撒母耳记下 24 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

撒母耳记下 24:1-25

大卫统计人口

1耶和华又向以色列人发怒,祂促使大卫来对付他们,让大卫统计以色列犹大的人口。 2大卫对统领军队的约押说:“你去走遍以色列各支派,从别示巴,统计以色列犹大的人口,让我知道国民的数目。” 3约押说:“我主我王,愿你的上帝耶和华使国民的人数比现在增加百倍,让你亲眼看到。但我主我王为什么要做这事呢?” 4大卫不听约押和其他将领的规劝。他们只好去统计以色列的人数。 5他们过了约旦河,在谷中亚罗珥城南面安营,又经过迦得前往雅谢6然后,他们到基列他停·合示地区、但·雅安,绕到西顿7再去泰尔的堡垒及希未人和迦南人的城邑。最后,他们到了犹大南部的别示巴8他们花了九个月零二十天的时间,走遍全国,最后回到耶路撒冷9约押把统计的人数奏告王:“以色列有八十万英勇的刀兵,犹大有五十万。”

10大卫统计了人口以后,内心不安,就对耶和华说:“我做这事犯了大罪。耶和华啊,求你赦免仆人的罪,我做了极其愚昧的事。” 11大卫第二天早上起来,耶和华对大卫的先见迦得先知说: 12“你去告诉大卫,耶和华说,‘我有三样灾祸,你可以选择让我降哪一样给你。’” 13迦得就来见大卫,对他说:“你愿意国内有七年饥荒呢?还是被敌人追杀三个月呢?还是国内发生三天瘟疫呢?请你考虑好后告诉我,我好回复那差我来的。” 14大卫说:“我实在为难!不过我宁愿落在耶和华的手中,也不愿落在人的手中,因为耶和华有极大的怜悯。”

15于是,耶和华在以色列降下瘟疫,从那天早晨一直持续到所定的时间,从别示巴共有七万人死亡。 16当天使准备伸手毁灭耶路撒冷的时候,耶和华心生怜悯,就对灭命天使说:“够了,住手吧!”当时,耶和华的天使正站在耶布斯亚劳拿的麦场上。 17大卫看见灭命天使,就对耶和华说:“是我犯了罪,做了恶事,这些百姓有什么过错呢?愿你的手惩罚我和我的家族。”

18就在那天,迦得来见大卫,对他说:“你要去耶布斯亚劳拿的麦场,在那里为耶和华建一座坛。” 19大卫就照耶和华借迦得所说的话去了麦场。 20亚劳拿看见王及他的臣仆来了,就上前俯伏在地,向王下拜, 21说:“我主我王到仆人这里有什么事?”大卫说:“我要买你的麦场,好在这里为耶和华筑一座坛,使民中的瘟疫止息。” 22亚劳拿说:“我主我王喜欢什么,就拿去献祭吧。这里有牛可以作燔祭,还有打麦的器具和牛轭可以作柴。 23王啊,仆人亚劳拿愿意把这一切都献给你,愿你的上帝耶和华悦纳你。” 24王却说:“不可,我一定要出钱买,我不要用白白得来之物作为燔祭献给我的上帝耶和华。”大卫就用十两银子买了亚劳拿的麦场和牛。 25大卫在那里为耶和华建了一座坛,献上燔祭和平安祭,耶和华垂听了他的祷告,瘟疫就在以色列止住了。

Kiswahili Contemporary Version

2 Samweli 24:1-25

Daudi Ahesabu Wapiganaji

(1 Nyakati 21:1-27)

124:1 Yos 9:15; Ay 1:6; Zek 3:1; Kut 30:12; 1Nya 27:23; 2Sam 16:10; 21:11; 1Fal 22:22; 1Nya 21:1; Yak 1:13Hasira ya Bwana ikawaka tena dhidi ya Israeli, naye akamchochea Daudi dhidi yao, akisema, “Nenda ukawahesabu Israeli na Yuda.”

224:2 2Sam 20:23; 3:10; 2Nya 2:17; 17:14; 25:5; Amu 20:1; Mwa 26:4; Kum 8:13-14; 2Nya 32:25-26; Mit 18:12; 29:23; Yer 17:5Kwa hiyo mfalme akamwambia Yoabu, pamoja na majemadari wa jeshi aliokuwa nao, “Nendeni kwa makabila yote ya Israeli kuanzia Dani hadi Beer-Sheba na mwandikishe watu wapiganaji, ili niweze kujua idadi yao.”

324:3 2Sam 2:18; Kum 1:11Lakini Yoabu akamjibu mfalme, “Bwana Mungu wako na azidishe jeshi mara mia, nayo macho ya bwana wangu mfalme na yaone hili. Lakini kwa nini bwana wangu mfalme anataka kufanya kitu cha namna hii?”

424:4 1Nya 21:4; Mhu 8:4; Mdo 5:29Hata hivyo, neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu pamoja na majemadari wa jeshi, kwa hiyo wakaondoka mbele ya mfalme kuandikisha wapiganaji wa Israeli.

524:5 Yos 13:9; Hes 21:32; Kum 2:36Baada ya kuvuka Yordani, walipiga kambi karibu na Aroeri, kusini ya mji ulioko kwenye bonde jembamba, ndipo wakipitia Gadi, wakaenda hadi Yazeri. 624:6 Mwa 10:19; Amu 1:31; Yos 19:28; Amu 18:28-29Walikwenda hadi Gileadi na pia eneo la Tahtimu-Hodshi, wakaendelea hadi Dani-Yaani na kuzunguka kuelekea Sidoni. 724:7 Yos 19:29; Kut 3:8; Kum 1:31; Yos 11:3; Mwa 21:21-33Kisha wakaenda kuelekea ngome ya Tiro pamoja na miji yote ya Wahivi na ya Wakanaani. Mwishoni, walikwenda mpaka Beer-Sheba katika Negebu ya Yuda.

8Baada ya kupita katika nchi nzima, walirudi Yerusalemu baada ya miezi tisa na siku ishirini.

924:9 Hes 1:44-46; 1Nya 21:5Yoabu akatoa hesabu ya wapiganaji kwa mfalme: Katika Israeli kulikuwako watu 800,000 wenye uwezo wa kupigana, na katika Yuda watu 500,000.

1024:10 1Sam 24:5; Hes 22:34; 12:11; 2Sam 12:13; 1Sam 13:13; Mit 18:4; 1Yn 3:20; 1Nya 21:8; Ay 33:27-28; Za 25:11Dhamiri ya Daudi ilishtuka baada ya kuwahesabu wapiganaji, naye akamwambia Bwana, “Nimefanya dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. Ee Bwana, sasa ninakusihi, ondoa hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.”

1124:11 1Sam 22:5; 9:9; 1Nya 29:29Kabla Daudi hajaamka kesho yake asubuhi, neno la Bwana lilikuwa limemjia Gadi nabii, aliyekuwa mwonaji wa Daudi, kusema: 12“Nenda ukamwambie Daudi, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana: Ninakupa wewe uchaguzi wa mambo matatu. Nichagulie mojawapo nitakalotenda dhidi yako.’ ”

1324:13 Kum 28:28-48; 32:24; Eze 14:21; Kut 5:3; 30:12; Law 26:25; Kum 28:21-28, 35; 1Nya 21:12Basi Gadi akaenda kwa Daudi na kumwambia, “Je, ije njaa ya miaka mitatu katika nchi yako? Au miezi mitatu ya kukimbia adui zako wakikufuatia? Au siku tatu za tauni katika nchi yako? Basi sasa, fikiri juu ya hilo na uamue jinsi nitakavyomjibu huyo aliyenituma.”

1424:14 Neh 9:28; Za 4:1; 51:1; 103:8-13; Isa 54:7; 55:7; Yer 33:8; 42:12; Dan 9:9; Isa 47:6; Zek 1:15Daudi akamjibu Gadi, “Nitataabika sana. Afadhali tuangukie mikononi mwa Bwana, kwa maana rehema zake ni kuu, lakini usiniache nianguke mikononi mwa wanadamu.”

1524:15 1Nya 24:24; 21:14; 27:24Basi Bwana akatuma tauni katika Israeli kuanzia asubuhi mpaka mwisho wa muda ulioamriwa, wakafa watu 70,000 kuanzia Dani hadi Beer-Sheba. 1624:16 Mwa 6:6; 16:7; 19:13; Kut 12:23; Mdo 12:23; 1Nya 21:15; Za 104:4; 1Sam 15:11; Za 78:38; Yer 18:5-10; Yoe 2:13; Yon 3:10Malaika aliponyoosha mkono wake ili kuangamiza Yerusalemu, Bwana akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anawadhuru watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa Bwana alikuwa kwenye sakafu ya kupuria ya Arauna,24:16 Pia anaitwa Ornani kwa Kiebrania. Myebusi.

1724:17 Za 74:1; 100:3; Yer 49:20; Mwa 18:23; Yon 1:12; 1Nya 21:17Ikawa Daudi alipomwona huyo malaika aliyekuwa akiwaua watu, akamwambia Bwana, “Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kukosa. Hawa ni kondoo tu. Wamefanya nini? Mkono wako uwe juu yangu na nyumba yangu.”

Daudi Ajenga Madhabahu

1824:18 Mwa 22:2; 2Nya 3:1Siku hiyo Gadi akamwendea Daudi na kumwambia, “Panda ukamjengee Bwana madhabahu kwenye sakafu ya kupuria ya Arauna Myebusi.” 19Kwa hiyo Daudi akakwea kama vile Bwana alivyokuwa ameamuru kwa kinywa cha Gadi. 20Arauna alipotazama na kumwona mfalme na watu wake wakija kumwelekea, alitoka nje na kusujudu mbele ya mfalme kifudifudi, akiuinamisha uso wake ardhini.

2124:21 Hes 16:44-50; Mwa 23:8Arauna akasema, “Mbona bwana wangu mfalme amekuja kwa mtumishi wake?”

Daudi akajibu, “Kununua sakafu yako ya kupuria, ili niweze kumjengea Bwana madhabahu, ili tauni iliyo katika watu iondolewe.”

2224:22 1Sam 6:14; 1Fal 19:21Arauna akamwambia Daudi, “Bwana wangu mfalme na achukue chochote kinachompendeza na akitoe sadaka. Hapa kuna maksai kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia kuna miti ya kupuria na nira za ngʼombe kwa ajili ya kuni. 2324:23 Mwa 23:11; Eze 20:40-41; Za 20:3; 119:108; 1Pet 2:5Ee mfalme, Arauna anatoa vyote hivi kwa mfalme.” Pia Arauna akamwambia mfalme, “Bwana Mungu wako na akukubali.”

2424:24 Mal 1:13-14; Mwa 23:16Lakini mfalme akamjibu Arauna, “La hasha, nasisitiza kuvilipia. Sitatoa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana Mungu wangu isiyonigharimu chochote.”

Kwa hiyo Daudi akanunua ile sakafu ya kupuria nafaka na maksai, akazilipia shekeli hamsini za fedha.24:24 Shekeli 50 za fedha ni sawa na gramu 600. 2524:25 1Sam 7:17; 2Sam 21:14; 1Nya 21:28; 22:1; 2Sam 21:14; 2Nya 33:13Kisha Daudi akamjengea Bwana madhabahu mahali hapo, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Kisha Bwana akajibu kwa ajili ya nchi, nayo tauni ikakoma katika Israeli.