启示录 20 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

启示录 20:1-15

捆绑魔鬼一千年

1我又看见一位天使从天而降,手里拿着无底坑的钥匙和一条大锁链。 2他捉住巨龙,就是那古蛇——魔鬼,又名撒旦,将它捆绑一千年。 3他把它扔进无底坑里关起来,加上封印,使它不能再欺骗各国的人。一千年期满后,它会暂时被释放。

同掌王权一千年

4我看见许多宝座,上面坐着的人得到了审判的权柄。他们是为基督做见证、为了上帝的道而被斩首之人的灵魂。他们没有拜兽和兽像,额上或手上也没有盖兽印。他们都一同复活,与基督同掌王权一千年。 5这是第一次的复活。其余已死的人要等到那一千年过去后,才会复活。 6在第一次复活的时候复活的人是有福的,是圣洁的,他们不在第二次死亡的权势之下。他们必做上帝和基督的祭司,与祂共掌王权一千年。

魔鬼的最终下场

7那一千年过后,撒旦会从被监禁的地方得到释放。 8它会再度欺骗天下各国,就是歌革玛各,叫他们召集军队准备打仗,军队的数目多如海沙。 9他们倾巢而出,布满大地,将圣徒的阵营和上帝所爱的城团团围住。那时烈火从天而降,烧灭了他们。 10那欺骗他们的魔鬼被扔进了怪兽和假先知所待的硫磺火湖中,在那里昼夜受苦,直到永永远远!

最后的审判

11我又看见一个白色的大宝座和坐在上面的那位。在祂面前,天地都逃避了,消失得无影无踪。 12我又看见死去的人,不论尊卑老少,都站在宝座前面。案卷都展开了,另有一卷,就是生命册也打开了。死去的人都要凭案卷中有关他们行为的记录受审判。 13海洋、死亡和阴间都交出了它们里面的死人,使他们按着各人的行为受审判。 14之后,死亡和阴间也被扔进火湖里,这火湖就是第二次的死。 15名字没有记在生命册上的都要被扔进火湖里。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ufunuo 20:1-15

Utawala Wa Miaka Elfu Moja

120:1 Ufu 10:1; 1:18Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa ameshika ufunguo wa lile Shimo na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 220:2 Ufu 12:9; 2Pet 2:4Akalishika lile joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ndiye ibilisi au Shetani, naye akamfunga kwa muda wa miaka 1,000. 320:3 Dan 6:17; Ufu 12:9Akamtupa katika lile Shimo, akamfunga humo na kulitia lakiri, ili kumzuia asiendelee kudanganya mataifa mpaka hiyo miaka 1,000 itimie. Baada ya hayo lazima afunguliwe kwa muda mfupi.

420:4 Dan 7:9; Ufu 6:9; 13:12, 16Kisha nikaona viti vya enzi vilivyokuwa vimekaliwa na hao waliopewa mamlaka ya kuhukumu, na nikaona roho za wale waliokatwa vichwa kwa sababu ya ushuhuda wa Yesu na kwa sababu ya neno la Mungu. Hawakuwa wamemsujudu huyo mnyama wala sanamu yake wala hawakupokea ile chapa yake kwenye vipaji vya nyuso zao au kwenye mikono yao. Wakawa hai na kutawala pamoja na Kristo miaka 1,000. 520:5 Lk 14:14; 1The 4:16(Wafu waliosalia hawakufufuka mpaka ilipotimia hiyo miaka 1,000.) Huu ndio ufufuo wa kwanza. 620:6 Ufu 14:13; 2:11; 1:6Waliobarikiwa na walio watakatifu ni wale walio na sehemu katika ufufuo wa kwanza. Hao mauti ya pili haina nguvu juu yao, bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye kwa muda wa miaka 1,000.

Kuhukumiwa Kwa Shetani

720:7 Ufu 20:2Hiyo miaka 1,000 itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka kifungoni mwake, 820:8 Eze 38:2; 39:1; Ufu 1:6naye atatoka ili kuyadanganya mataifa yaliyopo katika pembe nne za dunia, yaani, Gogu na Magogu apate kuwakusanya tayari kwa vita. Idadi yao ni kama mchanga ulioko pwani. 920:9 Eze 38:9, 16; 39:6; Za 87:2; Ufu 13:13Nao walitembea katika eneo lote la dunia, wakaizunguka kambi ya watakatifu na ule mji unaopendwa. Lakini moto ukashuka kutoka mbinguni na kuwateketeza. 1020:10 Ufu 19:20; 14:10, 11; Za 2:9Naye ibilisi aliyewadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti walikokuwa wametupwa yule mnyama na yule nabii wa uongo. Watateswa humo usiku na mchana, milele na milele.

Wafu Wanahukumiwa

1120:11 Ufu 4:2; 6:14; Mt 25:31-46; Dan 2:35Kisha nikaona kiti kikubwa cheupe cha enzi pamoja na yeye aliyeketi juu yake. Dunia na mbingu zikaukimbia uso wake wala mahali pao hapakuonekana. 1220:12 Dan 7:10; Mal 3:16; Yer 17:10; Mt 16:27Nami nikawaona wafu wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa. Pia kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni kitabu cha uzima. Hao wafu wakahukumiwa sawasawa na matendo yao kama yalivyoandikwa ndani ya hivyo vitabu. 1320:13 Ufu 6:8; Isa 26:19Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, nayo mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Kila mtu akahukumiwa kulingana na yale aliyoyatenda. 1420:14 1Kor 15:26; Ufu 20:13; 19:20; 2:11Kisha mauti na Kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 1520:15 Dan 12:1; Mt 25:41Iwapo mtu jina lake halikuonekana katika kile kitabu cha uzima, alitupwa ndani ya lile ziwa la moto.