撒母耳记上 28 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

撒母耳记上 28:1-25

扫罗求问巫婆

1非利士人召集大军与以色列人交战。亚吉大卫说:“你应该明白,你和部下要随我一起出战。” 2大卫答道:“仆人愿意效劳。”亚吉说:“很好!你就终生做我的护卫吧。” 3那时撒母耳已经死了,以色列举国都为他哀悼,把他葬在他的家乡拉玛。当时,扫罗已把所有占卜和行巫术的都逐出了以色列4非利士人集合起来,在书念扎营,扫罗率领以色列军队在基利波扎营。 5扫罗看见非利士军队声势浩大,吓得胆战心惊, 6就求问耶和华,但耶和华没有借着梦、乌陵或先知回答他。 7于是,扫罗命令臣仆找一个巫婆来,好求问她。臣仆在隐·多珥找到一个巫婆。

8扫罗乔装打扮,由两个人陪同乘夜赶到那妇人家里,说:“请你用法术把我要求问的亡灵招上来吧。” 9妇人对他说:“你知道扫罗铲除了国内占卜的和行巫术的,你为何来陷害我,置我于死地?” 10扫罗凭耶和华向妇人起誓,说:“我凭永活的耶和华起誓,你必不会因为此事而受到惩罚。” 11妇人问道:“你想让我招谁上来呢?”扫罗答道:“招撒母耳上来。” 12妇人看见了撒母耳,就惊叫起来,对扫罗说:“你是扫罗,你为什么骗我呢?” 13扫罗王对她说:“不要害怕,你看见什么了?”妇人说:“我看见一个灵从地里上来。” 14扫罗说:“他是什么模样?”妇人说:“是个身披长袍的老人。”扫罗知道是撒母耳,便俯伏在地,向他下拜。 15撒母耳扫罗说:“你为什么打扰我,招我上来呢?”扫罗答道:“我深陷困境,非利士人与我们交战,上帝也撇弃了我,不再借着先知或梦来回答我。因此,我只好招你上来,好告诉我该怎么办。” 16撒母耳说:“既然耶和华已经离弃了你,与你为敌,你为什么还来问我? 17耶和华应验了祂借着我所说的预言,祂已把你的国权夺去,交给了你的同胞大卫18耶和华今天这样对待你,是因为你没有听从祂的吩咐,没有把祂憎恶的亚玛力人灭绝。 19耶和华必把你和以色列人交在非利士人手里,明天你和你的儿子们必跟我在一起了。耶和华必把以色列的军队交在非利士人手里。”

20扫罗听了撒母耳的话,顿时吓得浑身僵直,倒在地上。他因一天一夜没有进食,已经毫无力气。 21妇人到扫罗跟前,看见他惊恐万分,就对他说:“婢女冒着生命危险服从你的命令,照你的吩咐做了。 22现在,请你听婢女的话,让我给你一些食物吃,你好有体力赶路。” 23扫罗不肯,说:“我不吃。”他的随从和妇人再三劝告,他才同意了,从地上起来坐到床上。 24妇人连忙宰了家中一只小肥牛,又和面烤了无酵饼, 25摆在扫罗和他的随从面前,他们吃完后,当晚就离开了。

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 28:1-25

Sauli Na Mchawi Wa Endori

128:1 1Sam 29:1-2Siku zile Wafilisti wakakusanya majeshi yao ili kupigana vita dhidi ya Israeli. Akishi akamwambia Daudi, “Lazima ujue kuwa wewe pamoja na watu wako mtafuatana nami kwenda vitani.”

228:2 Rum 12:9Daudi akasema, “Ndipo wewe mwenyewe utakapojionea jambo ambalo mtumishi wako anaweza kufanya.”

Akishi akamjibu Daudi, “Vyema sana, mimi nitakufanya uwe mlinzi wangu daima.”

328:3 1Sam 25:1; 7:17; Kut 22:18; Isa 57:1, 2; Mdo 16:16, 19; Law 19:31; 20:27; Kum 18:10Wakati huo Samweli alikuwa amekufa, nao Israeli wote walikuwa wamemwombolezea na kumzika kwenye mji wake mwenyewe huko Rama. Sauli alikuwa amewafukuza waaguzi na wachawi.

428:4 Yos 19:18; 1Sam 31:1-3; 2Sam 1:6, 21; 21:12; Law 19:31; Kum 18:10-11; 2Fal 4:8Wafilisti wakakusanyika na kupiga kambi yao huko Shunemu, naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote na kupiga kambi yao huko Gilboa. 528:5 Kut 19:16; Ay 15:21; 18:11; Za 48:5, 6; 73:19; Isa 57:20; Dan 5:6Sauli alipoona jeshi la Wafilisti, akaogopa; moyo wake ukajawa na hofu kuu. 628:6 1Sam 8:18; 14:37; Kum 13:3; Kut 28:30; Law 8:8; Eze 20:3; Amo 8:11; Mik 3:7; Hes 12:6; Mit 1:28; 1Nya 10:13-14Ndipo Sauli akauliza ushauri kwa Bwana, lakini Bwana hakumjibu kwa ndoto, wala kwa Urimu,28:6 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha. wala kwa njia ya manabii. 728:7 1Nya 10:13; Mdo 16:16; Yos 17:11; Za 83:10Basi Sauli akawaambia watumishi wake, “Nitafutieni mwanamke mwaguzi ili nimwendee, nipate kuuliza kwake.”

Watumishi wake wakamwambia, “Yuko mwanamke mmoja huko Endori.”

828:8 1Fal 22:30; 2Nya 18:29; 35:22; 2Fal 1:3; Isa 8:19; 1Nya 10:13Hivyo Sauli akajigeuza kwa kuvaa mavazi mengine, naye usiku akiwa amefuatana na watu wawili wakaenda kwa huyo mwanamke. Akamwambia, “Nibashirie kwa uaguzi, unipandishie yule nitakayekutajia.”

928:9 Ay 18:10; Za 31:4; 69:22; Isa 8:14Huyo mwanamke akamwambia, “Wewe unajua lile alilofanya Mfalme Sauli. Amewakatilia mbali waaguzi, wapiga ramli wote na wachawi katika nchi. Mbona umenitegea maisha yangu ili wapate kuniua?”

10Sauli akamwapia huyo mwanamke kwa Jina la Bwana, akasema, “Kwa hakika kama Bwana aishivyo, hutaadhibiwa kwa ajili ya jambo hili.”

11Ndipo yule mwanamke akauliza, “Je unataka nikupandishie nani?”

Sauli akasema, “Nipandishie Samweli.”

1228:12 Mwa 27:36; 1Fal 14:6; Isa 57:2; Ufu 14:13Yule mwanamke alipomwona Samweli, alipiga yowe kwa sauti kuu, naye akamuuliza Sauli, “Mbona umenidanganya? Wewe ndiwe Sauli.”

1328:13 Law 19:31; 2Nya 33:6Mfalme akamwambia, “Usiogope. Unaona nini?”

Yule mwanamke akasema, “Naona mungu unapanda kutoka ardhini.”

1428:14 1Sam 15:27; 24:8; 2The 2:10, 11Sauli akamuuliza, “Ni mfano wa nini?”

Yule mwanamke akasema, “Ni mwanaume mzee amevaa joho anayepanda.”

Ndipo Sauli akatambua kwamba ni Samweli. Sauli akasujudu kifudifudi, uso wake hadi ardhini.

1528:15 Amu 16:20; Kum 13:3; 1Sam 18:12Samweli akamuuliza Sauli, “Kwa nini unanitaabisha kwa kunipandisha juu?”

Sauli akasema, “Mimi ninasumbuka sana, kwa maana Wafilisti wanapigana vita dhidi yangu, naye Mungu ameniacha. Hanijibu tena wala kwa njia ya manabii wala kwa ndoto. Kwa hiyo nimekuita wewe ili unijulishe la kufanya.”

16Samweli akamuuliza, “Kwa nini uniulize mimi, maadamu Bwana amekuacha na kuwa adui yako? 1728:17 1Sam 15:28Bwana ametenda lile alilotangulia kusema kupitia kwangu. Bwana ameurarua ufalme kutoka mikononi mwako, naye amempa mmoja wa jirani zako, yaani Daudi. 1828:18 1Sam 15:20; Kum 9:8; 1Sam 15:3; Mwa 14:7; 1Sam 14:48Kwa sababu wewe hukumtii Bwana, wala hukumtimizia ghadhabu yake kali juu ya Waamaleki, Bwana amekutendea mambo haya leo. 1928:19 1Sam 31:2; 1Nya 8:33Zaidi ya hayo, Bwana atawatia Israeli pamoja na wewe mikononi mwa Wafilisti, na kesho wewe na wanao mtakuwa pamoja nami. Bwana pia atalitia jeshi la Israeli mikononi mwa Wafilisti.”

2028:20 1Sam 25:37; Za 50:21Papo hapo Sauli akaanguka chini, akajinyoosha, akiwa amejawa na hofu kwa ajili ya maneno ya Samweli. Nguvu zake zikamwishia kwa maana alikuwa hajala chochote mchana ule wote na usiku.

2128:21 Amu 9:17; 12:3; Ay 13:14; 1Sam 19:5Yule mwanamke alipomwendea Sauli na kumwona amepatwa na hofu, akamwambia, “Tazama, mimi mtumishi wako mwanamke nimekutii. Nimeweka maisha yangu hatarini kwa kufanya kile ulichoniagiza nifanye. 22Sasa tafadhali isikilize sauti ya mtumishi wako, uniruhusu nikupatie chakula kidogo ule ili uwe na nguvu za kurejea ulikotoka.”

2328:23 1Fal 21:4; 2Fal 5:13; Mwa 4:6; Mit 25:20, 21Akakataa, akisema, “Mimi sitaki kula.”

Lakini watumishi wake wakaungana na yule mwanamke wakamsihi ale, naye akakubali. Basi akainuka hapo chini, akaketi juu ya kitanda.

2428:24 Mwa 18:7, 8; Lk 15:23-30Yule mwanamke alikuwa na ndama aliyenona hapo nyumbani, akamchinja mara moja. Akachukua unga, akaukanda, akatengeneza mkate usio chachu. 25Ndipo akamwandalia meza Sauli pamoja na watu wake, nao wakala. Usiku ule ule wakainuka na kwenda zao.