启示录 7 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

启示录 7:1-17

为上帝的仆人盖印

1这些事情之后,我看见四位天使分别站在地的四个角落控制着四面的风,使风不再吹向地面、海洋和树木。 2我又看见一位天使从东方日出之地上来,手里拿着永活上帝的印。他对那领受权柄能伤害地和海的四位天使大声说: 3“我们还没在上帝的奴仆额上盖印之前,你们不可伤害地、海和树木。” 4我听见以色列各支派中盖了印的共有十四万四千人: 5犹大支派有一万二千,吕便支派有一万二千,迦得支派有一万二千, 6亚设支派有一万二千,拿弗他利支派有一万二千,玛拿西支派有一万二千, 7西缅支派有一万二千,利未支派有一万二千,以萨迦支派有一万二千, 8西布伦支派有一万二千,约瑟支派有一万二千,便雅悯支派有一万二千。

劫后余生的上帝子民

9后来我又看见一大群人,多得不可胜数。他们来自各国家、各部落、各民族、各语言族群,身穿白袍,手拿棕树枝,站在宝座和羔羊面前, 10大声呼喊说:“救恩来自我们坐在宝座上的上帝,也来自羔羊!” 11众天使都站在宝座、众长老和四个活物的周围,在宝座前俯伏敬拜上帝,说: 12“阿们!愿颂赞、荣耀、智慧、感谢、尊贵、权柄、能力都归给我们的上帝,直到永永远远。阿们!”

13长老中有一位问我:“这些身穿白袍的人是谁?他们从哪里来?”

14我回答说:“先生,你知道答案。”

他便说:“这些都是经过大灾难的人,他们用羔羊的血将衣裳洗得纯净洁白。 15因此,他们在宝座前,在圣殿中不分昼夜地事奉上帝。坐在宝座上的那位要庇护他们。 16他们不会再受饥饿和干渴的折磨,也不会再受太阳和酷热的煎熬, 17因为在宝座中央的羔羊要做他们的牧人,引导他们到生命之泉那里,上帝要擦干他们所有的眼泪。”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ufunuo 7:1-17

Waisraeli 144,000 Watiwa Muhuri

17:1 Yer 49:36; Mt 24:31Baada ya hili nikaona malaika wanne wakiwa wamesimama katika pembe nne za dunia, wakizuia hizo pepo nne za dunia, ili kwamba pasiwe na upepo utakaovuma juu ya nchi au juu ya bahari au juu ya mti wowote. 27:2 Ufu 9:4; Mt 16:16Nikaona malaika mwingine akipanda kutoka mawio ya jua akiwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akawaita kwa sauti kubwa wale malaika wanne waliokuwa wamepewa mamlaka ya kuidhuru nchi na bahari, akisema, 37:3 Ufu 6:6; Eze 9:4; Ufu 22:4“Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, hadi tuwe tumetia muhuri kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu.” 47:4 Ufu 9:16; 14:1-3Ndipo nikasikia idadi ya wale waliotiwa muhuri: yaani 144,000 kutoka makabila yote ya Israeli.

5Kutoka kabila la Yuda 12,000 walitiwa muhuri,

kutoka kabila la Reubeni 12,000,

kutoka kabila la Gadi 12,000,

6kutoka kabila la Asheri 12,000,

kutoka kabila la Naftali 12,000,

kutoka kabila la Manase 12,000,

7kutoka kabila la Simeoni 12,000,

kutoka kabila la Lawi 12,000,

kutoka kabila la Isakari 12,000,

8kutoka kabila la Zabuloni 12,000,

kutoka kabila la Yosefu 12,000,

na kutoka kabila la Benyamini 12,000.

Umati Mkubwa Wa Watu Kutoka Mataifa Yote

97:9 Ufu 5:9; 13:7; 7:15; Rum 11:25; Ufu 3:5; 6:11; 7:4Baada ya hili nikatazama na hapo mbele yangu palikuwa na umati mkubwa wa watu ambao hakuna yeyote awezaye kuuhesabu, kutoka kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao. 107:10 Za 3:8; Ufu 19:1Nao walikuwa wakipiga kelele kwa sauti kubwa wakisema:

“Wokovu una Mungu wetu,

yeye aketiye kwenye kiti cha enzi,

na Mwana-Kondoo!”

117:11 Ufu 4:4-10Malaika wote walikuwa wamesimama kukizunguka kile kiti cha enzi na wale wazee ishirini na wanne na wale viumbe wanne wenye uhai. Wakaanguka kifudifudi mbele ya hicho kiti cha enzi na kumwabudu Mungu, 127:12 Rum 11:36; Ufu 5:12-14wakisema:

“Amen!

Sifa na utukufu

na hekima na shukrani na heshima

na uweza na nguvu

viwe kwa Mungu wetu milele na milele.

Amen!”

137:13 Ufu 3:4; 7:9Kisha mmoja wa wale wazee ishirini na wanne akaniuliza, “Ni nani hawa waliovaa mavazi meupe, nao wametoka wapi?”

147:14 Ufu 22:14; Ebr 9:14; 1Yn 1:7Nikamjibu, “Bwana, wewe wajua.”

Naye akasema, “Hawa ni wale waliotoka katika ile dhiki kuu, nao wamefua mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo na kuyafanya meupe kabisa. 157:15 Ufu 22:3; 11:19; Isa 4:5-6Kwa hiyo,

“Wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu

na kumtumikia usiku na mchana

katika hekalu lake;

naye aketiye katika kile kiti cha enzi

atatanda hema yake juu yao.

167:16 Isa 49:10Kamwe hawataona njaa

wala kiu tena.

Jua halitawapiga

wala joto lolote liunguzalo.

177:17 Za 23:1; Yn 10:11; Isa 51:11; Ufu 21:3Kwa maana Mwana-Kondoo

aliyeko katikati ya kile kiti cha enzi

atakuwa Mchungaji wao;

naye atawaongoza kwenda

kwenye chemchemi za maji yaliyo hai.

Naye Mungu atafuta kila chozi

kutoka macho yao.”