历代志上 26 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

历代志上 26:1-32

圣殿的守卫

1以下是殿门守卫的班次:

可拉亚萨的后代有可利的儿子米施利米雅2米施利米雅的长子是撒迦利亚,次子是耶叠,三子是西巴第雅,四子是耶提聂3五子是以拦,六子是约哈难,七子是以利约乃4俄别·以东的长子是示玛雅,次子是约萨拔,三子是约亚,四子是沙甲,五子是拿坦业5六子是亚米利,七子是以萨迦,八子是毗乌利太,因为上帝赐福俄别·以东6他儿子示玛雅有几个儿子都很能干,在各自的家族中做首领。 7他们是俄得尼利法益俄备得以利萨巴。他们的亲族以利户西玛迦也很能干。 8这些都是俄别·以东的子孙,他们和他们的儿子及亲族共有六十二人,都是能干称职的人。 9米施利米雅的儿子及亲族共十八人,都很能干。 10米拉利的后代何萨的长子是申利,他本来不是长子,是被他父亲立为长子的。 11次子是希勒迦,三子是底巴利雅,四子是撒迦利亚何萨的儿子及亲族共十三人。

12这些按族长分成小组的殿门守卫在耶和华的殿里按班次供职,与他们的亲族一样。 13他们无论大小,都按照族系抽签,以决定看守哪个门。 14示利米雅抽中东门,他儿子撒迦利亚是个精明的谋士,抽中北门。 15俄别·以东抽中南门,他儿子抽中库房。 16书聘何萨抽中西门和上行之路的沙利基门,守卫与守卫相对而立。 17每天有六个利未人守东门,四人守北门,四人守南门,守库房的二人一组。 18至于西面的走廊,守卫街道的有四人,守卫走廊的有二人。 19以上是可拉的子孙和米拉利的子孙守门的班次。

圣殿里的其他职务

20利未亚希雅负责掌管上帝殿里的库房和放圣物的库房。 21革顺拉但的子孙中做族长的有耶希伊利22耶希伊利的两个儿子西坦约珥负责管理耶和华殿里的库房。 23暗兰族、以斯哈族、希伯伦族、乌薛族也各有其职。 24摩西的孙子、革舜的儿子细布业是库房的主管。 25细布业的亲族有以利以谢以利以谢的儿子是利哈比雅利哈比雅的儿子是耶筛亚耶筛亚的儿子是约兰约兰的儿子是细基利细基利的儿子是示罗密26示罗密及其亲族负责管理库房中的圣物,这些物品是大卫王、众族长、千夫长、百夫长和将领献给上帝的圣物。 27他们把战争中掳掠的财物献出来,以备修缮耶和华的殿。 28撒母耳先见、基士的儿子扫罗尼珥的儿子押尼珥洗鲁雅的儿子约押及其他人奉献的圣物都由示罗密及其亲族管理。

29以斯哈族的基拿尼雅及其众子做官长和审判官,为以色列管理圣殿以外的事务。 30希伯伦族的哈沙比雅及其亲族一千七百人都很能干,他们在以色列约旦河以西办理耶和华和王的事务。 31按家谱记载,希伯伦宗族的族长是耶利雅大卫执政第四十年,经过调查,在基列雅谢希伯伦族中找到一些能干的人。 32耶利雅的亲族有两千七百人,都是能干的族长。大卫王派他们在吕便支派、迦得支派和玛拿西半个支派中办理一切有关上帝和王的事务。

Kiswahili Contemporary Version

1 Nyakati 26:1-32

Mabawabu

126:1 1Nya 9:17; Hes 26:9-11; 2Nya 23:19; Hes 16:1-2; 1Nya 15:18; Yud 11; 1Nya 6:39Hii ndiyo migawanyo ya mabawabu:

Kutoka kwa wana wa Kora alikuwa: Meshelemia mwana wa Kore, mmoja wa wana wa Asafu.

226:2 1Nya 9:21Meshelemia alikuwa na wana wafuatao:

Zekaria mzaliwa wa kwanza,

Yediaeli wa pili,

Zebadia wa tatu,

Yathnieli wa nne,

3Elamu wa tano

Yehohanani wa sita

na Eliehoenai wa saba.

4Obed-Edomu naye alikuwa na wana wafuatao:

Shemaya mzaliwa wa kwanza,

Yehozabadi wa pili,

Yoa wa tatu,

Sakari wa nne,

Nethaneli wa tano,

526:5 Mwa 33; 5; 2Sam 5:10; 1Nya 13:13-14; Za 127:3Amieli wa sita,

Isakari wa saba,

na Peulethai wa nane.

(Kwa kuwa Mungu alikuwa amembariki Obed-Edomu.)

6Shemaya mwanawe pia alikuwa na wana, waliokuwa viongozi katika jamaa ya baba yao kwa sababu walikuwa watu wenye uwezo mkubwa. 7Wana wa Shemaya ni: Othni, Refaeli, Obedi na Elizabadi; jamaa zake Elihu na Semakia walikuwa pia watu wenye uwezo. 8Hawa wote walikuwa wazao wa Obed-Edomu; wao na wana wao na jamaa zao walikuwa watu wenye uwezo pamoja na nguvu za kufanya kazi. Wazao wa Obed-Edomu jumla yao walikuwa sitini na wawili.

9Meshelemia alikuwa na wana na jamaa zake, waliokuwa watu wenye uwezo: jumla yao watu kumi na wanane.

1026:10 Kum 21:16-17; 1Nya 16:38; 5:1; Mwa 4:7; 49:3Hosa, Mmerari, alikuwa na wana wafuatao: Shimri alikuwa mkuu wao (baba yake alikuwa amemweka yeye kuwa mkuu ijapokuwa hakuwa mzaliwa wa kwanza), 11Hilkia wa pili, Tabalia wa tatu na Zekaria wa nne. Wana na jamaa za Hosa jumla yao walikuwa watu kumi na watatu.

12Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwa Bwana kama jamaa zao walivyokuwa nazo. 1326:13 1Nya 24:5; 25:8; Mit 18:18; Yos 18:10; Yn 1:7; Mdo 1:26; 10:34; Gal 3:28; Kol 3:11Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo.

1426:14 1Nya 9:18-21Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia.26:14 Shelemia jina lingine ni Meshelemia. Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia. 1526:15 1Nya 13:13; 2Nya 25:24Kura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe. 1626:16 1Fal 10:5; 1Nya 24:31; Neh 12:24; 2Nya 9:4; 1Nya 25:8Kura za Lango la Magharibi na Lango la Shalekethi kwenye barabara ya juu zikawaangukia Shupimu na Hosa.

Zamu za walinzi ziligawanywa kwa usawa: 17Kulikuwa na Walawi sita kila siku upande wa mashariki, wanne upande wa kaskazini, wanne upande wa kusini, na wawili wawili kwa mara moja kwenye ghala. 18Kuhusu ukumbi kuelekea magharibi, kulikuwa na wanne barabarani na wawili kwenye ukumbi wenyewe.

1926:19 Neh 7:1; Eze 44:11Hii ndiyo iliyokuwa migawanyo ya mabawabu waliokuwa wazao wa Kora na wa Merari.

Watunza Hazina Na Maafisa Wengine

2026:20 2Nya 24:5; 1Nya 28:12; 22:14-16; Kum 12:6; 1Fal 7:51; 14:26; 1Nya 9:26-29; Mal 3:10; 2Nya 31:11-12Katika Walawi, Ahiya alikuwa mwangalizi wa hazina za nyumba ya Mungu na mwangalizi wa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.

2126:21 1Nya 6:17; 23:8; 29:8Wazao wa Ladani, waliokuwa Wagershoni kupitia Ladani na waliokuwa viongozi wa jamaa za Ladani Mgershoni, walikuwa Yehieli, 22wana wa Yehieli, wana wa Zethamu na wa nduguye Yoeli. Wao walikuwa waangalizi wa hazina za Hekalu la Bwana.

2326:23 Hes 3:27; Kut 6:18; 1Nya 23:12Kutoka kwa wana wa Amramu, wana wa Ishari, wana wa Hebroni na wana wa Uzieli:

2426:24 1Nya 23:16-18; 24:20Shebueli, mzao wa Gershomu mwana wa Mose, alikuwa afisa mwangalizi wa hazina. 2526:25 1Nya 23:18; 24:22Jamaa zake kutoka kwa Eliezeri, wanawe walikuwa: Rehabia, Yeshaya, Yoramu, Zikri na Shelomithi. 2626:26 2Sam 8:11Shelomithi na jamaa zake walikuwa waangalizi wa hazina zote za vitu vile vilivyowekwa wakfu na Mfalme Daudi, kwa viongozi wa jamaa waliokuwa majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, na kwa maafisa wengine wa jeshi. 2726:27 Hes 31:50; Yos 6:19, 24; 1Nya 22:14-16; 2Nya 15:11, 18; 2Fal 12:14; 22:4-5; Neh 10:32Baadhi ya nyara zilizotekwa vitani waliziweka wakfu kwa ajili ya ukarabati wa Hekalu la Bwana. 2826:28 1Sam 9:9Kila kitu kilichokuwa kimewekwa wakfu na Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya, pamoja na vitu vingine vyote vilivyokuwa vimewekwa wakfu, vyote vilikuwa chini ya uangalizi wa Shelomithi na jamaa zake.

2926:29 Kum 17:8-13; Neh 11:16; 2Nya 19:8-11; 1Nya 23:4Kutoka kwa wana wa Ishari: Kenania na wanawe walipewa kazi nje ya Hekalu kama maafisa na waamuzi juu ya Israeli.

3026:30 1Nya 27:17Kutoka kwa wana wa Hebroni: Hashabia na jamaa zake, watu 1,700 wenye uwezo, waliwajibika katika Israeli magharibi ya Yordani kwa ajili ya kazi zote za Bwana na utumishi wa mfalme. 3126:31 1Nya 23:19; 2Sam 5:4; Isa 16:9; Yer 48:32; 1Fal 2:11; 1Nya 29:27; Yos 21:39Kuhusu wana wa Hebroni, Yeria alikuwa mkuu wao kufuatana na orodha ya jamaa yao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi uchunguzi ulifanyika katika kumbukumbu, nao watu wenye uwezo miongoni mwa wana wa Hebroni wakapatikana huko Yazeri katika Gileadi. 3226:32 2Nya 19:11Yeria alikuwa na jamaa ya watu 2,700 waliokuwa watu wenye uwezo na viongozi wa jamaa, naye Mfalme Daudi akawaweka kuangalia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila Manase kuhusu kila jambo lililomhusu Mungu na shughuli za mfalme.