利未记 19 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

利未记 19:1-37

有关圣洁生活的条例

1耶和华对摩西说: 2“你要告诉以色列全体会众,‘你们要圣洁,因为我——你们的上帝耶和华是圣洁的。 3你们每个人都必须孝敬父母,遵守我的安息日。我是你们的上帝耶和华。 4不要祭拜虚无的神明,也不要为自己铸造神像。我是你们的上帝耶和华。 5你们献平安祭给我时,要使你们所献的蒙悦纳。 6要在献祭当天或第二天吃完祭物。如果第三天还有剩余,都要烧掉。 7如果有人第三天还吃那些祭物,祭物就不洁净,我不会悦纳。 8那人要自担罪责,因为他亵渎了我的圣物。要将他从民中铲除。

9“‘你们收割的时候,不要割净田角地边的庄稼,也不要捡那些掉在田里的穗子。 10不要摘净葡萄园里的葡萄,也不要捡掉在地上的葡萄。要把这些留给穷人和寄居在你们中间的外族人。我是你们的上帝耶和华。 11不可偷盗,不可撒谎,不可互相欺骗。 12不可奉我的名起假誓,从而亵渎你们上帝的名。我是耶和华。 13不可欺压邻居,也不可抢夺他的东西。要当天支付雇工的工钱,不可拖到第二天。 14不可咒骂耳聋的,也不可把绊脚石放在盲人面前,应当敬畏你们的上帝。我是耶和华。 15不可徇私枉法,不可偏袒穷人,不可谄媚权贵之人,要秉公审判。 16不可到处搬弄是非,不可危害邻居的生命安全。我是耶和华。 17对同胞不可心中怀恨。同胞有错,要当面指正,免得自己因他而担罪。 18不可报复,不可埋怨同胞,要爱邻如己。我是耶和华。

19“‘你们要遵守我的律例。不可让牲畜杂交;不可在同一块田播撒两种不同的种子;不可穿两种材料织成的衣服。

20“‘一个已经许配人的婢女尚未被赎或未获自由时,如果有人与她同寝,就要受到处罚,但不可处死他们,因为那婢女还未获自由。 21和她同寝的人要把一只公绵羊牵到会幕门口,作为赎过祭献给耶和华。 22祭司要用作赎过祭的公绵羊在耶和华面前为那人赎罪,他犯的罪便得到赦免。

23“‘你们到了迦南,在那里栽种各样果树后,前三年不可吃树上的果子,要视它们是不洁净的19:23 “不洁净的”希伯来文是“未受割礼的”。24第四年,树上的所有果子都是圣洁的,要献给耶和华作颂赞之祭。 25第五年,你们可以吃树上的果子。你们这样做,果树会为你们结出更多果子。我是你们的上帝耶和华。

26“‘不可吃带血的肉,不可占卜或行巫术。 27不可修剪鬓角或胡须。 28不可因哀悼死人而割伤身体,也不可纹身。我是耶和华。 29不可辱没自己的女儿,使她沦为娼妓,免得你们居住的地方充满淫乱和邪恶。 30要遵守我的安息日,敬畏我的圣所。我是耶和华。 31不可求问灵媒或巫师,玷污自己。我是你们的上帝耶和华。

32“‘在年长者面前,要恭敬站立,要敬重年长者。要敬畏你们的上帝。我是耶和华。 33不可欺负住在你们境内的外族人, 34要视他们如同胞,爱他们如爱自己,因为你们也曾经寄居埃及。我是你们的上帝耶和华。 35在称重和度量时,不可欺诈。 36要使用准确的秤、尺子和升斗。我是你们的上帝耶和华,曾带领你们离开埃及37你们要遵行我的一切律例和典章。我是耶和华。’”

Kiswahili Contemporary Version

Walawi 19:1-37

Sheria Mbalimbali

1Bwana akamwambia Mose, 2“Sema na kusanyiko lote la Israeli na uwaambie: ‘Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi, Bwana Mungu wenu, ni mtakatifu.

319:3 Kut 20:8, 12; Law 11:44; Neh 9:14; 13:15-21; Isa 58:13; Mk 2:27“ ‘Kila mmoja wenu ni lazima amheshimu mama yake na baba yake, na pia ni lazima kuzishika Sabato zangu. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.

419:4 Kut 20:4; Amu 17:3; Za 96:5; 115:4-7; 135:15; 1Kor 10:14“ ‘Msiabudu sanamu, wala msijitengenezee miungu ya shaba. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.

5“ ‘Mnapotoa dhabihu ya sadaka ya amani kwa Bwana, toeni kwa namna ambayo itakubaliwa kwa niaba yenu. 619:6 Law 7:16-18Sadaka hiyo italiwa siku iyo hiyo mnayoitoa, au kesho yake; chochote kitakachobaki hadi siku ya tatu lazima kiteketezwe kwa moto. 7Kama sehemu yoyote ya sadaka hiyo italiwa siku ya tatu, itakuwa si safi, nayo haitakubaliwa. 819:8 Law 22:2, 15-16; Hes 18:32; Mwa 17:14Yeyote atakayekula atawajibishwa, kwa sababu amenajisi kitu kilicho kitakatifu kwa Bwana; mtu huyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.

919:9 Rut 2:2-7; Law 23:10, 22; Kum 24:19-22; Ay 24:10; Kut 23:11; Kum 15:1-18“ ‘Wakati uvunapo mavuno ya nchi yako, usivune hadi kwenye mipaka ya shamba lako, wala usikusanye mabaki ya mavuno yako. 1019:10 Kum 24:19-22; Za 140:12; Mit 14:31; Isa 3:12-15; Mhu 5:8Usirudi mara ya pili katika shamba lako la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini. Ziache kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

1119:11 Kut 20:15-16; 23:4; Lk 3:14; Efe 4:25; Law 6:2; 1Fal 13:18; Yer 9:3-5; Mdo 5:3-4“ ‘Usiibe.

“ ‘Usiseme uongo.

“ ‘Msidanganyane.

1219:12 Yer 5:2; 7:9; 34:16; 44:16, 26; Mal 3:5; Kut 3:13; 20:7; Kum 18:19; Mit 18:10; Isa 42:8; Mt 5:33“ ‘Usiape kwa uongo kwa Jina langu, na hivyo kulinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.

1319:13 Law 25:14, 17; Kut 20:15; 22:15, 25-27; Ay 7:2; 24:12; 31:39; Isa 16:14; Mal 3:5; Kum 24:15; Yer 22:13; Mt 20:8; 1Tim 5:18; Yak 5:4“ ‘Usimdhulumu wala kumwibia jirani yako.

“ ‘Usishikilie mshahara wa kibarua usiku kucha hadi asubuhi.

1419:14 Kut 4:11; Law 21:18; 25:17, 36; Kum 27:18; Rum 14:13; 1Pet 2:17“ ‘Usimlaani kiziwi, wala usiweke kikwazo mbele ya kipofu, lakini umche Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.

1519:15 Kut 13:2; 23:8; Kum 24:17; Ay 13:8, 10; 32:21; 34:19; Mit 24:23; 28:21; Mal 2:9; Yak 2:1-4“ ‘Usipotoshe haki; usionyeshe kumpendelea maskini, wala upendeleo kwa mwenye cheo, bali mwamulie jirani yako kwa haki.

1619:16 Za 15:3, 5; 31:13; 41:6; 101:5; Yer 6:28; 9:4; Eze 22:9, 12; Kut 23:7; Kum 10:17; 27:25“ ‘Usieneze uchochezi miongoni mwa watu wako.

“ ‘Usifanye kitu chochote kile kinachohatarisha maisha ya jirani yako. Mimi ndimi Bwana.

1719:17 1Yn 2:9; Mt 18:15; Lk 17:3; Mwa 27:41“ ‘Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Karipia jirani yako kwa uwazi ili usishiriki hatia yake.

1819:18 Mwa 4:23; Rum 12:19; 13:9; Ebr 10:30; Za 103:9; Kut 20:16; Mt 5:43; 19:16; 22:39; Mk 12:31; Lk 10:27; Yn 13:34; Gal 5:14; Yak 2:8“ ‘Usijilipizie kisasi wala kuwa na kinyongo dhidi ya mmoja wa jamaa yako, lakini mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Bwana.

1919:19 Mwa 26:5; Kum 22:9, 11“ ‘Mtazishika amri zangu.

“ ‘Usiwaache wanyama wako wa kufugwa wakazaana na wengine wa aina tofauti.

“ ‘Usipande mbegu za aina mbili katika shamba lako.

“ ‘Usivae nguo iliyofumwa kwa nyuzi za aina mbili tofauti.

2019:20 Kum 22:23-27“ ‘Kama mwanaume anakutana kimwili na mwanamke ambaye ni msichana mtumwa aliyeposwa na mwanaume mwingine, lakini ambaye hajakombolewa wala hajapewa uhuru, lazima iwepo adhabu inayofaa. Hata hivyo hawatauawa, kwa sababu msichana alikuwa bado hajaachwa huru. 2119:21 Law 5:15Lakini huyo mtu lazima alete kondoo dume kwenye ingilio la Hema la Kukutania kwa ajili ya sadaka ya hatia kwa Bwana. 22Kupitia kwa huyo kondoo dume wa sadaka ya hatia, kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Bwana kwa ajili ya dhambi aliyotenda, naye atasamehewa dhambi yake.

23“ ‘Mtakapoingia katika hiyo nchi na kupanda aina yoyote ya mti wa matunda, hesabuni matunda yake kama yaliyokatazwa. Kwa miaka mitatu mtayahesabu kwamba yamekatazwa; hayaruhusiwi kuliwa. 2419:24 Kut 22:29; Mit 3:9; Kum 12:17-18Katika mwaka wa nne matunda yote ya mti huo yatakuwa matakatifu, sadaka ya sifa kwa Bwana. 25Bali katika mwaka wa tano mnaweza kula matunda ya mti huo. Kwa njia hii mavuno yenu yataongezewa. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

2619:26 Mwa 9:4; 30:27; Isa 44:25; Eze 22:18; 2Fal 17:17“ ‘Msile nyama yoyote yenye damu ndani yake.

“ ‘Msifanye uaguzi wala uchawi.

2719:27 Law 21:5; 2Sam 10:4-5; Yer 41:5; 48:37; Eze 5:1-5; Yer 9:26“ ‘Msikate nywele za kichwa denge, wala kunyoa pembe za ndevu zenu.

2819:28 Law 21:5; 1Fal 18:28; Yer 16:6; 41:5; 47:5“ ‘Msichanje chale miili yenu kwa ajili ya mfu, wala msijichore alama juu ya miili yenu. Mimi ndimi Bwana.

2919:29 Law 21:9; Kum 23:18; Mwa 34:7“ ‘Usimdhalilishe binti yako kwa kumfanya kahaba, la sivyo nchi itageukia ukahaba na kujaa uovu.

3019:30 Kut 20:8; Law 26:2“ ‘Shika Sabato zangu na kuheshimu mahali pangu patakatifu. Mimi ndimi Bwana.

3119:31 Kut 22:18; 1Sam 28:7-20; 1Nya 10:13; Law 20:6; 2Fal 21:6; 23:24; Isa 8:19; 19:3; 29:4; 47:12; 65:4“ ‘Msiende kwa waaguzi, wala msitafute wapunga pepo, kwa maana watawanajisi. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

3219:32 1Fal 12:8; Ay 29:8; 32:4; Mit 23:22; Mao 5:12; 1Tim 5:1; Law 11:44“ ‘Uwapo mbele ya mzee, simama ili kuonyesha heshima kwa wazee, nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.

33“ ‘Wakati mgeni anaishi pamoja nawe katika nchi yako, usimnyanyase. 3419:34 Kut 12:48; 22:21; 23:9; Kum 10:19; 23:7; Za 146:9Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

3519:35 Kum 25:13-16“ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi. 3619:36 Ay 31:6; Mit 11:1; 20:10; Hes 12:7; Mik 6:11; Amu 6:19; Rut 2:17; 1Sam 1:24; 17:17; Eze 45:10-11; Kum 25:13-15; Kut 12:17Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efa19:36 Efa kilikuwa kipimo cha vitu vikavu. halali, na hini19:36 Hini kilikuwa kipimo cha vitu vimiminika. halali. Mimi ndimi Bwana Mungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri.

3719:37 2Fal 17:37; 2Nya 7:17; Za 119:5; Eze 18:9; Mwa 26:5; Kum 6:25; Law 18:4-5“ ‘Shika amri zangu zote na sheria zangu zote, nawe uzifuate. Mimi ndimi Bwana.’ ”