利未记 9 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

利未记 9:1-24

亚伦献祭

1第八天,摩西召来亚伦父子们和以色列的众长老。 2他对亚伦说:“你要在耶和华面前献上一头公牛犊作赎罪祭、一只公绵羊作燔祭,这些祭牲都要毫无残疾。 3然后,你要告诉以色列人,‘你们要取一只公山羊作赎罪祭、毫无残疾的一岁牛犊和羊羔各一只作燔祭、 4公牛和公绵羊各一只作平安祭,连同调油的素祭一起献给耶和华,因为今天耶和华要向你们显现。’” 5于是,以色列人遵照摩西的吩咐,把祭物带到会幕前。全体会众都聚集到那里,站在耶和华面前。 6摩西对他们说:“耶和华吩咐你们这样做,是为了向你们显出祂的荣耀。” 7随后,摩西亚伦说:“你要到坛前来,献上你的赎罪祭和燔祭,为自己和民众赎罪。也要按照耶和华的吩咐,为百姓献上他们的祭物,为他们赎罪。”

8于是,亚伦走到坛前,宰杀为他作赎罪祭的牛犊。 9他儿子们把牛犊的血递给他,他用手指蘸血抹在坛角上,将剩下的血倒在坛脚旁。 10他照耶和华对摩西的吩咐,在坛上焚烧牛犊的脂肪、肾脏和肝叶, 11把皮和肉带到营外焚烧。

12亚伦宰了燔祭祭牲,他儿子们把祭牲的血递给他洒在祭坛四周。 13他们将祭牲切成块,连头颅一起交给亚伦献在坛上焚烧。 14亚伦洗净祭牲的内脏和腿,放在祭坛的燔祭上焚烧。

15随后,亚伦为民众献祭。他牵来那只为民众作赎罪祭的公山羊,宰杀后,像刚才为自己献赎罪祭一样为他们献上赎罪祭。 16他又牵来燔祭祭牲,依照条例献上燔祭。 17除了早晨的燔祭,亚伦又取来素祭,从中拿了一把献在坛上焚烧。 18然后,他宰了公牛和公绵羊,为民众献平安祭。他儿子们把祭牲的血递给他,他把血洒在祭坛四周。 19他们把公牛和公绵羊的脂肪,即肥尾巴、遮盖内脏的脂肪、肾脏和肝叶, 20放在祭牲的胸上,然后亚伦把那些脂肪放在坛上焚烧, 21将胸肉和右腿肉作为摇祭在耶和华面前摇一摇,都遵照摩西的吩咐。

22亚伦献完赎罪祭、燔祭和平安祭,举手为民众祝福后,走下祭坛。 23之后,摩西亚伦走进会幕,又出来为民众祝福。这时,耶和华的荣耀向所有民众显现。 24有火从耶和华那里降下来,烧尽祭坛上的燔祭和脂肪。民众看见这景象,都欢呼起来,俯伏在地。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Walawi 9:1-24

Makuhani Waanza Huduma Yao

19:1 Eze 43:27; Law 4:15Katika siku ya nane, Mose akawaita Aroni na wanawe, na wazee wa Israeli. 29:2 Law 4:3; 8:14-18Akamwambia Aroni, “Chukua ndama dume kwa ajili ya sadaka yako ya dhambi, na kondoo dume kwa sadaka yako ya kuteketezwa, wote wawili wasiwe na dosari, nao uwalete mbele za Bwana. 39:3 Law 4:3, 32; 10:16; Ezr 6:17; Isa 53:10; Rum 8:3; 1Pet 2:24Kisha waambie Waisraeli: ‘Chukueni mbuzi dume kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na ndama na mwana-kondoo, wote wawili wawe wa umri wa mwaka mmoja, na wasio na dosari, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, 49:4 Law 4:10; Kut 32:6; 29:43; 9:6; 16:7; 24:16; 40:34-35; 1Fal 8:10-12na pia maksai na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya amani, ili kutoa dhabihu mbele za Bwana, pamoja na sadaka ya nafaka iliyochanganywa na mafuta. Kwa kuwa leo Bwana atawatokea.’ ”

5Wakavileta vile vitu Mose alivyowaagiza mbele ya Hema la Kukutania, nalo kusanyiko lote likakaribia na kusimama mbele za Bwana. 6Ndipo Mose akasema, “Hili ndilo Bwana alilowaagiza mlifanye, ili utukufu wa Bwana upate kuonekana kwenu.”

79:7 Law 16:6; Kut 30:10; Ebr 4:1-4; 7:27; 1Sam 3:14Mose akamwambia Aroni, “Njoo madhabahuni ili utoe dhabihu yako ya sadaka ya dhambi na sadaka yako ya kuteketezwa, ufanye upatanisho kwa ajili yako mwenyewe na kwa ajili ya watu. Kisha utoe sadaka ya upatanisho kwa ajili ya watu, kama vile Bwana alivyoagiza.”

89:8 Law 4:1-12; 10:19; 9:9; Kut 29:12; Eze 43:20; Law 4:7; 8:15Hivyo Aroni akaja madhabahuni na kumchinja yule ndama kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe. 9Wanawe wakamletea damu, naye akachovya kidole chake katika hiyo damu, akaitia kwenye pembe za madhabahu, nayo damu iliyobaki akaimwaga chini ya madhabahu. 10Juu ya madhabahu akateketeza mafuta, figo na mafuta yanayofunika ini kutoka kwenye hiyo sadaka ya dhambi, kama Bwana alivyomwagiza Mose. 119:11 Law 4:11-12Akateketeza nyama na ngozi nje ya kambi.

129:12 Law 10:19Kisha Aroni akachinja sadaka ya kuteketezwa. Wanawe wakamletea damu, naye akainyunyiza pande zote za madhabahu. 139:13 Law 1:8-9Wakamletea sadaka ya kuteketezwa kipande kwa kipande, pamoja na kichwa, naye akaviteketeza juu ya madhabahu. 149:14 Isa 53:10; 1Kor 15:3; 2Kor 5:21; Gal 1:4; Ebr 2:17; 1Pet 2:24; 3:18Akasafisha sehemu za ndani na miguu, akaviteketeza juu ya sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu.

159:15 Law 4:27-31Kisha Aroni akaleta sadaka ile iliyokuwa kwa ajili ya watu. Akachukua yule mbuzi wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya watu, akamchinja na kumtoa kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kama alivyofanya kwa ile ya kwanza.

169:16 Law 1:1-13Aroni akaleta sadaka ya kuteketezwa na kuitoa kama ilivyoelekezwa. 179:17 Law 2:1-2; 3:5; Kut 29:38; 9:18; Law 3:1-11Pia akaleta sadaka ya nafaka, akachukua konzi moja na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi.

18Akachinja maksai na kondoo dume kama sadaka ya amani kwa ajili ya watu. Wanawe Aroni wakampa ile damu, naye akainyunyiza kwenye madhabahu pande zote. 19Lakini sehemu zile za mafuta ya yule maksai na kondoo dume, yaani mafuta ya mkia, mafuta yaliyofunika tumbo, ya figo na yaliyofunika ini, 20hivi vyote wakaviweka juu ya vidari, kisha Aroni akayateketeza hayo mafuta ya wanyama juu ya madhabahu. 219:21 Kut 29:24-26; Law 7:30-34Aroni akaviinua vile vidari na paja la kulia mbele za Bwana ili viwe sadaka ya kuinuliwa, kama Mose alivyoagiza.

229:22 Mwa 48:20; Kut 39:43; Lk 24:50Kisha Aroni akainua mikono yake kuwaelekea watu na kuwabariki. Naye baada ya kutoa dhabihu ya sadaka ya dhambi, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya amani, akashuka chini.

239:23 Kut 40:2; 24:16; 2Sam 6:18; 2Nya 16:2; Hes 16:19Kisha Mose na Aroni wakaingia kwenye Hema la Kukutania. Walipotoka nje, wakawabariki watu. Nao utukufu wa Bwana ukawatokea watu wote. 249:24 Kut 19:18; Amu 6:21; 13:20; 1Fal 18:39; Mwa 15:17; 2Nya 7:1; Ezr 3:1Moto ukaja kutoka uwepo wa Bwana, ukairamba ile sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sehemu ya mafuta yaliyokuwa juu ya madhabahu. Watu wote walipoona jambo hili, wakapiga kelele kwa furaha na kusujudu.