尼希米记 12 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

尼希米记 12:1-47

祭司和利未人的名单

1以下是与撒拉铁的儿子所罗巴伯耶书亚一起回来的祭司和利未人:

祭司有西莱雅耶利米以斯拉2亚玛利雅玛鹿哈突3示迦尼利宏米利末4易多近顿亚比雅5米雅民玛底雅璧迦6示玛雅约雅立耶大雅7撒路亚木希勒迦耶大雅。这些人在耶书亚的时代是祭司和他们弟兄的首领。

8利未人有耶书亚宾内甲篾示利比犹大玛他尼玛他尼及其弟兄负责感恩诗歌。 9他们的弟兄八布迦乌尼站在他们对面供职。

耶书亚大祭司的后代

10耶书亚约雅金约雅金以利亚实以利亚实耶何耶大11耶何耶大约拿单约拿单押杜亚

做族长的祭司

12约雅金时代,祭司家族的族长有西莱雅家族的米拉雅耶利米家族的哈拿尼雅13以斯拉家族的米书兰亚玛利雅家族的约哈难14米利古家族的约拿单示巴尼家族的约瑟15哈琳家族的押拿米拉约家族的希勒恺16易多家族的撒迦利亚近顿家族的米书兰17亚比雅家族的细基利米拿民家族的无名氏,摩亚底家族的毗勒太18璧迦家族的沙姆亚示玛雅家族的约拿单19约雅立家族的玛特乃耶大雅家族的乌西20撒来家族的加莱亚木家族的希伯21希勒迦家族的哈沙比雅耶大雅家族的拿坦业

祭司和利未家族的记录

22以利亚实耶何耶大约哈难押杜亚的时代,利未人的族长都列入名册;在波斯大流士执政期间,祭司的族长也都列入名册。 23做族长的利未子孙的名字都记录在历代志上,直到以利亚实的儿子约哈难的时代。

圣殿供职的班次

24哈沙比雅示利比甲篾的儿子耶书亚利未人的首领。他们的弟兄站在他们对面,照上帝仆人大卫的吩咐一班一班地赞美、称颂上帝。 25负责守卫库房的是玛他尼八布迦俄巴底亚米书兰达们亚谷26他们任职时正值约萨达的孙子、耶书亚的儿子约雅金尼希米省长和律法教师以斯拉祭司的时代。

尼希米奉献新城墙

27耶路撒冷的城墙典礼之际,民众把各处的利未人请到耶路撒冷,来称颂、歌唱、敲钹、鼓瑟、弹琴,欢庆典礼。 28歌乐手的子孙从耶路撒冷周围地区、尼陀法人的村庄、 29伯·吉甲,以及迦巴亚斯玛弗地区被招聚起来,因为歌乐手已在耶路撒冷周围为自己建立了村庄。 30祭司和利未人自洁,然后洁净民众、城门和城墙。

31我率犹大的首领上到城墙上,使称颂的歌乐手分成两大队,一队从城墙上向右前往粪厂门, 32跟在他们后面的有何沙雅和半数的犹大首领, 33还有亚撒利雅以斯拉米书兰34犹大便雅悯示玛雅耶利米35还有一些吹号的祭司,包括约拿单的儿子撒迦利亚约拿单示玛雅的儿子,示玛雅玛他尼的儿子,玛他尼米该亚的儿子,米该亚撒刻的儿子,撒刻亚萨的儿子; 36还有撒迦利亚的弟兄示玛雅亚撒利米拉莱基拉莱玛艾拿坦业犹大哈拿尼,他们都拿着上帝仆人大卫的乐器。队伍由律法教师以斯拉带领。 37他们经过泉门,沿大卫城的台阶,顺城墙的地势而上,经过大卫的宫殿,走到东面的水门。

38第二队称颂的歌乐手向左走,我和半数的民众在城墙上跟着他们,经过炉楼一直走到宽墙, 39然后又经过以法莲门、古门、鱼门、哈楠业楼、哈米亚楼,远至羊门,之后停在护卫门。 40这两队称颂的歌乐手站在上帝的殿里,我和半数的首领也站在那里, 41同时还有吹号的祭司以利亚金玛西雅米拿民米该亚以利约乃撒迦利亚哈楠尼亚42以及玛西雅示玛雅以利亚撒乌西约哈难玛基雅以拦以谢。歌乐手在伊斯拉希雅的领导下高声歌唱。 43那天,众人献上许多祭物,满心欢喜,因为上帝赐给他们极大的喜乐,连妇孺也都欢喜,耶路撒冷的欢声远处可闻。

预备圣殿的需要

44那天,有人被委派管理库房,把举祭、初熟之物和十一奉献收集在库房里。他们要照律法的规定从各城田地收集祭司和利未人当得的份,因为犹大人对祭司和利未人的供职很满意。 45祭司和利未人遵行上帝的吩咐,遵守洁净的礼。歌乐手和殿门守卫也遵照大卫和他儿子所罗门的命令行事。 46远在大卫亚萨的时代就有歌乐手,并有赞美、称颂上帝的诗歌。 47所罗巴伯尼希米的时代,全体以色列人供应歌乐手和殿门守卫的日常需用,并分出一份给利未人,利未人又分出一份给亚伦的子孙。

Kiswahili Contemporary Version

Nehemia 12:1-47

Makuhani Na Walawi Waliorudi Na Zerubabeli

112:1 Neh 10:2-8; Zek 4:6-10; Ezr 3:2Hawa wafuatao walikuwa makuhani na Walawi ambao walirudi na Zerubabeli mwana wa Shealtieli pamoja na Yeshua:

Seraya, Yeremia, Ezra,

2Amaria, Maluki, Hatushi,

3Shekania, Rehumu, Meremothi,

412:4 Lk 1:5; 1Nya 24:10Ido, Ginethoni, Abiya,

5Miyamini, Moadia, Bilga,

612:6 1Nya 24:7Shemaya, Yoyaribu, Yedaya,

712:7 Hag 1:1; Zek 5:1; Ezr 3:2Salu, Amoki, Hilkia na Yedaya.

Hawa walikuwa viongozi wa makuhani na wenzao wakati wa Yeshua.

812:8 Neh 11:17; 1Nya 16:8Walawi walikuwa Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na pia Matania, ambaye pamoja na wenzake, alikuwa kiongozi wa nyimbo za shukrani. 9Bakbukia na Uni, wenzao, walisimama mkabala nao wakati wa ibada.

1012:10 Ezr 10:24; Neh 3:20Yeshua alikuwa baba wa Yoyakimu, Yoyakimu alikuwa baba wa Eliashibu, Eliashibu alikuwa baba wa Yoyada, 11Yoyada alikuwa baba wa Yonathani, na Yonathani alikuwa baba wa Yadua.

12Katika siku za Yoyakimu, kulikuwa na wakuu wa jamaa za kikuhani:

wa jamaa ya Seraya, Meraya;

wa jamaa ya Yeremia, Hanania;

13wa jamaa ya Ezra, Meshulamu;

wa jamaa ya Amaria, Yehohanani;

14wa jamaa ya Maluki, Yonathani;

wa jamaa ya Shebania, Yosefu;

15wa jamaa ya Harimu, Adna;

wa jamaa ya Meremothi, Helkai;

1612:16 Neh 12:4wa jamaa ya Ido, Zekaria;

wa jamaa ya Ginethoni, Meshulamu;

1712:17 1Nya 24:10wa jamaa ya Abiya, Zikri;

wa jamaa ya Miniamini na ya Maazia, Piltai;

18wa jamaa ya Bilgai, Shamua;

wa jamaa ya Shemaya, Yehonathani;

19wa jamaa ya Yoyaribu, Matenai;

wa jamaa ya Yedaya, Uzi;

20wa jamaa ya Salu, Kalai;

wa jamaa ya Amoki, Eberi;

21wa jamaa ya Hilkia, Hashabia;

wa jamaa ya Yedaya, Nethaneli.

22Wakuu wa jamaa za Walawi katika siku za Eliashibu, Yoyada, Yohanani na Yadua, pia wale jamaa za makuhani, waliandikishwa wakati wa utawala wa Dario, Mwajemi. 2312:23 1Nya 9:14Wakuu wa jamaa miongoni mwa wazao wa Lawi hadi wakati wa Yohanani mwana wa Eliashibu waliandikishwa katika kitabu cha kumbukumbu. 2412:24 Ezr 2:40; 3:11; 1Nya 23:1Viongozi wa Walawi walikuwa: Hashabia, Sherebia, Yeshua mwana wa Kadmieli na wenzao, waliosimama mkabala nao kusifu na kushukuru, sehemu moja ikipokezana na nyingine kama ilivyoagizwa na Daudi mtu wa Mungu.

25Mabawabu waliokuwa wakilinda kwenye malango ya ghala ni: Matania, Bakbukia, Obadia, Meshulamu, Talmoni na Akubu. 2612:26 Neh 8:9; Ezr 7:6, 11Walihudumu siku za Yoyakimu mwana wa Yeshua, mwana wa Yosadaki, na katika siku za mtawala Nehemia, na za Ezra kuhani na mwandishi.

Kuwekwa Wakfu Ukuta Wa Yerusalemu

2712:27 Kum 20:5; 2Sam 6:5; 1Nya 25:6; Za 81:1-3; 92:3Wakati wa kuwekwa wakfu ukuta wa Yerusalemu, Walawi walitafutwa kule walikokuwa wakiishi, nao wakaletwa Yerusalemu kuadhimisha kwa shangwe huko kuweka wakfu kwa nyimbo za shukrani na kwa uimbaji wakitumia matoazi, vinubi na zeze. 2812:28 1Nya 2:54; 9:16Pia waimbaji walikusanywa pamoja kutoka maeneo yaliyozunguka Yerusalemu, kutoka vijiji vya Wanetofathi, 29kutoka Beth-Gilgali, na kutoka eneo la Geba na Azmawethi, kwa kuwa waimbaji walikuwa wamejijengea vijiji kuzunguka Yerusalemu. 3012:30 Kut 19:10; Ay 1:5Wakati makuhani na Walawi walipokuwa wamekwisha kujitakasa kwa kufuatana na desturi, waliwatakasa watu, malango na ukuta.

3112:31 Neh 2:13; Ezr 3:10; Hes 10:2; 2Nya 5:12Niliwaagiza viongozi wa Yuda wapande juu ya ukuta. Pia niliagiza makundi mawili makubwa ya waimbaji waimbe nyimbo za kumshukuru Mungu. Kundi moja lilipanda juu ya ukuta upande wa kuume, kuelekea Lango la Samadi. 32Hoshaya na nusu ya viongozi wa Yuda wakawafuata, 33pamoja na Azaria, Ezra, Meshulamu, 3412:34 Ezr 1:5Yuda, Benyamini, Shemaya, Yeremia, 3512:35 Ezr 3:10pamoja na baadhi ya makuhani wenye tarumbeta, na pia walikuwa na Zekaria mwana wa Yonathani, mwana wa Shemaya, mwana wa Matania, mwana wa Mikaya, mwana wa Zakuri, mwana wa Asafu, 3612:36 1Nya 23:5; 15:16; 2Nya 8:14pamoja na wenzake, Shemaya, Azareli, Milalai, Gilalai, Maai, Nethaneli, Yuda na Hanani, wakiwa na vyombo vya uimbaji, kama ilivyoagizwa na Daudi mtu wa Mungu. Mwandishi Ezra aliongoza maandamano. 3712:37 Neh 2:14; 3:3-15; 3:26; 2Sam 5:7-9Kwenye Lango la Chemchemi waliendelea moja kwa moja mpaka kwenye ngazi za Mji wa Daudi, kwenye mwinuko wa ukuta, na kupitia juu ya nyumba ya Daudi mpaka kwenye Lango la Maji upande wa mashariki.

3812:38 Neh 3:8-11Kundi la pili la waimbaji lilielekea upande wa kushoto. Niliwafuata juu ya ukuta, pamoja na nusu ya watu kupitia Mnara wa Tanuru mpaka kwenye Ukuta Mpana, 3912:39 2Fal 14:13; Neh 8:16; 2Nya 33:14; Neh 3:1-6juu ya Lango la Efraimu, Lango la Yeshana, Lango la Samaki, Mnara wa Hananeli, na Mnara wa Mia, mpaka kwenye Lango la Kondoo. Walipofika kwenye Lango la Ulinzi wakasimama.

4012:40 Za 42:4Kisha yale makundi mawili ya waimbaji yaliyoshukuru yakachukua nafasi zao katika nyumba ya Mungu. Nami pia nikafanya hivyo, pamoja na nusu ya maafisa, 41na makuhani wafuatao: Eliakimu, Maaseya, Miniamini, Mikaya, Elioenai, Zekaria na Hanania wakiwa na tarumbeta zao, 42na pia Maaseya, Shemaya, Eleazari, Uzi, Yehohanani, Malkiya, Elamu na Ezeri. Makundi haya yaliimba chini ya uongozi wa Yezrahia. 4312:43 Za 9:2; 92:4Siku hiyo watu walitoa dhabihu nyingi, wakishangilia kwa sababu Mungu aliwapa furaha kuu. Wanawake na watoto walishangilia pia. Sauti ya kushangilia huko Yerusalemu iliweza kusikika mbali sana.

4412:44 Neh 13:4, 13; Law 27:30; Kum 18:8Wakati huo watu walichaguliwa kuwa wasimamizi wa vyumba vya ghala kwa ajili ya matoleo, malimbuko na zaka. Kutoka kwenye yale mashamba yaliyozunguka miji walipaswa walete kwenye ghala mafungu kama sheria ilivyoamuru kwa ajili ya makuhani na Walawi, kwa kuwa Yuda alifurahishwa na huduma ya makuhani na Walawi. 4512:45 1Nya 25:1; 2Nya 8:14; 1Nya 6:31; 23:5Walifanya ibada ya Mungu wao na ibada ya utakaso, nao waimbaji na walinzi wa lango wakafanya hivyo pia, kufuatana na amri za Daudi na Solomoni mwanawe. 4612:46 2Nya 35:15; 29:27Muda mrefu uliopita, katika siku za Daudi na Asafu, walikuwepo viongozi wa waimbaji na wa nyimbo za sifa na za kumshukuru Mungu. 4712:47 Hes 18:21; Kum 18:8Kwa hiyo katika siku za Zerubabeli na za Nehemia, Israeli wote walitoa mafungu kila siku kwa ajili ya waimbaji na mabawabu. Pia walitenga fungu kwa ajili ya Walawi wengine, nao Walawi walitenga fungu kwa ajili ya wazao wa Aroni.