利未记 5 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

利未记 5:1-19

1“如果有人当庭作证,却不肯把自己所知所见的说出来,就是犯罪,要担负罪责。 2如果有人接触了不洁净之物,如野兽的尸体、家畜的尸体或爬虫的尸体,即使无意也已不洁净,是有罪的。 3如果有人无意中接触了别人的不洁之物,当他意识到后,就有罪了。 4如果有人草率起誓,不论出于善意还是恶意,即使当初没有察觉,后来才意识到,也是有罪的。 5如果有人犯了以上任何一种罪,就必须认罪。 6为了赎过,他必须献给耶和华一只母绵羊或母山羊作赎罪祭。祭司要为他赎罪。

7“他若献不起羊,就要献给耶和华两只斑鸠或两只雏鸽,一只作赎罪祭,一只作燔祭。 8他要把它们带到祭司那里,祭司要先用一只鸟献赎罪祭,要扭断鸟脖子,但不可扯掉头。 9要把一些鸟血洒在祭坛边,剩下的血要倒在坛脚旁。这是赎罪祭。 10祭司要依照献燔祭的条例献上另一只鸟。这样,祭司为他赎了罪,他就会得到赦免。

11“他若献不起两只斑鸠或雏鸽,就要献一公斤细面粉作赎罪祭。细面粉中不可浇油或加乳香,因为这是赎罪祭。 12他要把细面粉带到祭司那里,祭司要从中取出一把作为象征放在坛上,与献给耶和华的火祭一起焚烧。这是赎罪祭。 13这样,祭司为他赎了罪,他就会得到赦免。剩下的细面粉要归祭司,像献素祭一样。”

献赎过祭的条例

14耶和华对摩西说: 15“如果有人无意中违犯了耶和华圣物的条例,为了赎过,他要从羊群中选一只毫无残疾的公绵羊献给耶和华,或按圣所的秤献上同等价值的银子。这是赎过祭。 16他要赔偿所造成的损失,并加赔五分之一,要把这些都交给祭司。祭司要为他献上公绵羊作赎过祭,为他赎罪,他就会得到赦免。

17“如果有人触犯耶和华的诫命,即使他不知道,也是有罪的,必须担当罪责。 18他要从羊群中选一只毫无残疾的公绵羊,或把同等价值的银子带到祭司那里作赎过祭。祭司要为他的无心之过赎罪,他就会得到赦免。 19这是赎过祭,因为他在耶和华面前确实有罪。”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Walawi 5:1-19

Sadaka Zingine Za Kuondoa Dhambi

15:1 Mit 29:24; Mt 26:63; Kut 28:38; Law 7:18; 17:16; 19:8; 20:17; 24:15; Hes 5:31; 9:15; 15:31; 19:20; 30:15“ ‘Ikiwa mtu atakuwa ametenda dhambi kwa sababu hakusema alipotakiwa kutoa ushahidi hadharani kuhusu jambo aliloona au kujua habari zake, yeye anastahili adhabu.

25:2 Law 7:21; 11:8, 11, 24-40; 13:45; Kum 14:8; Isa 6:5; 52:11; 64:5; Hes 19:22; Ay 15:16; Za 51:5; Eze 36:17; Hag 2:13“ ‘Au kama mtu akigusa kitu chochote ambacho ni najisi, iwe ni mizoga ya wanyama pori walio najisi, au ya wanyama wafugwao walio najisi, au ya viumbe vitambaavyo ardhini, hata akiwa hana habari, amekuwa najisi na mwenye hatia.

35:3 Hes 5:2; 9:6; 19:7, 11-16; Law 7:20; 11:25; 14:19; 21:1; Eze 44:25“ ‘Au kama akigusa kitu kilicho kichafu kinachotokana na binadamu, kitu chochote kile kinachoweza kumfanya awe najisi, hata akiwa hana habari, atakapofahamu atakuwa na hatia.

45:4 Isa 41:23; 1Sam 14:24; 25:22; Mdo 23:12; Mk 6:23“ ‘Au kama mtu ameapa kufanya kitu chochote bila kufikiri, kiwe chema au kibaya, kwa vyovyote mtu aweza kuapa bila kujali, hata akiwa hana habari, atakapofahamu atakuwa na hatia.

55:5 Law 16:21; 26:40; Hes 5:7; Yos 7:19; 1Fal 8:47; Mit 28:13“ ‘Wakati mtu yeyote atakapokuwa na hatia katika mojawapo ya haya, lazima akiri ni kwa njia gani ametenda dhambi, 65:6 Law 1:10; 4:3, 28; Kum 32:30na kama adhabu ya dhambi aliyoitenda, lazima alete kwa Bwana kondoo jike au mbuzi jike kutoka kwenye kundi lake kama sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yake.

75:7 Law 12:8; 14:21-40; 27:8; Mwa 15:9; Hes 6:10“ ‘Lakini huyo mtu kama hataweza kumtoa mwana-kondoo, ataleta hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa Bwana kuwa adhabu kwa ajili ya dhambi yake, mmoja wa hao ndege kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na wa pili kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. 85:8 Law 1:15-17Atawaleta kwa kuhani, ambaye atamtoa kwanza ndege mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo na kuacha kichwa chake kikiningʼinia, 95:9 Kut 24:6; Law 1:15; 4:17naye atanyunyiza sehemu ya hiyo damu ya sadaka ya dhambi kwenye pembe za madhabahu. Damu iliyobaki lazima ichuruzwe chini ya madhabahu. Hii ni sadaka ya dhambi. 105:10 Law 1:14-17; 4:26; 1Nya 15:13; Kut 32:30Kisha kuhani atamtoa yule ndege wa pili kama sadaka ya kuteketezwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa, na hivyo kufanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi aliyoitenda, naye atasamehewa.

115:11 Mwa 15:9; Law 2:1; Kut 16:36; Hes 5:15“ ‘Ikiwa basi, hawezi kupata hua wawili au makinda mawili ya njiwa, ataleta sehemu ya kumi ya efa5:11 Sehemu ya kumi ya efa ni sawa na kilo moja. ya unga laini kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Kamwe asiweke mafuta wala uvumba juu yake, kwa sababu ni sadaka ya dhambi. 125:12 Law 2:2, 9; 4:35Atauleta unga kwa kuhani, ambaye atachukua konzi moja kama sehemu ya kumbukumbu na atauteketeza kwenye madhabahu juu ya sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto. Hii ni sadaka ya dhambi. 135:13 Kut 32:30; 29:41; Law 2:3Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yoyote ya hizo alizotenda, naye atasamehewa. Sadaka iliyobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyokuwa ile sadaka ya nafaka.’ ”

Sadaka Ya Hatia

14Bwana akamwambia Mose: 155:15 Law 4:2; 6:6; 14:12-17; 19:21-22; 22:14; Kut 29:3; 30:13; Hes 5:8; 6:12, 18; 15:6; 18:9; 28:11; 1Sam 9:3; Eze 10:19; Isa 53:10“Mtu anapokiuka na kutenda dhambi pasipo kukusudia kuhusu mojawapo ya mambo matakatifu ya Bwana, huyo mtu ataleta kwa Bwana kama adhabu kondoo dume mmoja kutoka kundi lake, asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Hii ni sadaka ya hatia. 165:16 Law 6:4; 27:13; Hes 5:7; Law 22:14; Ebr 9:13-14Ni lazima alipe kwa yale aliyoshindwa kufanya kuhusu vitu vitakatifu, kwa kuongeza sehemu ya tano ya thamani ile na kuitoa yote kwa kuhani, ambaye atamfanyia upatanisho kwa huyo kondoo dume kama sadaka ya dhambi, naye atasamehewa.

175:17 Law 4:2; Za 19:12; Lk 12:48“Kama mtu akifanya dhambi na kufanya yale yaliyokatazwa katika mojawapo ya amri za Bwana, hata ikiwa hajui, yeye ana hatia na anastahili adhabu. 185:18 Law 6:6; 14:12Atamletea kuhani kama sadaka ya hatia kondoo dume kutoka kundi lake, kondoo asiye na dosari na mwenye thamani halisi kifedha. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa kosa alilotenda bila kukusudia, naye atasamehewa. 195:19 2Fal 12:16; Isa 53:10; Ezr 10:2Hii ni sadaka ya hatia; amekuwa na hatia kwa kufanya kosa dhidi ya Bwana.”