约珥书 2 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

约珥书 2:1-32

耶和华审判的日子

1你们要在锡安吹响号角,

在我的圣山上发出警讯,

此地的居民都要颤抖,

因为耶和华的日子将要来临,

已经近了。

2那是昏暗阴沉的日子,

是乌云密布的日子。

来了一支空前绝后、强盛无比的大军,

它们像曙光一样布满山岭。

3它们前面有燎原之火,

后面有熊熊烈焰。

它们到来之前,

大地就像伊甸园;

它们过去之后,

大地变成荒凉的旷野。

地上的一切都逃不过这一场浩劫。

4它们的形状像马,

疾驰如战马,

5在山岭上跳跃奔腾,

如隆隆战车,

好像烈火吞噬干草的声音,

又如大军列阵备战。

6百姓一看到它们,就惊慌失措,

面如死灰。

7它们快速奔跑像勇士,

攀登城墙如战士,

有条不紊地前进。

8队伍整齐,各行其道,

长驱直入,势不可挡。

9它们冲向城邑,蹿上城墙,

爬进房屋,

如盗贼般破窗而入。

10所到之处,

天摇地动,

日月昏暗,

星辰无光。

11耶和华向祂的军队发号施令,

祂的队伍不计其数,

执行祂命令的是劲旅。

耶和华的日子伟大而可畏,

谁能承受得住呢?

呼吁人民悔改

12耶和华说:

“现在你们要禁食、哭泣、哀号,

全心回转归向我。”

13你们要撕心般地痛悔,

而不是撕裂衣服。

归向你们的上帝耶和华吧,

因为祂有恩典、好怜悯,

不轻易发怒,

充满慈爱,

不忍心降灾祸。

14或许祂转念心生怜悯,

给你们留下祝福,

使你们可以再次向你们的上帝耶和华献上素祭和奠祭。

有谁知道呢?

15要在锡安山吹响号角,

宣布禁食的圣日,

举行庄严的聚会。

16要招聚老人,

聚集孩童和吃奶的婴儿;

要吩咐新郎出洞房、

新娘出内室;

要召集全体人民,

让会众洁净自己。

17让事奉耶和华的祭司站在圣殿门廊和祭坛中间,

哭泣恳求说:

“耶和华啊,

求你顾惜你的子民,

不要让外族人侮辱、

讥笑你的产业说,

‘他们的上帝在哪里呢?’”

再赐祝福

18耶和华笃爱祂的土地,

祂怜悯自己的子民。

19祂回应他们说:

“我必赐五谷、新酒和橄榄油给你们,

使你们饱足,

不再让你们受列国的羞辱。

20我要使北方的军队远离你们,

把他们驱逐到一个干旱荒芜的地方,

把他们的领头部队赶进死海,

再把他们的殿后部队赶进地中海,

那时他们必臭气冲天、

恶味上腾,

因为耶和华为你们行了大事。”

21土地啊,不要害怕,

倒要欢喜快乐;

因为耶和华行了大事。

22田野的走兽啊,不要害怕,

因为青草铺遍了旷野,

树木也结满了果子,

无花果树和葡萄树都结实累累。

23锡安的人民啊,

你们要快乐,

因你们的上帝耶和华而喜乐。

因为祂按时2:23 “按时”希伯来文是“按公义”。降下甘霖,

像从前一样赐给你们秋雨和

春雨。

24麦场必堆满五谷,

酒槽里的酒和油槽里的油必满溢。

25“我派蝻虫、蚱蜢、蚂蚱

和蝗虫大军在那些年所吃掉的,

我要补偿你们。

26你们必吃得饱足,

并赞美你们的上帝耶和华的名,

因祂为你们行了奇事。

我的子民永远不会再蒙羞。

27这样,你们就知道我在以色列

知道我是你们的上帝耶和华,

除我以外别无他神。

我的子民永远不会再蒙羞。

28“以后,我要将我的灵浇灌所有的人。

你们的儿女要说预言,

老人要做异梦,

青年要见异象。

29在那些日子,

我要将我的灵浇灌我的奴仆和婢女。

30“我要在天上地下行奇事,你们将看见血、火和烟柱。 31太阳要变得昏暗,月亮要变得血红。在耶和华伟大而可畏的日子来临以前,这些事都会发生。 32那时候,凡求告耶和华之名的人都必得救,因为在锡安山,在耶路撒冷城,必有逃脱灾难的人,耶和华所呼召的人必幸存下来,正如耶和华所言。”

Kiswahili Contemporary Version

Yoeli 2:1-32

Jeshi La Nzige

12:1 Hos 10:2, 7; Kut 15:17; Oba 1:15; Sef 1:14-16; Eze 12:23Pigeni tarumbeta katika Sayuni;

pigeni mbiu katika mlima wangu mtakatifu.

Wote waishio katika nchi na watetemeke,

kwa kuwa siku ya Bwana inakuja. Iko karibu,

22:2 Ay 9:7; Isa 8:22; 13:10; Amo 5:18; Kut 10:14; Dan 9:12; Mt 24:21; Eze 34:12siku ya giza na huzuni,

siku ya mawingu na utusitusi.

Kama mapambazuko yasambaavyo

toka upande huu wa milima

hata upande mwingine

jeshi kubwa na lenye nguvu linakuja.

Jambo kama hili halijakuwepo tangu zamani

wala halitakuwepo tena kamwe

kwa vizazi vijavyo.

32:3 Za 97:3; 105:34-35; Kut 10:12-15; Isa 14:17; Zek 7:14; Isa 1:31Mbele yao moto unateketeza,

nyuma yao miali ya moto

inawaka kwa nguvu.

Mbele yao nchi iko kama bustani ya Edeni,

nyuma yao ni jangwa lisilofaa:

hakuna kitu kinachowaepuka.

4Wanaonekana kama farasi;

wanakwenda mbio

kama askari wapanda farasi.

52:5 Ufu 9:9; Isa 5:24; 30:30Wanatoa sauti kama magari ya vita,

wanaporukaruka juu ya vilele vya milima,

kama mlio wa miali ya moto ilayo mabua,

kama jeshi kubwa lililojipanga kwa ajili ya vita.

62:6 Yer 8:21; Isa 13Wanapoonekana, mataifa yanakuwa katika maumivu makuu;

kila uso unabadilika rangi.

72:7 Isa 5:27; Mit 30:27; Ay 16:14Wanashambulia kama wapiganaji wa vita;

wanapanda kuta kama askari.

Wote wanatembea katika safu,

hawapotoshi safu zao.

8Hakuna anayemsukuma mwenzake;

kila mmoja anakwenda mbele moja kwa moja.

Wanapita katika vizuizi

bila kuharibu safu zao.

92:9 Yer 9:21; Kut 10:6Wanaenda kasi kuingia mjini;

wanakimbia ukutani.

Wanaingia ndani ya nyumba;

kwa kuingilia madirishani kama wevi.

102:10 Isa 5:30; 13:10; Za 18:7; 102:26; Ufu 9:2; Ay 9:7; Eze 38:19Mbele yao dunia inatikisika,

anga linatetemeka,

jua na mwezi vinatiwa giza,

na nyota hazitoi mwanga wake tena.

112:11 Isa 2:12; Hes 24:23; Ufu 6:17; 18:8; Sef 2:11; Eze 30:3; Yoe 1:15; Yer 50:34; Mal 3:2; Za 29:3Bwana anatoa mshindo wa ngurumo

mbele ya jeshi lake;

majeshi yake hayana idadi,

ni wenye nguvu nyingi

wale ambao hutii agizo lake.

Siku ya Bwana ni kuu,

ni ya kutisha.

Ni nani anayeweza kuistahimili?

Rarueni Mioyo Yenu

122:12 Kum 4:30; Hos 12:6; Eze 33:11; 1Sam 7:3“Hata sasa,” asema Bwana,

“nirudieni kwa mioyo yenu yote,

kwa kufunga, kwa kulia na kuomboleza.”

132:13 Za 34:18; 51:17; 86:5; Mwa 37:29; Hes 14:6; Kut 34:6; Yon 4:2; Isa 57:15; 2Fal 22:19; Mt 5:3-4; Ay 1:20Rarueni mioyo yenu

na siyo mavazi yenu.

Mrudieni Bwana, Mungu wenu,

kwa maana yeye ndiye mwenye neema

na mwingi wa huruma,

si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo,

huona huruma, hujizuia kuleta maafa.

142:14 Yer 26:3; 31:14; Yn 3:9; Sef 2:3; Isa 65:8; Zek 8:13; Yos 14:12; Amo 5:15; Hag 2:19; Mal 3:10Ni nani ajuaye? Yeye aweza kugeuka na kuwa na huruma

na kuacha baraka nyuma yake:

sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji

kwa ajili ya Bwana Mungu wenu.

152:15 2Nya 20:3; Hes 10:2-3; Yer 36:9Pigeni tarumbeta katika Sayuni,

tangazeni saumu takatifu,

liiteni kusanyiko takatifu.

162:16 Kut 19:10; 2Nya 20:13; 1Kor 7:5; Za 19Wakusanyeni watu,

wekeni wakfu kusanyiko;

waleteni pamoja wazee,

wakusanyeni watoto,

wale wanyonyao maziwa.

Bwana arusi na atoke chumbani mwake

na bibi arusi naye atoke katika chumba chake.

172:17 Eze 8:16; Mt 23:35; Kum 9:26-29; Ay 17:6; Za 42:3; Kut 32:11; Isa 37:20; Yoe 1:13; Isa 22:12Makuhani, ambao wanahudumu mbele za Bwana,

na walie katikati ya ukumbi

wa Hekalu na madhabahu.

Waseme, “Wahurumie watu wako, Ee Bwana.

Usifanye urithi wako kitu cha kudharauliwa,

neno la dhihaka kati ya mataifa.

Kwa nini wasemezane miongoni mwao,

‘Yuko wapi Mungu wao?’ ”

Jibu La Bwana

182:18 Isa 26:11; 42:13; Zek 8:2; 1:14; Kum 32:36; Za 103:13; 72:13Kisha Bwana atakuwa na wivu kwa ajili ya nchi yake

na kuwa na huruma juu ya watu wake.

192:19 Yer 31:12; Eze 34:29; Za 4:7; Law 26:5Bwana atawajibu:

“Ninawapelekea nafaka,

mvinyo mpya na mafuta,

vya kuwatosha ninyi

hadi mridhike kabisa;

kamwe sitawafanya tena

kitu cha kudharauliwa na mataifa.

202:20 Yer 1:14-15; Zek 14:8; Kum 11:24; Kut 10:19; Isa 34:3“Nitafukuza jeshi la kaskazini likae mbali nanyi,

nikilisukuma ndani ya jangwa,

askari wa safu za mbele wakienda

ndani ya bahari ya mashariki

na wale wa safu za nyuma

katika bahari ya magharibi.

Uvundo wake utapaa juu;

harufu yake itapanda juu.”

Hakika ametenda mambo makubwa.

212:21 Sef 3:16-17; Isa 25:1; 29:22; 54:4; 1Yn 4:18Usiogope, ee nchi;

furahi na kushangilia.

Hakika Bwana ametenda mambo makubwa.

222:22 Yoe 1:18-20; Zek 8:12; Za 65:12; Hes 16:14; 1Fal 4:25Msiogope, enyi wanyama pori,

kwa kuwa mbuga za malisho yenu

zinarudia ubichi.

Miti nayo inazaa matunda,

mtini na mzabibu inatoa utajiri wake.

232:23 Hab 3:18; Yak 5:7; Za 28:7; 33:21; Law 26:4Furahini, enyi watu wa Sayuni,

shangilieni katika Bwana Mungu wenu,

kwa kuwa amewapa mvua za vuli

kwa kipimo cha haki.

Anawapelekea mvua nyingi,

mvua ya vuli na ya masika, kama mwanzoni.

242:24 Law 26:10; Mal 3:10; Mit 3:10; Amo 9:13; Yoe 3:18Sakafu za kupuria zitajaa nafaka,

mapipa yatafurika mvinyo mpya na mafuta.

252:25 Kut 14:10; Amo 4:9“Nitawalipa kwa ajili ya miaka ile iliyoliwa na nzige:

parare, madumadu na tunutu,

jeshi langu kubwa ambalo

nililituma katikati yenu.

262:26 Law 23:40; 26:5; Isa 25:1; 29:22; 62:9; Za 126:3; Mik 6:14Mtakuwa na wingi wa vyakula mpaka mshibe,

na mtalisifu jina la Bwana Mungu wenu,

ambaye amefanya maajabu kwa ajili yenu;

kamwe watu wangu hawataaibishwa tena.

272:27 Kut 6:2; Isa 44:8; 45:5; 54:4; Yoe 3:17; Law 26:11; Sef 3:11Ndipo mtakapojua kwamba mimi niko katika Israeli

kwamba mimi ndimi Bwana Mungu wenu,

na kwamba hakuna mwingine;

kamwe watu wangu hawataaibika tena.

Siku Ya Bwana

282:28 Yn 7:38; 11:2; Eze 39:29; Mdo 21:9; Hes 11:17; Gal 3:14; 1Sam 19:20“Hata itakuwa, baada ya hayo,

nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili.

Wana wenu na binti zenu watatabiri,

wazee wenu wataota ndoto,

na vijana wenu wataona maono.

292:29 1Kor 12:13; Gal 3:28; Eze 36:27Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake,

katika siku zile nitamimina Roho wangu.

302:30 Lk 21:11; Mk 13:24-25Nami nitaonyesha maajabu katika mbingu

na duniani:

damu, moto na mawimbi ya moshi.

312:31 Isa 22:5; Mt 24:29; Isa 13:9-10; Mal 3:2; Yer 4:23; Yoe 1:15Jua litageuzwa kuwa giza

na mwezi kuwa mwekundu kama damu,

kabla ya kuja siku ya Bwana

ile kuu na ya kutisha.

322:32 Rum 9:27; 10:13; Oba 1:17; Mik 4:7; 7:18; Isa 11:11; 46:13; Za 106:8; 50:12; Yer 33:3; Mwa 4:26; Mdo 2:21, 39Na kila mtu atakayeliitia

jina la Bwana ataokolewa.

Kwa maana juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu

kutakuwepo wokovu,

kama Bwana alivyosema,

miongoni mwa walionusurika

ambao Bwana awaita.