24; 10:15Lakini nawaambia, itakuwa rahisi zaidi kwa Tiro na Sidoni kustahimili katika siku ya hukumu, kuliko ninyi. 2311:23 Mt 4:13; Isa 14:13-15Nawe Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha, utashushwa mpaka kuzimu.11:23 Kuzimu ni Mahali pa wafu. Miujiza iliyofanyika kwako ingefanyika huko Sodoma, mji huo ungalikuwepo hadi leo. 2411:24 Mt 10:15Lakini nakuambia kwamba, itakuwa rahisi zaidi kwa Sodoma kustahimili katika siku ya hukumu kuliko wewe.”

Hakuna Amjuaye Baba Ila Mwana

(Luka 10:21-22)

2511:25 Lk 23:34; Yn 12:27-28; Mt 13:11; 1Kor 1:26-29Wakati huo Yesu alisema, “Nakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo. 26Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza.

2711:27 Mt 28:18; Yn 3:35; 10:15; 17:25-26“Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: Hakuna mtu amjuaye Mwana ila Baba, wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana na yeyote ambaye Mwana anapenda kumfunulia.

Yesu Awaita Waliolemewa Na Mizigo

2811:28 Yn 7:37“Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 2911:29 Flp 2:5; 1Yn 2:6; Za 116:7; Yer 6:16Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 3011:30 1Yn 5:3Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.”