利未记 4 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

利未记 4:1-35

献赎罪祭的条例

1耶和华对摩西说: 2“你把以下条例告诉以色列人。

“如果有人无意中犯罪,触犯耶和华的任何诫命,要按以下方式献赎罪祭。

3“若大祭司犯罪,祸及众民,他必须献给耶和华一头毫无残疾的公牛犊作赎罪祭。 4他要把公牛犊牵到会幕门口,将手放在牛头上,在耶和华面前宰牛。 5他要取一些公牛的血带进会幕里, 6在耶和华面前用手指蘸血向圣所的幔子弹洒七次, 7也要把一些公牛的血抹在耶和华面前的香坛凸起的四角上,再把剩下的血倒在会幕门口的燔祭坛脚。 8他要取出作赎罪祭的公牛犊的所有脂肪,即包裹内脏的脂肪和内脏上的脂肪、 9两个肾脏和肾脏上靠近腰部的脂肪以及肝叶, 10正如取出平安祭牲的脂肪一样。他要将这一切放在燔祭坛上焚烧。 11-12至于公牛剩下的部分,即皮、所有的肉、头、腿、内脏和粪便,他要带到营外洁净之处,就是倒坛灰的地方,放在柴上焚烧。

13以色列全体会众若无意中触犯耶和华的任何诫命,即使没有意识到,也是犯罪。 14他们察觉自己犯罪后,必须献上一头公牛犊作赎罪祭。要将公牛犊带到会幕前, 15会众的长老要把手放在公牛的头上,在耶和华面前宰牛。 16大祭司要带一些牛血进入会幕, 17在耶和华面前用手指蘸血向幔子弹洒七次, 18也要把一些血抹在耶和华面前的香坛凸起的四角上,再把剩下的血倒在会幕门前的燔祭坛脚。 19他要取出公牛犊的所有脂肪,放在祭坛上焚烧, 20正如取出赎罪祭牲的脂肪一样。这样,祭司为全体会众赎了罪,他们就会得到赦免。 21他要把这公牛犊剩下的部分拿到营外焚烧,像焚烧前一头公牛犊一样。这是为全体会众所献的赎罪祭。

22“首领若无意中触犯他上帝耶和华的任何诫命,也是犯罪。 23他察觉自己犯罪后,必须献上一只毫无残疾的公山羊作祭物。 24他要把手放在羊头上,在杀燔祭牲的地方,在耶和华面前宰羊。这是他的赎罪祭。 25祭司要用手指蘸一些赎罪祭牲的血抹在燔祭坛凸起的四角上,再把剩下的血倒在燔祭坛脚。 26要像焚烧平安祭牲的脂肪一样,把羊的所有脂肪都放在坛上焚烧。这样,祭司为他赎了罪,他就会得到赦免。

27“平民若无意中触犯耶和华的任何诫命,也是犯罪。 28他察觉自己犯罪后,必须献上一只毫无残疾的母山羊作赎罪祭。 29他要把手放在赎罪祭牲的头上,在杀燔祭牲的地方宰羊。 30祭司要用手指蘸一些羊血抹在燔祭坛凸起的四角上,再把剩下的血倒在燔祭坛脚。 31献祭者要像取出平安祭牲的脂肪一样,取出母山羊的所有脂肪。祭司要把这一切放在坛上焚烧,作为蒙耶和华悦纳的馨香之祭。这样,祭司为他赎了罪,他就会得到赦免。

32“他若献绵羊作赎罪祭,必须献一只毫无残疾的母绵羊。 33他要把手放在羊头上,在杀燔祭牲的地方宰羊。 34祭司要用手指蘸一些羊血抹在燔祭坛凸起的四角上,再把剩下的血倒在燔祭坛脚。 35献祭者要像取出平安祭牲的脂肪一样,取出母绵羊的所有脂肪。祭司要把这一切放在坛上,与献给耶和华的祭物一起焚烧。这样,祭司为他赎了罪,他就会得到赦免。

Kiswahili Contemporary Version

Walawi 4:1-35

Sadaka Ya Dhambi

1Bwana akamwambia Mose, 24:2 Law 5:15-18; 22:14; Hes 15:22, 24-29; 35:11-15; Yos 20:3-9; Ebr 9:4; 1Sam 14:27; Za 19:12“Waambie Waisraeli: ‘Mtu yeyote afanyapo dhambi bila kukusudia na akatenda lile lililokatazwa katika amri yoyote ya Bwana:

34:3 Kut 12:5; 28:41; 30:10; Mwa 18:23; Law 3:12; 5:6-13; 9:2-22; 8:14; 10:16; 16:3-5; Hes 15:27; Za 66:15; Eze 43:19-23; Ebr 9:13-14“ ‘Ikiwa kuhani aliyetiwa mafuta amefanya dhambi na kuwaletea watu hatia, lazima alete kwa Bwana fahali mchanga asiye na dosari, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya dhambi aliyotenda. 44:4 Law 1:3; Hes 8:12; 19:4Atamkabidhi huyo fahali kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za Bwana. Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha huyo fahali na kumchinja mbele za Bwana. 54:5 Law 16:14Kisha kuhani huyo aliyetiwa mafuta atachukua sehemu ya damu ya huyo fahali na kuileta katika Hema la Kukutania. 64:6 Kut 24:8; 25:8; Law 16:14-19; Isa 42:21; Yn 8:20; Rum 3:24; 2Kor 5:19; Efe 2:13; Ufu 5:9Atachovya kidole chake katika hiyo damu na kuinyunyiza sehemu yake mara saba mbele za Bwana mbele ya pazia la mahali patakatifu. 74:7 Kut 27:2; 29:12; Law 8:15; 5:9; 9:9; 16:18; Ebr 9:21-25; Yos 7:11Kisha kuhani atatia sehemu ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu ya kufukizia uvumba wenye harufu nzuri iliyoko mbele za Bwana katika Hema la Kukutania. Damu iliyobaki ya huyo fahali ataimwaga chini ya hayo madhabahu ya kuteketezea sadaka kwenye ingilio la Hema la Kukutania. 8Atayaondoa mafuta yote ya fahali huyo wa sadaka ya dhambi, mafuta yale yanayofunika sehemu za ndani au zile zinazounganika nazo, 94:9 Law 3:4figo zote mbili na mafuta yaliyo juu yake karibu na kiuno na yale yanayofunika ini ambayo atayaondoa pamoja na figo zote, 104:10 Kut 32:2; 29:13kama vile mafuta yanayoondolewa kutoka kwenye maksai aliyetolewa sadaka ya amani. Kisha kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. 114:11 Kut 29:14; Law 8:17; 9:11; Hes 19:5; 4:12; Kut 29:14; Law 1:16; 6:11, 30; 8:17; 9:11; 10:14; Ebr 13:11; Hes 19:9Lakini ngozi ya huyo fahali na nyama zake zote, pamoja na kichwa na miguu yake, sehemu za ndani na matumbo, 12yaani sehemu nyingine zote zilizobaki za huyo fahali, lazima azitoe nje ya kambi mpaka mahali palipo safi kiibada, ambapo majivu hutupwa, naye atamchoma kwa moto juu ya kuni zilizoko juu ya lundo la majivu.

134:13 Hes 15:24-26“ ‘Ikiwa jumuiya yote ya Israeli watatenda dhambi pasipo kukusudia na kufanya lile lililokatazwa katika amri yoyote ya Bwana, hata kama jumuiya haifahamu juu ya jambo hilo, wana hatia. 144:14 Hes 15:24; 4:15; Kut 3:16; 19:7; 29:10; 2Nya 29:23; Hes 8:10; Isa 53:6; Mt 8:17; Ebr 9:2; 9:12-14Wanapotambua kuhusu dhambi waliyoitenda, lazima kusanyiko lilete fahali mchanga kuwa sadaka ya dhambi na kuikabidhi mbele ya Hema la Kukutania. 15Wazee wa jumuiya wataweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo fahali aliye mbele za Bwana, naye fahali atachinjwa mbele za Bwana. 16Kisha kuhani aliyetiwa mafuta ataiingiza sehemu ya damu ya huyo fahali ndani ya Hema la Kukutania. 174:17 Hes 19:4, 18Atachovya kidole chake kwenye damu na kuinyunyiza mara saba mbele za Bwana mbele ya hilo pazia. 184:18 Law 5:9; 6:30; 8:15; 10:18; 17:6; 2Nya 29:22Atatia sehemu ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu yaliyo mbele za Bwana katika Hema la Kukutania. Damu iliyobaki ataimwaga chini ya madhabahu ya kuteketezea sadaka, penye ingilio la Hema la Kukutania. 19Atayaondoa mafuta yote ya yule fahali na kuyateketeza juu ya madhabahu, 204:20 Kut 29:36; 32:30; Rum 3:25; Ebr 10:10-15; Hes 15:25; Dan 9:24naye atamfanyia fahali huyu kama alivyomfanyia yule fahali mwingine wa sadaka ya dhambi. Kwa njia hii kuhani atawafanyia watu upatanisho, nao watasamehewa. 214:21 Law 16:5, 15; 2Nya 29:21Kisha atamchukua yule fahali nje ya kambi na kumteketeza kama alivyomteketeza yule wa kwanza. Hii ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya jumuiya.

224:22 Hes 31:13“ ‘Wakati kiongozi ametenda dhambi bila kukusudia na kufanya yaliyokatazwa katika amri yoyote ya Bwana Mungu wake, ana hatia. 234:23 Law 1:10; Kut 18:21; Hes 16:2; Ezr 9:2; Mdo 3:17; 2Sam 21:1-3Atakapofahamishwa dhambi aliyotenda, ni lazima alete mbuzi dume asiye na dosari kama sadaka yake. 244:24 Law 6:25Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha yule mbuzi na kumchinja mahali pale ambapo sadaka za kuteketezwa huchinjiwa mbele za Bwana. Hii ni sadaka ya dhambi. 254:25 Law 9:9; 16:18; Eze 43:20-22Kisha kuhani atachukua sehemu ya damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuitia kwenye pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketeza, na kuimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu. 264:26 Kut 32:30; Law 5:10; 12:8; Hes 15:28Atayateketeza mafuta yote juu ya madhabahu, kama alivyoteketeza mafuta ya sadaka ya amani. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho wa dhambi kwa ajili ya yule mtu, naye atasamehewa.

274:27 Hes 15:27“ ‘Kama mtu katika jumuiya ametenda dhambi pasipo kukusudia na kufanya lile lililokatazwa katika amri yoyote ya Bwana, yeye ana hatia. 284:28 Eze 40:39; 44:27; Law 1:10Atakapofahamishwa dhambi yake aliyoitenda, ni lazima alete mbuzi jike asiye na dosari kama sadaka yake kwa ajili ya dhambi aliyotenda. 294:29 Law 1:4; Mwa 8:21Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka ya dhambi na kumchinjia mahali pa kuteketezea sadaka. 30Kisha kuhani atachukua sehemu ya ile damu kwa kidole chake na kuitia kwenye pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kuimwaga damu iliyobaki chini ya madhabahu. 314:31 Mwa 8:21; Law 1:4; 3:14; Kut 29:18; Ezr 6:10Atayaondoa mafuta yote, kama vile mafuta yaondolewavyo kwenye sadaka ya amani, naye kuhani atayateketeza juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa.

324:32 Kut 29:38; Law 9:3; 14:10; 1:3-4; Isa 53:7; Yn 1:29; Mdo 8:32; Ufu 5:6-14“ ‘Ikiwa ataleta mwana-kondoo kama sadaka yake ya dhambi, atamleta jike asiye na dosari. 33Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha huyo mwana-kondoo na kumchinja kwa ajili ya sadaka ya dhambi mahali sadaka ya kuteketezwa huchinjiwa. 34Kisha kuhani atachukua sehemu ya damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuitia juu ya pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na ile damu iliyobaki ataimwaga chini ya madhabahu. 35Ataondoa mafuta yote, kama vile mafuta yaondolewavyo kutoka kwenye mwana-kondoo wa sadaka ya amani, naye kuhani atayateketeza juu ya madhabahu juu ya zile sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto. Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi aliyoitenda, naye atasamehewa.