马可福音 13 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

马可福音 13:1-37

预言圣殿被毁

1耶稣走出圣殿的时候,有一个门徒对祂说:“老师,你看!这是多么大的石头,多么宏伟的建筑啊!”

2耶稣说:“你看见这些宏伟的建筑了吗?将来要被完全拆毁,找不到两块叠在一起的石头。”

3耶稣面向圣殿坐在橄榄山上,彼得雅各约翰安得烈私下来问祂: 4“请告诉我们,这些事什么时候会发生?有什么预兆?”

5耶稣回答说:“你们要小心,免得被人迷惑。 6将来会有许多人冒我的名来,说,‘我是基督’,欺骗许多人。

7“你们听见战争爆发、战讯频传时,不要惊慌,因为这些事必然发生,只是末日还没有到。

8“民族将攻打民族,国家将攻打国家,各处将有地震和饥荒。这些只是灾难13:8 “灾难”希腊文是“生产之痛”。的开始。

9“你们要小心谨慎,因为你们将被送上法庭,并在会堂里被鞭打,又将为了我的缘故在官长和君王面前做见证。 10不过,福音一定要先传遍天下。 11当你们被拘捕,押去受审时,不要先担心该说什么话,到时候赐给你们什么话,你们就说什么话,因为那时候说话的不是你们自己,而是圣灵。

12“那时,人将把自己的弟兄置于死地,父亲将把儿子置于死地,儿女将反叛父母,置他们于死地。 13你们将因我的名而被众人憎恨,但坚忍到底的必定得救。

大灾难

14“当你们看见‘那带来毁灭的可憎者’13:14 但以理书9:2711:3112:11站在不当站的地方时(读者须会意),犹太地区的人要逃到山上去; 15在屋顶上的人不要下来,不要进屋拿东西; 16在田间的人不要回家取外衣。 17那时,孕妇和哺育婴儿的母亲们可就遭殃了! 18你们要祈求上帝使这些事不要在冬天发生, 19因为那是上帝创造天地以来空前绝后的大灾难。 20如果主不缩短灾期,恐怕没有人能活命,但为了祂的选民,祂已经缩短灾期。 21那时,如果有人对你们说,‘看啊,基督在这里!’或说,‘基督在那里!’你们不要相信。 22因为假基督和假先知将出现,行各种神迹奇事,如果可能,甚至要迷惑上帝的选民。 23你们要小心,我已经把一切预先告诉你们了。

人子降临

24“大灾难过后,

‘太阳昏暗,

月亮无光,

25星宿陨落,

天体震动。’13:25 以赛亚书13:1034:4

26那时,世人必看到人子驾着云、带着极大的能力和荣耀降临。 27祂必差遣天使从四面八方、天涯海角招聚祂拣选的人。

28“你们可以从无花果树学个道理。当无花果树发芽长叶的时候,你们就知道夏天快来了。 29同样,当你们看见这些事情发生时,就知道人子快来了,就在门口。 30我实在告诉你们,这个世代还没有过去,这一切都要发生。 31天地都要消逝,但我的话永不消逝。

32“但没有人知道那日子和时辰何时来到,连天上的天使也不知道,人子也不知道,只有天父知道。 33你们要小心,保持警醒,因为你们不知道那日子何时来到。

34“这就好像一个人在出远门之前,把家中的事交给仆人,让他们各做各的工作,又吩咐守门的人要警醒。 35所以你们要警醒,因为你们不知道家主什么时候回来,可能是黄昏,可能是夜半,也可能是黎明或早上。 36别让他突然回来时看到你们在睡觉。 37我劝你们,也劝所有的人,要警醒!”

Kiswahili Contemporary Version

Marko 13:1-37

Dalili Za Siku Za Mwisho

(Mathayo 24:1-2; Luka 21:5-6)

113:1 Mt 24:1; Lk 21:5Yesu alipokuwa akitoka Hekaluni, mmojawapo wa wanafunzi wake akamwambia, “Mwalimu! Tazama jinsi mawe haya yalivyo makubwa, na majengo haya yalivyo mazuri!”

213:2 Lk 19:44Ndipo Yesu akajibu akasema, “Je, unayaona majengo haya yalivyo makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, bali yote yatabomolewa.”

Mateso Yatabiriwa

(Mathayo 24:3-14; Luka 21:7-19)

313:3 Mt 21:1; 4:21Yesu alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni mkabala na Hekalu, Petro, Yakobo, Yohana na Andrea wakamuuliza faraghani, 413:4 Mt 24:3; Lk 21:7“Tafadhali tuambie, mambo haya yatatukia lini? Nayo dalili ya kuwa hayo yote yanakaribia kutimia itakuwa gani?”

513:5 Yer 29:8; 1Tim 4:1Yesu akawaambia: “Jihadharini mtu yeyote asiwadanganye. 6Wengi watakuja kwa Jina langu wakidai, ‘Mimi ndiye,’ nao watawadanganya wengi. 7Msikiapo habari za vita na uvumi wa vita, msiwe na hofu. Mambo haya hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. 813:8 Mt 24:8; Isa 19:2; 2Nya 15:6Taifa litainuka dhidi ya taifa na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na mitetemeko sehemu mbalimbali na njaa. Haya yatakuwa ndio mwanzo wa utungu.

913:9 Mt 10:17“Lakini ninyi jihadharini. Kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kupigwa mijeledi katika masinagogi. Mtashtakiwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao. 1013:10 Mt 10:19-20Nayo habari njema lazima ihubiriwe kwanza kwa mataifa yote kabla ule mwisho haujawadia. 1113:11 Lk 12:11-12Mtakapokamatwa na kushtakiwa, msisumbuke awali kuhusu mtakalosema. Semeni tu lolote mtakalopewa wakati huo, kwa kuwa si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho Mtakatifu.

1213:12 Mik 7:6; Lk 12:51-53“Ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, naye baba atamsaliti mtoto wake. Watoto nao wataasi dhidi ya wazazi wao na kusababisha wauawe. 1313:13 Yn 15:21; Mt 10:22Watu wote watawachukia kwa ajili ya Jina langu. Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa.

Chukizo La Uharibifu

(Mathayo 24:15-28; Luka 21:20-24)

1413:14 Dan 11:31; 12:11“Mtakapoona ‘chukizo la uharibifu’ limesimama mahali pasipolipasa (asomaye na afahamu), basi wale walioko Uyahudi wakimbilie milimani. 15Yeyote aliye juu ya dari ya nyumba asishuke au kuingia ndani ili kuchukua chochote. 16Aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake. 1713:17 Lk 22:39; 21:23Ole wao wenye mimba na wale wanaonyonyesha watoto siku hizo! 18Ombeni mambo haya yasitokee wakati wa baridi. 1913:19 Mk 10:6; Dan 9:26; Yoe 2:2Kwa maana siku hizo zitakuwa za dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo, hapo Mungu alipoumba ulimwengu, mpaka leo, na wala haitakuwako tena kamwe. 20Kama Bwana asingelifupisha siku hizo, kamwe asingeliokoka mtu yeyote. Lakini kwa ajili ya wateule, wale aliowachagua, amezifupisha siku hizo. 2113:21 Lk 17:23; 21:8Wakati huo mtu yeyote akiwaambia, ‘Tazama, Kristo13:21 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. huyu hapa!’ au, ‘Tazama, yuko kule,’ msisadiki. 2213:22 Mt 7:15; Yn 4:48; 2The 2:9-10Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo, nao watafanya ishara na maajabu ili kuwapotosha, ikiwezekana, hata wale wateule. 2313:23 2Pet 3:17Hivyo jihadharini. Nimekwisha kuwaambia mambo haya yote mapema kabla hayajatukia.

Kuja Kwa Mwana Wa Adamu

(Mathayo 24:29-31; Luka 21:25-28)

2413:24 Isa 13:10“Lakini katika siku hizo, baada ya hiyo dhiki,

“ ‘jua litatiwa giza

nao mwezi hautatoa nuru yake;

2513:25 Isa 34:4; Mt 24:9nazo nyota zitaanguka kutoka angani,

na nguvu za anga zitatikisika.’

2613:26 Dan 7:13; Ufu 1:7“Ndipo watu wote watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu. 2713:27 Zek 2:6Naye atawatuma malaika wake wawakusanye wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka miisho ya dunia hadi miisho ya mbingu.

Somo Kuhusu Mtini

(Mathayo 24:32-35; Luka 21:29-33)

2813:28 Mt 24:32; Lk 21:29“Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 29Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni. 3013:30 Lk 17:25; Mk 9:11Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. 3113:31 Mt 5:18Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Hakuna Ajuaye Siku Wala Saa

(Mathayo 24:36-44)

3213:32 Mdo 1:7; 1The 5:1-2“Kwa habari ya siku ile na saa hakuna yeyote ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake. 33Jihadharini! Kesheni! Kwa maana hamjui wakati ule utakapowadia. 3413:34 Mt 25:14Ni kama mtu anayesafiri. Anaiacha nyumba yake na kuwaachia watumishi wake kuiangalia, kila mtu na kazi yake, kisha akamwamuru yule bawabu aliye mlangoni akeshe.

3513:35 Mt 24:42, 44“Basi kesheni kwa sababu hamjui ni lini mwenye nyumba atakaporudi: iwapo ni jioni, au ni usiku wa manane, au alfajiri awikapo jogoo, au mapambazuko. 36Kama akija ghafula, asije akawakuta mmelala. 3713:37 Lk 12:35-40Lile ninalowaambia ninyi, nawaambia watu wote: ‘Kesheni!’ ”