申命记 5 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

申命记 5:1-33

十诫

1摩西把所有的以色列人召来,对他们说:“以色列人啊,要留心听我今天对你们宣讲的律例和典章,要学习并谨慎遵行。 2我们的上帝耶和华曾在何烈山与我们立约, 3这约不是与我们祖先立的,而是与我们今天还活着的人立的。 4耶和华在山上的烈火中面对面跟你们说话。 5那时,因为你们害怕那烈火,没有到山上去,我就站在耶和华和你们中间,把耶和华的话传给你们。耶和华说:

6“‘我是你的上帝耶和华,曾把你从受奴役之地埃及领出来。

7除我以外,你不可有别的神明。

8不可为自己雕刻神像,不可仿照天上、地上和地底下水中的任何形象造神像, 9不可跪拜它们,也不可供奉它们,因为我——你的上帝耶和华痛恨不贞,我必追讨背弃我之人的罪,从父到子直到三四代。 10但那些爱我、遵守我诫命的人,我必以慈爱待他们,直到千代。

11不可妄用你上帝耶和华的名,违者必被耶和华定罪。

12要遵照你的上帝耶和华的吩咐守安息日为圣日。 13你一周可劳碌工作六天, 14但第七天是你的上帝耶和华的安息日,这一天你和儿女、仆婢、牛驴等牲畜及你那里的外族人不可做任何工,好让仆婢和你一样得到休息。 15要记住,你曾在埃及做奴隶,你的上帝耶和华伸出臂膀,用大能的手把你从那里领出来。因此,你的上帝耶和华吩咐你守安息日。

16要遵照你的上帝耶和华的吩咐孝敬父母,以便在你的上帝耶和华要赐给你的土地上享长寿,蒙祝福。

17不可杀人。

18不可通奸。

19不可偷盗。

20不可作伪证陷害人。

21不可贪恋别人的妻子,不可贪图别人的房屋、田地、仆婢、牛驴,或其他任何物品。’

22“这是耶和华在山上的烈火、乌云和幽暗中高声颁布给你们全体会众的诫命。此外,祂没有说别的。祂把这些话写在两块石版上交给我。 23当时,山上燃烧着烈焰,你们听见声音从黑暗中传来。你们各支派的首领和长老都到我跟前, 24说,‘看啊,我们的上帝耶和华向我们彰显了祂的荣耀和威严,我们听见了祂从火中发出的声音。今天我们已经看见,人听见上帝说话后还能活着。 25但我们何必冒死,被这烈火吞噬呢?我们若再次听到我们的上帝耶和华的声音,必然丧命。 26世上有谁像我们一样,听见永活上帝从火中说话后还能活着呢? 27你近前听我们上帝耶和华所说的话,然后回来把祂的话告诉我们,我们必听从、遵行。’

28“耶和华听见了你们的话,就对我说,‘我听见了民众对你说的话,他们所说的都对。 29但愿他们常常敬畏我,遵从我的一切诫命,以便他们和他们的子孙世世代代可以蒙福。 30你吩咐他们回到自己的帐篷, 31但你要留在我这里,我要把所有的诫命、律例和典章都赐给你,你要把这些传授给众人,使他们可以在我要赐给他们的土地上遵行。’ 32所以,你们要谨遵你们上帝耶和华的吩咐,不可偏离左右。 33你们要遵行你们上帝耶和华的一切吩咐,就可以在你们将要占领的土地上存活、亨通、长久。

Kiswahili Contemporary Version

Kumbukumbu 5:1-33

Amri Kumi

(Kutoka 20:1-17)

15:1 Kut 18:20Mose akawaita Israeli wote, akawaambia:

Ee Israeli, sikilizeni amri na sheria ninazowatangazia leo. Jifunzeni, na mwe na hakika kuzifuata. 25:2 Kut 19:5Bwana Mungu wetu alifanya Agano nasi katika mlima wa Horebu. 35:3 Kum 11:2-7; Hes 26:63-65; Ebr 8:9; Mt 13:17Si kwamba Bwana alifanya Agano na baba zetu, bali alifanya nasi, nasi sote ambao tuko hai hapa leo. 45:4 Kut 19:9, 18-19; 20:22; Kum 4:33, 36; 34:10; Hes 14:4Bwana alisema nanyi uso kwa uso kutoka moto juu ya mlima. 55:5 Gal 3:19; Mwa 3:10; Ebr 12:18-21; Kut 20:18-21; 20:18-21; Hes 16:48; Za 106:23; Yer 30:21(Wakati huo nilisimama kati ya Bwana na ninyi kuwatangazia neno la Bwana, kwa sababu mliogopa ule moto, nanyi hamkupanda mlimani.) Naye Mungu alisema:

65:6 Kut 13:3; 29:46; Law 26:1; Kum 6:4; Za 81:10“Mimi ndimi Bwana Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.

75:7 Kut 20:3“Usiwe na miungu mingine ila mimi.

85:8 Law 26:1; Kum 4:15-16; Za 78:58; 97:7; Kut 20:4; Mdo 17:29Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni au duniani chini au ndani ya maji. 95:9 Hes 26:11; Kut 34:7; Hes 10:35; 14:18; Kut 34:7Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 105:10 Kut 34:2; Hes 14:18; Kum 7:9; Neh 1:5; Yer 32:18; Dan 9:4lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.

115:11 Za 139:20; Law 19:12; Kum 10:20; Mt 5:33-37Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, kwa kuwa Bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.

125:12 Kut 16:23-30; 31:13; Mk 2:27-28; Kut 20:8Adhimisha siku ya Sabato na kuiweka takatifu, kama Bwana Mungu wako alivyokuagiza. 13Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote. 145:14 Mwa 2:2; Mt 12:2; Mk 2:17; Ebr 4:4; Ay 31:13; Yer 34:9-11; 17:21-24Lakini siku ya Saba ni Sabato kwa Bwana, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au mtumishi wa kike, wala ngʼombe wako, punda wako au mnyama wako yeyote, wala mgeni aliyeko malangoni mwako, ili kwamba mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika kama wewe. 155:15 Mwa 15:13; Kut 6:1; Za 108:6; Yer 32:21; Kum 4:34Kumbuka mlikuwa watumwa huko Misri, na Bwana Mungu wenu aliwatoa huko kwa mkono wenye nguvu na kwa mkono ulionyooshwa. Kwa hiyo Bwana Mungu wako amekuagiza kuiadhimisha siku ya Sabato.

165:16 Mal 1:6; Kut 21:17; Law 19:3; Eze 22:7; Mt 15:4; 19:19; Mk 7:10; 10:19; Lk 18:20; Efe 6:2-3; Kum 4:40; 11:9; Mit 3:1-2Waheshimu baba yako na mama yako, kama Bwana Mungu wako alivyokuagiza, ili siku zako zipate kuwa nyingi na kufanikiwa katika nchi Bwana Mungu wako anayokupa.

175:17 Mwa 9:6; Law 24:17; Mhu 3:3; Yer 40:15; 41:3; Mt 5:21-22; 19:19; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11Usiue.

185:18 Law 20:10; Mt 5:27-30; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11Usizini.

195:19 Law 19:11; Mt 19:19; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9Usiibe.

205:20 Kut 23:1; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20Usimshuhudie jirani yako uongo.

215:21 Rum 7:7; 13:9Usitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ngʼombe au punda wake, wala kitu chochote cha jirani yako.”

225:22 Kut 20:21; 24:12; 31:18; Kum 4:13Hizi ndizo amri alizozitangaza Bwana kwa sauti kubwa kwa kusanyiko lenu lote huko mlimani kutoka kwenye moto, wingu na giza nene, wala hakuongeza chochote zaidi. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, naye akanipa mimi.

Woga Wa Watu Mlimani

(Kutoka 20:18-21)

235:23 Kut 3:16Mliposikia sauti kutoka kwenye giza, mlima ulipokuwa ukiwaka moto, viongozi wenu wote wa makabila yenu na wazee wenu walinijia mimi. 245:24 Kum 4:34; 8:5; 11:2; Isa 53:4; Kum 3:24; Kut 19:19Nanyi mkasema, “Bwana Mungu wetu ametuonyesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kwenye moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye. 255:25 Kut 20:18-19; Kum 18:16; Ebr 12:19Lakini sasa, kwa nini tufe? Moto huu mkubwa utatuteketeza sisi na tutakufa kama tukiendelea kusikia sauti ya Bwana Mungu wetu zaidi. 265:26 Kut 33:20; Kum 4:33; Amu 6:22-23; 13:22; Isa 6:5Ni mtu yupi mwenye mwili ambaye amewahi kuisikia sauti ya Mungu aliye hai akizungumza kutoka kwenye moto, kama sisi tulivyoisikia, naye akaishi? 275:27 Kut 19:8; 24:7Sogea karibu usikie yale yote asemayo Bwana Mungu wetu. Kisha utuambie chochote kile ambacho Bwana Mungu wetu anakuambia. Tutasikiliza na kutii.”

285:28 Kum 18:17Bwana aliwasikia wakati mlipozungumza nami, na Bwana akaniambia, “Nimesikia kile hawa watu walichokuambia. Kila kitu walichokisema ni kizuri. 295:29 Za 81:8, 13; Yos 22:5; Za 78:7; Kum 4:1-40; 12:25; 22:7; Isa 48:18; Kum 12:25; Yer 44:4; Mt 23:37; Lk 19:42; 2Kor 5:20; 6:1; 7:1; Ebr 12:25; Yn 15:14; Ufu 22:14Laiti kama mioyo yao ingekuwa na mwelekeo wa kuniogopa na kuzishika amri zangu zote daima, ili kwamba wafanikiwe wao pamoja na watoto wao milele!

305:30 Mal 4:4; Gal 3:19“Nenda uwaambie warudi kwenye mahema yao. 315:31 Kut 24:12Lakini wewe baki hapa pamoja nami ili niweze kukupa maagizo yote, amri na sheria ambazo utawafundisha wazifuate katika nchi ninayokwenda kuwapa waimiliki.”

325:32 Kum 4:29; 10:12; 17:11, 20; 28:14; Yos 1:7; 1Fal 15:5; 2Fal 22:2; Mit 4:27; Kum 10:12; Za 119:6; Mhu 8:12; 1Tim 4:8; Efe 6:3Hivyo kuweni waangalifu kuyafanya yale Bwana Mungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto. 335:33 Isa 3:10; Yer 7:23; 38:20; Lk 1:6; Kum 4:40Fuateni yale yote ambayo Bwana Mungu wenu aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.