约翰福音 19 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

约翰福音 19:1-42

1于是彼拉多命人鞭打耶稣。 2士兵用荆棘编成冠冕戴在祂头上,又拿紫袍给祂穿上, 3来到祂面前说:“犹太人的王万岁!”然后又用手掌打祂。

4彼拉多又走到外面对众人说:“我把祂带到你们面前,好让你们知道我查不出祂有什么罪。” 5于是,耶稣戴着荆棘冠冕、穿着紫色长袍走出来。彼拉多对众人说:“你们看这个人!”

6祭司长和差役一看见耶稣,就喊道:“把祂钉在十字架上!把祂钉在十字架上!”

彼拉多说:“你们自己把祂带去钉十字架吧!因为我查不出祂有什么罪。”

7犹太人回答说:“我们有律法,按照那律法,祂理当被处死,因为祂自称是上帝的儿子。”

8彼拉多听了这话,更加害怕, 9又将耶稣带回总督府,问祂:“你到底是从哪里来的?”但耶稣没有回答。

10彼拉多说:“你不回答我吗?难道你不知道我有权释放你,也有权把你钉在十字架上吗?”

11耶稣回答说:“若非从天上赐下权柄给你,你根本无权处置我。因此,把我交给你的那人罪更大。”

12从那时起,彼拉多想要释放耶稣,可是犹太人却一直喊叫:“你如果释放这个人,就不是凯撒的忠臣19:12 “忠臣”希腊文是“朋友”。。凡自以为王的,就是背叛凯撒。”

13彼拉多听了这话,就带着耶稣来到一个地方,名叫“铺石地”,希伯来话叫厄巴大彼拉多在那里开庭审判祂。 14那天正是逾越节的预备日,大约正午,彼拉多犹太人说:“看,你们的王!”

15众人喊道:“除掉祂!除掉祂!把祂钉在十字架上!”

彼拉多说:“我可以把你们的王钉在十字架上吗?”

祭司长答道:“除了凯撒,我们没有别的王!”

16于是,彼拉多将耶稣交给他们去钉十字架,他们就把耶稣带走了。

钉十字架

17耶稣背着自己的十字架出来,前往髑髅地19:17 可能当地的石灰岩地形看起来像一具骷髅头,故此得名。,那地方希伯来话叫各各他18他们在那里把耶稣钉在十字架上。同时还钉了两个人,一边一个,耶稣在当中。 19彼拉多写了一个告示,安在十字架上,上面写着:“犹太人的王,拿撒勒人耶稣。” 20因为耶稣被钉十字架的地方离城不远,告示上面的字是用希伯来罗马希腊三种文字写的,所以很多犹太人读了上面的字。

21犹太人的祭司长对彼拉多说:“不要写‘犹太人的王’,应该写‘这人自称是犹太人的王’。”

22彼拉多说:“我写了就写了。”

23士兵把耶稣钉在十字架上,又把祂的衣服分成四份,每人一份。剩下的内衣从上到下是一块布,没有缝口。 24他们就商量说:“不要撕破它,让我们抽签决定给谁吧。”19:24 诗篇22:18这件事是要应验圣经上的话:“他们分了我的外衣,又为我的内衣抽签。”士兵果然这样做了。

25耶稣的十字架旁边站着祂母亲、祂母亲的姊妹、革罗罢的妻子玛丽亚抹大拉玛丽亚26耶稣看见祂的母亲和祂爱的门徒都站在旁边,就对母亲说:“女士,看啊,他是你的儿子。” 27然后对那门徒说:“看啊,她是你的母亲。”从那天起,那个门徒就把她接到自己家里去了。

耶稣之死

28之后,耶稣知道一切都完成了,就说:“我渴了。”这是要应验圣经上的话。 29那里有一个器皿盛满了酸酒。有人用海绵蘸满了酸酒,绑在牛膝草上送到祂嘴边, 30耶稣喝了那酸酒,然后说:“成了!”就垂下头来,将灵魂交给了上帝。

31因为那天是预备日,第二天的安息日是个大日子,为了避免在安息日有尸首留在十字架上,犹太人便求彼拉多叫人打断他们的腿,把他们搬走。 32于是,士兵上前把与耶稣同钉十字架的两个人的腿都打断了。 33但是他们来到耶稣那里时,发现祂已经死了,就没有打断祂的腿, 34只是有一个士兵用矛刺了一下祂的肋旁,顿时有血和水流了出来。 35看见这事的人为此做见证,他的见证是真实的,他知道自己所说的是事实,好让你们可以相信。 36这些事的发生是为了应验圣经上的话:“祂的骨头一根也不会折断。”19:36 出埃及记12:46民数记9:12诗篇34:20 37还有经文说:“他们必仰望自己所刺的那位。”19:37 撒迦利亚书12:10

安葬耶稣

38事后,有一个名叫约瑟亚利马太人请求彼拉多让他为耶稣收尸。他因为畏惧犹太人,只是暗中做耶稣的门徒。彼拉多批准后,他就把耶稣的遗体领去。 39曾经夜访耶稣的尼哥德慕也来了,他带来了没药和沉香调成的香料,重约三十四公斤。 40他们按照犹太人殡葬的习俗,用细麻布加上香料把耶稣的遗体裹好。 41在耶稣被钉十字架的地方有一个园子,里边有一座新坟墓,从来没有安葬过人。 42因为那天是犹太人的预备日,这座新坟墓也在附近,他们就把耶稣安放在那里。

Kiswahili Contemporary Version

Yohana 19:1-42

Yesu Ahukumiwa Kusulubiwa

(Mathayo 27:15-31; Marko 15:6-20; Luka 23:13-25)

119:1 Kum 25:3; Mt 27:26Ndipo Pilato akamtoa Yesu akaamuru apigwe mijeledi. 2Askari wakasokota taji ya miiba, wakamvika Yesu kichwani. Wakamvalisha joho la zambarau. 319:3 Mt 27:29; Yn 18:22Wakawa wanapanda pale alipo tena na tena, wakisema, “Salamu! Mfalme wa Wayahudi!” Huku wakimpiga makofi usoni.

419:4 Yn 18:38; 19:6; Lk 23:4Pilato akatoka tena nje akawaambia wale waliokusanyika, “Tazameni, namkabidhi Yesu kwenu kuwajulisha kwamba mimi sikumwona ana hatia.” 519:5 Yn 19:2Kwa hiyo Yesu akatoka nje akiwa amevaa ile taji ya miiba na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, “Tazameni, huyu hapa huyo mtu!”

619:6 Mdo 3:13; Yn 19:4; Lk 23:4Wale viongozi wa makuhani na maafisa walipomwona, wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe! Msulubishe!”

Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi mkamsulubishe, mimi sioni hatia juu yake.”

719:7 Law 24:16; Mt 26:63-66; Yn 5:18Wayahudi wakamjibu, “Sisi tunayo sheria na kutokana na sheria hiyo, hana budi kufa kwa sababu yeye alijiita Mwana wa Mungu.”

8Pilato aliposikia haya, akaogopa zaidi. 919:9 Yn 18:33; Mk 14:61Akaingia tena ndani ya jumba la kifalme, akamuuliza Yesu, “Wewe umetoka wapi?” Lakini Yesu hakumjibu. 10Pilato akamwambia, “Wewe unakataa kuongea na mimi? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukuachia huru au kukusulubisha?”

1119:11 Rum 13:1; Yn 18:28-30; Mdo 3:13Ndipo Yesu akamwambia, “Wewe hungekuwa na mamlaka yoyote juu yangu kama hungepewa kutoka juu. Kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako ana hatia ya dhambi iliyo kubwa zaidi.”

1219:12 Lk 23:2Tangu wakati huo, Pilato akajitahidi kutafuta njia ya kumfungua Yesu, lakini Wayahudi wakazidi kupiga kelele wakisema, “Ukimwachia huyu mtu, wewe si rafiki wa Kaisari. Mtu yeyote anayedai kuwa mfalme anampinga Kaisari.”

1319:13 Mt 27:19; Yn 5:2Pilato aliposikia maneno haya akamtoa Yesu nje tena akaketi katika kiti chake cha hukumu, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe, kwa Kiebrania paliitwa Gabatha19:13 Gabatha ni neno la Kiebrania ambalo maana yake ni Sakafu ya jiwe; ni mahali pa wazi palipoinuliwa ambako palitumika kama mahakama. 1419:14 Mt 27:62; Mk 15:25Basi ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, yapata kama saa sita hivi.

Pilato akawaambia Wayahudi, “Huyu hapa mfalme wenu!”

1519:15 Yn 19:6Wao wakapiga kelele, “Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!”

Pilato akawauliza, “Je, nimsulubishe mfalme wenu?”

Wale viongozi wa makuhani wakamjibu, “Sisi hatuna mfalme mwingine ila Kaisari.”

1619:16 Mt 27:26; Mk 15:15Ndipo Pilato akamkabidhi Yesu kwao ili wamsulubishe.

Kusulubiwa Kwa Yesu

(Mathayo 27:32-44; Marko 15:21-32; Luka 23:26-43)

Kwa hiyo askari wakamchukua Yesu. 1719:17 Mwa 22:6; Lk 14:27; 23:33; Yn 5:2Yesu, akiwa ameubeba msalaba wake, akatoka kuelekea mahali palipoitwa Fuvu la Kichwa (kwa Kiebrania ni Golgotha). 1819:18 Lk 23:32Hapo ndipo walipomsulubisha. Pamoja naye walisulubisha watu wengine wawili, mmoja kila upande wake, naye Yesu katikati.

1919:19 Mk 1:24; 14:21Pilato akaamuru tangazo liandikwe na liwekwe juu kwenye msalaba wa Yesu, likasema: “Yesu wa Nazareti, Mfalme wa Wayahudi.” 2019:20 Ebr 13:12Kwa kuwa mahali hapo Yesu aliposulubiwa palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi walisoma maandishi haya yaliyokuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kiyunani na Kilatini. 2119:21 Yn 19:14Viongozi wa makuhani wa Wayahudi wakapinga, wakamwambia Pilato, “Usiandike ‘Mfalme wa Wayahudi,’ bali andika kwamba mtu huyu alisema yeye ni mfalme wa Wayahudi.”

22Pilato akawajibu, “Nilichokwisha kuandika, nimeandika!”

Mavazi Ya Yesu Yagawanywa

2319:23 Mt 27:35; Mk 15:24; Lk 23:34Askari walipokwisha kumsulubisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini. 2419:24 Yn 19:28, 36, 37; Mt 1:22; Za 22:18Wakaambiana, “Tusilichane ila tulipigie kura ili kuamua ni nani atalichukua.”

Hili lilitukia ili Maandiko yapate kutimizwa yale yaliyosema,

“Wanagawana nguo zangu,

na vazi langu wanalipigia kura.”

Hayo ndiyo waliyoyafanya wale askari.

2519:25 Mk 15:40, 41; Lk 23:49; Mt 12:46; Yn 13:23Wakati huo huo karibu na msalaba wa Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada wa mamaye, na Maria mke wa Klopa, na Maria Magdalene. 2619:26 Mt 12:46; Yn 13:23Yesu alipomwona mama yake mahali pale pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wamesimama karibu, akamwambia mama yake, “Mwanamke, huyo hapo ndiye mwanao,” 2719:27 Yn 1:11; 16:32kisha akamwambia yule mwanafunzi, “Nawe huyo hapo ndiye mama yako.” Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Yesu nyumbani kwake.

Kifo Cha Yesu

(Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Luka 23:44-49)

2819:28 Za 69:21; Yn 19:30; 13:1; 19:24, 36, 37; Mt 1:22Baada ya haya, Yesu hali akijua kuwa mambo yote yamemalizika, alisema ili kutimiza Maandiko, “Naona kiu.” 2919:29 Za 69:21; Mt 27:48Hapo palikuwa na bakuli lililojaa siki. Kwa hiyo wakachovya sifongo kwenye hiyo siki, wakaiweka kwenye ufito wa mti wa hisopo, wakampelekea mdomoni. 3019:30 Lk 12:50Baada ya kuionja hiyo siki, Yesu akasema, “Imekwisha.” Akainamisha kichwa chake, akaitoa roho yake.

Yesu Achomwa Mkuki Ubavuni

3119:31 Yn 19:42; Mk 15:42; Kum 21:23Kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, Wayahudi hawakutaka miili ibaki msalabani siku ya Sabato, hasa kwa kuwa hiyo Sabato ingekuwa Sikukuu. Wakamwomba Pilato aamuru miguu ya wale waliosulubiwa ivunjwe ili wafe haraka miili iondolewe kwenye misalaba. 3219:32 Yn 19:18Kwa hiyo askari wakaenda wakavunja miguu ya mtu wa kwanza aliyesulubiwa pamoja na Yesu na yule mwingine pia. 33Lakini walipomkaribia Yesu, wakaona ya kuwa amekwisha kufa, hivyo hawakuvunja miguu yake. 3419:34 Zek 12:10; Ufu 1:7; 1Yn 5:6, 8Badala yake mmoja wa wale askari akamchoma mkuki ubavuni na mara pakatoka damu na maji. 3519:35 Lk 24:48; 15:27; 21:24Mtu aliyeona mambo hayo ndiye alitoa ushuhuda, nao ushuhuda wake ni kweli. Anajua kuwa anasema kweli, naye anashuhudia ili pia nanyi mpate kuamini. 3619:36 Yn 19:24, 28, 37; Mt 1:22; Kut 12:46; Hes 9:12; Za 34:20Kwa maana mambo haya yalitukia ili Maandiko yapate kutimia, yale yasemayo, “Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.” 3719:37 Zek 12:10; Ufu 1:7Tena Andiko lingine lasema, “Watamtazama yeye waliyemchoma.”

Maziko Ya Yesu

(Mathayo 27:57-61; Marko 15:42-47; Luka 23:50-56)

38Baada ya mambo haya, Yosefu wa Arimathaya, aliyekuwa mfuasi wa Yesu, ingawa kwa siri kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi, alimwomba Pilato ruhusa ili kuuchukua mwili wa Yesu. Pilato alimruhusu, hivyo akaja, akauchukua. 3919:39 Yn 3:1; 7:50Naye Nikodemo, yule ambaye kwanza alimwendea Yesu usiku, akaja, akaleta mchanganyiko wa manemane na manukato, yenye uzito wa zaidi ya kilo thelathini19:39 Zaidi ya kilo 30; tafsiri nyingine zinasema ratili 100, na nyingine ratili 75, ambazo ni kama kilo 34. 4019:40 Ebr 13:12Wakauchukua mwili wa Yesu, wakaufunga katika sanda ya kitani safi pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi. 41Basi palikuwa na bustani karibu na mahali pale aliposulubiwa, na pale ndani ya ile bustani palikuwa na kaburi jipya, ambalo halikuwa limezikiwa mtu bado. 42Kwa hiyo, kwa kuwa ilikuwa siku ya Wayahudi ya Maandalio, nalo kaburi hilo lilikuwa karibu, wakamzika Yesu humo.