列王纪上 16 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

列王纪上 16:1-34

1耶和华吩咐哈拿尼的儿子耶户先知责备巴沙说: 2“我从尘土中提拔你,立你为我以色列子民的首领,你却重蹈耶罗波安的覆辙,使我的子民陷入罪中,惹我发怒。 3所以我必除掉你和你全家,像除掉尼八的儿子耶罗波安家一样。 4你家人中,死在城中的必被狗吃,死在野外的必被鸟吃。”

5巴沙其他的事迹和功业都记在《以色列列王史》上。 6巴沙与祖先同眠后葬在得撒,他儿子以拉继位。 7耶和华借哈拿尼的儿子耶户先知谴责巴沙和他全家,是因为他像耶罗波安家一样做耶和华视为恶的事,惹耶和华发怒,也因为他杀了耶罗波安全家。

以拉做以色列王

8犹大亚撒执政第二十六年,巴沙的儿子以拉得撒登基做以色列王,执政两年。 9以拉的一半战车由部下心利掌管。心利却背叛他,趁他在得撒宫廷总管亚杂家中喝醉时, 10进去杀了他,篡了位。那一年是亚撒犹大王第二十七年。

11心利一登基做王,就杀了巴沙全家,他亲友家的男子也无一幸免。 12巴沙惨遭灭门之祸,正应验了耶和华借耶户先知谴责他的话。 13这是因为巴沙以拉父子二人作恶多端,祭拜假神,使以色列人陷入罪中,惹以色列的上帝耶和华发怒。 14以拉其他的事及一切所为都记在《以色列列王史》上。

心利做以色列王

15犹大亚撒执政第二十七年,心利开始在得撒做王,执政仅七天。那时以色列军正在攻打非利士基比顿城。 16他们听说心利谋反弑君,就在当天拥立军中元帅暗利以色列王。 17暗利率领以色列军离开基比顿,上去围攻得撒18心利见城被攻破,就走进王宫的城堡中放火烧宫,自焚而死。 19这是因为他犯罪,行耶和华视为恶的事,步耶罗波安的后尘,使以色列人陷入罪中。 20心利其他的事及其谋反篡位的经过,都记在《以色列列王史》上。

暗利做以色列王

21那时,以色列人分为两派,一派拥立基纳的儿子提比尼做王,另一派支持暗利22暗利一派强于提比尼一派。提比尼死后,暗利做了王。

23犹大亚撒执政第三十一年,暗利登基做以色列王,执政共十二年,其中六年在得撒24暗利用了一千四百两银子向撒玛买了撒玛利亚山,在上面建了一座城,按原来主人撒玛的名字称之为撒玛利亚25暗利做耶和华视为恶的事,比以前的诸王更坏。 26他步尼八的儿子耶罗波安的后尘,使以色列人陷入罪中,祭拜假神,惹以色列的上帝耶和华发怒。 27暗利其他的事及一切所为都记在《以色列列王史》上。 28暗利与祖先同眠后葬在撒玛利亚,他儿子亚哈继位。

亚哈做以色列王

29犹大亚撒执政第三十八年,暗利的儿子亚哈登基做以色列王,他在撒玛利亚执政二十二年。 30暗利的儿子亚哈做耶和华视为恶的事,比以前的诸王更坏。 31他不但步尼八的儿子耶罗波安的后尘,还娶了西顿叶巴力的女儿耶洗别为妻,供奉、祭拜巴力32他在撒玛利亚巴力建庙,在庙里为巴力设立祭坛。 33他还造了亚舍拉神像,所作所为比先前诸王更惹以色列的上帝耶和华发怒。 34亚哈执政期间,伯特利希伊勒重建耶利哥城。他立地基的时候,长子亚比兰死了;安城门的时候,幼子西割死了。这应验了耶和华借的儿子约书亚说的话。

Kiswahili Contemporary Version

1 Wafalme 16:1-34

116:1 1Fal 16:7; 2Nya 19:2Ndipo neno la Bwana likamjia Yehu mwana wa Hanani dhidi ya Baasha, kusema: 216:2 1Fal 14:7-9“Nilikuinua kutoka mavumbini na kukufanya kiongozi wa watu wangu Israeli, lakini ukaenenda katika njia za Yeroboamu na kusababisha watu wangu Israeli kutenda dhambi na kunikasirisha kwa dhambi zao. 316:3 1Fal 16:11; 21:22Basi nitamwangamiza Baasha pamoja na nyumba yake, nami nitaifanya nyumba yako kama ile ya Yeroboamu mwanawe Nebati. 416:4 1Fal 14:11Mbwa watawala watu wa Baasha watakaofia mjini na ndege wa angani watajilisha kwa wale watakaofia mashambani.”

5Kwa matukio mengine ya utawala wa Baasha, aliyoyafanya na mafanikio yake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 6Baasha akalala na baba zake naye akazikwa huko Tirsa. Naye Ela mwanawe akawa mfalme baada yake.

716:7 1Fal 16:11Zaidi ya hayo, neno la Bwana likamjia Baasha pamoja na nyumba yake kupitia kwa nabii Yehu mwana wa Hanani, kwa sababu ya maovu yote aliyokuwa ametenda machoni pa Bwana, akamkasirisha kwa mambo aliyotenda, na kuwa kama nyumba ya Yeroboamu, na pia kwa sababu aliiangamiza.

Ela Mfalme Wa Israeli

8Katika mwaka wa ishirini na sita wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala huko Tirsa kwa miaka miwili.

916:9 1Fal 20:12; Mit 31:4-5Zimri, mmoja wa maafisa wake, aliyekuwa na amri juu ya nusu ya magari yake ya vita, akafanya hila mbaya dhidi ya Ela. Wakati huo Ela alikuwa Tirsa, akilewa katika nyumba ya Arsa, mtu aliyekuwa msimamizi wa jumba la kifalme huko Tirsa. 1016:10 2Fal 9:31Zimri akaingia, akampiga na kumuua katika mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda. Kisha Zimri akaingia mahali pake kuwa mfalme.

11Mara tu alipoanza kutawala na kuketi juu ya kiti cha ufalme, aliua jamaa yote ya Baasha. Hakumwacha mwanaume hata mmoja, akiwa ni ndugu au rafiki. 12Hivyo Zimri akaangamiza jamaa yote ya Baasha, kulingana na neno la Bwana lililonenwa dhidi ya Baasha kupitia nabii Yehu: 1316:13 Kum 32:21kwa sababu ya dhambi zote Baasha na mwanawe Ela walizokuwa wametenda na wakasababisha Israeli kuzitenda, basi wakamkasirisha Bwana, Mungu wa Israeli kwa sanamu zao zisizofaa.

14Kwa matukio mengine ya utawala wa Ela, na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?

Zimri Mfalme Wa Israeli

1516:15 Yos 19:44Katika mwaka wa ishirini na saba wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri akatawala huko Tirsa siku saba. Jeshi lilikuwa limepiga kambi karibu na Gibethoni, mji wa Wafilisti. 16Wakati Waisraeli waliokuwa kambini waliposikia kuwa Zimri alikuwa amefanya hila mbaya dhidi ya mfalme na kumuua, wakamtangaza Omri, jemadari wa jeshi, kuwa mfalme wa Israeli siku iyo hiyo huko kambini. 17Ndipo Omri na Waisraeli wote pamoja naye wakaondoka Gibethoni na kuizingira Tirsa. 18Wakati Zimri alipoona kuwa mji umechukuliwa, alikwenda ndani ya ngome ya jumba la kifalme na kulichoma moto jumba la kifalme na kujiteketeza ndani yake. Kwa hiyo akafa, 19kwa sababu ya dhambi alizofanya, akitenda maovu machoni pa Bwana na kuenenda katika njia za Yeroboamu na katika dhambi alizofanya na kusababisha Israeli kuzifanya.

20Kwa matukio mengine ya utawala wa Zimri, na uasi alioutenda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?

Omri Mfalme Wa Israeli

21Ndipo watu wa Israeli wakagawanyika katika makundi mawili, nusu wakamuunga mkono Tibni mwana wa Ginathi ili awe mfalme na nusu nyingine wakamuunga mkono Omri. 22Lakini wafuasi wa Omri wakajionyesha wenye nguvu kuliko wale wa Tibni mwana wa Ginathi. Hivyo Tibni akafa na Omri akawa mfalme.

2316:23 Yos 12:24Katika mwaka wa thelathini na moja wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala kwa miaka kumi na miwili, sita kati ya hiyo katika Tirsa. 2416:24 1Fal 13:32; Mt 10:5Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta mbili16:24 Talanta mbili za fedha ni sawa na kilo 70. za fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho.

2516:25 Kum 4:25; Mik 6:16Lakini Omri akatenda maovu machoni pa Bwana na kutenda dhambi kuliko wote waliomtangulia. 2616:26 Kum 32:21Akaenenda katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake, ambazo alisababisha Israeli kutenda, hivyo basi wakamkasirisha Bwana, Mungu wa Israeli kwa sanamu zao zisizofaa.

27Kwa matukio mengine ya utawala wa Omri, yale aliyofanya na vitu alivyovifanikisha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli? 2816:28 1Fal 13:32Omri akalala pamoja na baba zake na akazikwa huko Samaria. Ahabu mwanawe akatawala mahali pake.

Ahabu Afanywa Mfalme Wa Israeli

29Katika mwaka wa thelathini na nane wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Ahabu mwana wa Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala Israeli akiwa Samaria kwa miaka ishirini na miwili. 3016:30 1Fal 14:9Ahabu mwana wa Omri akafanya maovu zaidi machoni mwa Bwana kuliko yeyote aliyewatangulia. 3116:31 1Fal 11:2; 2Fal 9:34; Amu 3:6Kama vile haikutosha kuishi kama Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti wa Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, naye akaanza kumtumikia Baali na kumwabudu. 3216:32 Amu 6:28; Yer 43:12Akajenga madhabahu kwa ajili ya Baali katika hekalu la Baali lile alilolijenga huko Samaria. 3316:33 Amu 3:7; 2Fal 13:6Pia Ahabu akatengeneza nguzo ya Ashera na kufanya mengi ili kumkasirisha Bwana, Mungu wa Israeli, kuliko walivyofanya wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.

3416:34 Yos 6:26Katika wakati wa Ahabu, Hieli, Mbetheli, akaijenga upya Yeriko. Aliweka misingi yake kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza Abiramu, na kuweka malango yake kwa gharama ya mwanawe mdogo Segubu, kulingana na neno la Bwana alilosema kupitia Yoshua mwana wa Nuni.