历代志上 29 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

历代志上 29:1-30

为建殿而献的礼物

1大卫王又对全体会众说:“我儿所罗门是上帝特别拣选的,但他还年轻,缺乏经验。建殿的工程浩大,因为这殿不是为人造的,而是为耶和华上帝造的。 2我已竭尽所能为我上帝的殿预备了制作金器、银器、铜器、铁器和木器所需的金银铜铁及木头,还有大量玛瑙、镶嵌用的宝石、彩石、大理石及其他贵重的石头。 3而且,我因为爱慕我上帝的殿,除了预备以上物品外,还把自己珍藏的金银献上,用来建造我上帝的殿。 4我献上两百万两俄斐金、四百八十万两纯银,用来贴殿墙, 5供匠人制作金器银器。今天,有谁乐意向耶和华奉献?”

6结果,各族长、以色列各支派的首领、千夫长、百夫长和负责王室事务的官员都乐意奉献, 7他们为上帝的殿奉献了三百四十万两金子,六百八十万两银子,六百二十吨铜,三千四百吨铁。 8有宝石的人都把宝石交到耶和华殿的库房,由革顺耶歇保管。 9因为他们诚心诚意地把东西献给耶和华,百姓欢喜不已,大卫王也非常欢喜。

大卫颂赞耶和华

10大卫在会众面前颂赞耶和华,说:“我们先祖以色列的上帝耶和华啊,你永永远远当受颂赞! 11耶和华啊,伟大、权能、荣耀、尊贵和威严都是你的,天上地下的一切都是你的。耶和华啊,国度是你的,你是万有的至高主宰。 12富贵和尊荣都从你而来,你掌管一切,你手中有权柄和能力,能使人尊大、强盛。 13我们的上帝啊,我们称颂你,赞美你荣耀的名。

14“我算什么,我的人民算什么,怎么能向你奉献?因为万物都从你而来,我们只是把从你那里得来的献给你。 15我们在你面前只是客旅,是寄居的,像我们祖先一样;我们在世的日子就像影子一样转瞬即逝。 16我们的上帝耶和华啊,我们为你的圣名建造殿宇所预备的这一切财物,都是从你那里来的,都属于你。 17我的上帝啊,我知道你洞察人心,喜爱正直的人。我怀着正直的心甘愿献上这一切,我也看见你这里的子民甘心乐意地将财物献给你。 18我们祖先亚伯拉罕以撒以色列的上帝耶和华啊!求你使你的子民常存这样的心志,使他们的心忠于你。 19求你赐给我儿所罗门忠诚的心,以遵行你的诫命、法度和律例,用我预备的材料建造殿宇。”

20大卫对全体会众说:“你们要颂赞你们的上帝耶和华。”于是,全体会众颂赞他们祖先的上帝耶和华,向耶和华和王俯伏下拜。

所罗门被立为王

21次日,他们向耶和华献平安祭和燔祭。他们代表全以色列献上一千头公牛、一千只公绵羊、一千只羊羔,同时还献上奠祭及许多其他祭。 22那一天,他们在耶和华面前欢欢喜喜地吃喝。

他们再次拥立大卫的儿子所罗门做王,在耶和华面前膏立他做首领,又膏立撒督做祭司。 23于是,所罗门登上了耶和华所赐的王位,接替他父亲大卫做王。他凡事亨通,以色列众人都服从他, 24众首领、勇士和大卫王的众子都效忠于他。 25耶和华使所罗门倍受以色列人尊崇,赐他君王的威严,超过在他之前的所有以色列王。

大卫去世

26耶西的儿子大卫是全以色列的王, 27他统治以色列四十年,他在希伯仑执政七年,在耶路撒冷执政三十三年。 28大卫年纪老迈,享尽富贵尊荣后,寿终正寝。他儿子所罗门继位。 29大卫王的事迹自始至终都记在撒母耳先见、拿单先知和迦得先见的史记上。 30书中记述了他的政绩和英勇事迹,还有他和以色列及列国所遭遇的事。

Kiswahili Contemporary Version

1 Nyakati 29:1-30

Matoleo Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Hekalu

129:1 1Fal 3:7; 2Nya 13:7; Mit 4:3; 1Nya 22:5Ndipo Mfalme Daudi akaliambia kusanyiko lote: “Mwanangu Solomoni, yeye ambaye Mungu amemchagua, ni kijana mdogo na asiye na uzoefu. Kazi hii ni kubwa, kwa sababu Hekalu hili la fahari si kwa ajili ya mwanadamu bali ni kwa ajili ya Bwana. 229:2 Ezr 6:5; Ufu 21:18; Hag 2:8; Isa 54:11; 1Nya 22:2-5; Kut 28:9Kwa uwezo wangu wote nimetenga mali kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu: dhahabu kwa kazi za dhahabu, fedha kwa ajili ya fedha, shaba kwa kazi za shaba, chuma kwa kazi za chuma na miti kwa kazi za miti, vivyo hivyo vito vya shohamu kwa ajili ya kutia kwenye vijalizo, almasi, mawe ya rangi mbalimbali, aina zote za vito vya thamani na marmar; yote haya kwa wingi mno. 329:3 2Nya 24:10; Za 28:9; 2Nya 35:8; Za 26:8; 27:4; Mit 3:9Zaidi ya hayo, kwa kujitolea kwangu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, sasa ninatoa hazina zangu mwenyewe za dhahabu na fedha kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, zaidi ya mali niliyotoa kwa ajili ya Hekalu hili takatifu: 429:4 Mwa 10:29; 1Nya 22:14; Ay 22:24; 1Fal 9:28; 2Nya 8:18talanta 3,00029:4 Talanta 3,000 za dhahabu sawa na tani 110. za dhahabu (dhahabu ya Ofiri) na talanta 7,00029:4 Talanta 7,000 za fedha ni sawa na tani 260. za fedha safi iliyosafishwa, kwa ajili ya kufunika kuta za Hekalu, 5kwa kazi ya dhahabu na kazi ya fedha na kwa kazi yote itakayofanywa na mafundi. Basi, ni nani anayependa kujitoa kwa Bwana leo?”

629:6 1Nya 28:1; Kut 36:2; Ezr 7:15Ndipo viongozi wa jamaa, maafisa wa kabila za Israeli, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, pamoja na maafisa waliokuwa wasimamizi wa kazi za mfalme wakatoa kwa hiari yao.

7Wakatoa kwa ajili ya kazi ya Hekalu la Mungu talanta 5,00029:7 Talanta 5,000 za dhahabu ni sawa na tani 190. na darkoni 10,00029:7 Darkoni 10,000 za dhahabu ni sawa na kilo 84. za dhahabu, talanta 10,00029:7 Talanta 10,000 za fedha ni sawa na tani 375. za fedha, talanta 18,00029:7 Talanta 18,000 za shaba ni sawa na tani 675. za shaba na talanta 100,00029:7 Talanta 100,000 za chuma ni sawa na tani 3,750. za chuma. 829:8 Kut 35:27; 1Nya 26:21Kila mmoja aliyekuwa na vito vya thamani akavitoa katika hazina ya Hekalu la Bwana chini ya uangalizi wa Yehieli Mgershoni. 929:9 1Fal 8:61; 2Kor 9:7Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwa Bwana. Mfalme Daudi pia akafurahi sana.

Maombi Ya Daudi

1029:10 1Fal 8:15-16; 2Nya 6:4; Za 72:18; Eze 3:12Daudi akamhimidi Bwana mbele ya kusanyiko lote, akisema:

“Uhimidiwe wewe, Ee Bwana,

Mungu wa Israeli baba yetu,

tangu milele hata milele.

1129:11 Za 24:8; 89:11; Mt 6:13; Ufu 5:12-13; Dan 4:34-35; 1Tim 1:17Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Bwana,

na utukufu na enzi na uzuri,

kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani

ni chako wewe.

Ee Bwana, ufalme ni wako;

umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.

1229:12 Ezr 7:27; Mhu 5:19; 2Nya 20:6; Rum 11:36; Kum 8:18; 1Sam 2:7-8; Za 75:6; Mit 10:22; Yak 1:17Utajiri na heshima vyatoka kwako;

wewe ndiwe utawalaye vitu vyote.

Mikononi mwako kuna nguvu na uweza

ili kuinua na kuwapa wote nguvu,

13Sasa, Mungu wetu, tunakushukuru

na kulisifu Jina lako tukufu.

14“Lakini mimi ni nani, nao watu wangu ni nani, hata tuweze kukutolea kwa ukarimu namna hii? Vitu vyote vyatoka kwako, nasi tumekutolea tu vile vitokavyo mkononi mwako. 1529:15 Mwa 47:9; 23:4; Ebr 11:13; Mhu 6:12; Za 102:11; Ay 14:2; Za 39:12; 1Pet 2:11; Za 90:9; 144:4Sisi ni wageni na wapitaji machoni pako, kama walivyokuwa baba zetu wote. Siku zetu duniani ni kama kivuli, bila tumaini. 16Ee Bwana Mungu wetu, kwa wingi wote huu ambao tumekutolea kwa kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina lako Takatifu, vimetoka mkononi mwako, navyo vyote ni mali yako. 1729:17 Mit 17:3; Yer 11:20; Za 15:1-5; Mit 11:20; Ebr 4:13; Kum 8:2; 1Sam 16:7; 1Nya 28:9; Za 7:9; Yer 17:10; Mit 16:2Ninajua, Mungu wangu, kwamba wewe huujaribu moyo na unapendezwa na unyofu. Vitu hivi vyote nimetoa kwa hiari na kwa moyo mnyofu. Nami sasa nimeona kwa furaha jinsi watu wako walioko hapa kwa hiari yao walivyokutolea wewe. 1829:18 Za 10:17; Yer 10:23Ee Bwana, Mungu wa baba zetu Abrahamu, Isaki na Israeli, weka shauku hii ndani ya mioyo ya watu wako daima na uifanye mioyo yao iwe na uaminifu kwako. 1929:19 1Fal 8:61; Isa 38:3; 1Nya 22:14; Za 72:1Nawe umpe mwanangu Solomoni kujitolea kwako kwa moyo wote ili kuzishika amri zako, masharti yako, maagizo yako na kufanya kila kitu ili kujenga Hekalu hili la fahari ambalo kwa ajili yake nimetoa.”

20Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote, “Mhimidini Bwana Mungu wenu.” Hivyo wote wakamhimidi Bwana, Mungu wa baba zao. Wakasujudu na kuanguka kifudifudi mbele za Bwana na mfalme.

Solomoni Akubalika Kuwa Mfalme

21Siku ya pili yake wakamtolea Bwana dhabihu na sadaka za kuteketezwa: mafahali 1,000, kondoo dume 1,000 na wana-kondoo dume 1,000, pamoja na sadaka za kinywaji na sadaka nyingine nyingi sana kwa ajili ya Israeli. 2229:22 1Nya 12:40; 1Sam 2:35; 1Fal 1:33-39Wakala na kunywa kwa furaha kubwa mbele za Bwana siku ile.

Wakamtawaza Solomoni mwana wa Daudi mara ya pili kuwa mfalme, wakamtia mafuta kwa ajili ya Bwana ili awe mfalme na Sadoki kuwa kuhani. 2329:23 1Fal 2:12; 1Nya 17:14Solomoni akaketi kwenye kiti cha enzi cha Bwana kuwa mfalme mahali pa Daudi baba yake. Akafanikiwa sana na Israeli wote wakamtii. 2429:24 Mwa 24:2; 47:29; Eze 17:18; 2Nya 30:8Maafisa wote na mashujaa, pamoja na wana wote wa Daudi, wakaahidi kumtii Mfalme Solomoni.

2529:25 1Fal 10:7; 3:13; Mhu 2:9; 2Nya 1:12; Dan 5:18-19; Ebr 2:9Bwana akamtukuza sana Solomoni mbele ya Israeli wote na kumvika fahari ya kifalme ambayo hakuna mfalme yeyote wa Israeli kabla yake aliwahi kuwa nayo.

Muhtasari Wa Utawala Wa Daudi

2629:26 1Nya 18:14Daudi mwana wa Yese alikuwa mfalme wa Israeli yote. 2729:27 2Sam 5:4-5; 1Fal 2:11Alitawala Israeli kwa miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.

2829:28 Mwa 15:15; Mdo 13:36; 1Nya 23:1; Mwa 25:8; Hes 23:10; Ay 5:26Daudi akafa akiwa mzee mwenye umri mwema, akiwa ameshiba siku, utajiri na heshima. Naye Solomoni mwanawe akawa mfalme baada yake.

2929:29 1Sam 9:9; 22:5; 2Sam 7:2; Ay 5:26Kuhusu matukio ya utawala wa Mfalme Daudi, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kumbukumbu za mwonaji Samweli, na kumbukumbu za nabii Nathani na kumbukumbu za mwonaji Gadi, 3029:30 Dan 2:21pamoja na habari zote za utawala wake, nguvu zake na matukio yaliyompata yeye, na Israeli, na falme za nchi nyingine zote.