出埃及记 12 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

出埃及记 12:1-51

逾越节

1耶和华在埃及摩西亚伦说: 2“你们要以这个月为一月,为一年之首。 3你要向以色列全体会众宣布,本月的第十日,每家都要预备一只羊羔,一家一只。 4倘若家人太少,吃不了一只,可以跟最近的邻居共享一只,你们要按人数和各人的食量预备羊羔。 5羊羔必须是毫无残疾、一岁的公绵羊或公山羊。 6以色列全体会众要把羊留到本月十四日,在黄昏时分宰杀, 7然后取点血涂在房子的门框和门楣上,他们要在房子里吃羊肉。 8当晚,你们要用火把羊肉烤熟,与无酵饼和苦菜一起吃。 9不可吃生羊肉,也不可煮着吃,要把整只羊,连头带腿和内脏一并烤着吃。 10不可把肉留到早晨,留到早晨的肉要烧掉。 11你们吃的时候,要束腰、穿鞋、手中拿杖,要赶快吃,这是耶和华的逾越节。

12“因为那一夜我要巡遍埃及,把境内所有长子和头生的牲畜全都杀掉,也要严惩埃及所有的神明。我是耶和华。 13涂在你们房屋上的血是一个记号,我见到这血就会越过你们。我击打埃及的时候,那灾祸不会落到你们身上。 14你们要记住这一天,守为耶和华的节期,作为世代不变的律例。

除酵节

15“七天之内你们都要吃无酵饼。第一天,要清除家中所有的酵。任何人若在这七天当中吃有酵的食物,要将他从以色列人中铲除。 16在节期的第一天和第七天,你们都要举行圣会。这两天所有人都不得工作,除了预备各人要吃的以外,不可做任何工。 17你们要守这除酵节,因为我在这天把你们的大军从埃及领了出来。你们要守这节期,作为世代不变的律例。 18从一月十四日傍晚开始,直到二十一日傍晚,你们都要吃无酵饼。 19在这七天内,你们屋里不能有酵。任何人若吃了有酵的东西,不论他是寄居者还是本地人,都要将他从以色列会众中铲除。 20无论你们住在哪里都要吃无酵饼,不能吃任何有酵的食物。”

21于是,摩西召集以色列的众长老,对他们说:“你们家家户户都要挑选羔羊,把这逾越节的羔羊宰了。 22拿一把牛膝草蘸盆里的血,把血涂在门楣和两边的门框上。天亮前,你们不可踏出门外。 23因为耶和华要巡行各地,击杀埃及人,祂看见你们的门框和门楣上有血,就必越过你们的家门,不让灭命者进你们家杀人。 24这是你们及后代永远当守的律例。 25你们进入耶和华应许给你们的地方以后,要守这逾越节。 26当你们的儿女问你们守这节期的意义时, 27你们就说,‘这是献给耶和华逾越节的祭,因为我们从前在埃及时,祂击杀埃及人,却越过以色列人所住的房子,救了我们各家。’”百姓听了摩西这番话,都俯伏敬拜。 28耶和华怎么吩咐摩西亚伦以色列人就照样遵行。

29到了半夜,耶和华把所有埃及人的长子都杀了,包括坐王位的法老的长子、牢中囚犯的长子和一切头生的牲畜。 30当晚,法老及其臣仆和所有埃及人都惊醒了,到处都是哭号声,因为没有一家不死人的。 31法老连夜召见摩西亚伦,对他们说:“你们和以色列人起来走吧,离开我的人民。就照你们的要求,去事奉耶和华吧! 32照你们的要求,把所有的牛羊都带走吧!也要为我祝福。” 33埃及人催促以色列人赶快离开埃及,因为他们说:“我们都要死了。” 34于是,以色列百姓就把没有酵的面团放在揉面盆里,用衣服包起来扛在肩上, 35又遵照摩西的吩咐向埃及人索取金器、银器和衣服。 36耶和华使埃及人恩待以色列人,他们要什么,埃及人就给什么。这样,以色列人夺取了埃及人的财富。

37以色列百姓从埃及兰塞启行,前往疏割,妇女孩童不算在内,单是步行的男子就有六十万, 38同行的还有许多外族人和大群的牛羊。 39他们用从埃及带出来的面团烤成无酵饼,面团没有酵,因为他们被催促离开埃及,没有时间准备食物。 40以色列人在埃及共住了四百三十年, 41正好满了四百三十年的那一天,耶和华带领全军离开了埃及42那天晚上是耶和华把祂的子民带出埃及之夜,因此以后世世代代的以色列人都要在那日守夜,以尊崇耶和华。

43耶和华对摩西亚伦说:“以下是逾越节的条例。

“所有外族人都不可吃逾越节的羊羔, 44但那些买来的奴隶若接受了割礼,就可以吃。 45寄居的外族人和雇工不可吃。 46你们吃的时候,应当在房子里吃,不得把肉带到外面去,也不可折断羊羔的一根骨头。 47以色列全体会众都要守这节期。 48跟你们住在一起的外族人如果想为耶和华守逾越节,他全家的男子都必须接受割礼,这样才可以像以色列人一样守逾越节,但没有接受割礼的人绝不可吃逾越节的羊羔。 49本地人和在你们中间寄居的外族人都要遵守这规矩。”

50耶和华怎样吩咐摩西亚伦以色列百姓都遵命而行。 51就在那一天,耶和华带领以色列大军离开了埃及

Kiswahili Contemporary Version

Kutoka 12:1-51

Pasaka

1Bwana akamwambia Mose na Aroni katika nchi ya Misri, 212:2 Kut 13:4; 23:15; 34:18; 40:2; Kum 16:1; Kut 12:18“Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu, yaani mwezi wa kwanza wa mwaka wenu. 312:3 Mk 14:12; 1Kor 5:7Iambie jumuiya yote ya Israeli kwamba katika siku ya kumi ya mwezi huu, kila mtu atatwaa mwana-kondoo mmoja kwa ajili ya familia yake, mmoja kwa kila nyumba. 4Ikiwa nyumba yoyote ina watu wachache wasioweza kumaliza huyo mwana-kondoo mzima, nyumba hiyo itabidi ishirikiane na nyumba ya jirani wa karibu, baada ya kuzingatia idadi ya watu waliomo. Mtaangalia ni kiasi gani cha nyama kitahitajika kulingana na mahitaji ya kila mtu. 512:5 Kut 29:1; Law 1:3; 3:1; 4:3; 22:18-21; 23:12; Hes 6:14; 15:8; 28:3; Kum 15:21; 17:1; Ebr 9:14; 1Pet 1:19Wanyama mtakaowachagua, lazima wawe wa kiume wa umri wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari, mwaweza kuwachukua kati ya kondoo au mbuzi. 612:6 Law 23:5; Hes 9:1-11; Yos 5:10; 2Nya 30:2; Kut 16:12; Kum 16:4-6Tunzeni wanyama hao mpaka siku ya kumi na nne ya mwezi, ambapo lazima watu wa jumuiya yote ya Israeli wachinje wanyama hao wakati wa jioni. 712:7 Eze 9:6Ndipo watakapochukua baadhi ya hiyo damu na kuipaka kwenye vizingiti vya juu na miimo ya milango ya nyumba ambamo watakula wana-kondoo hao. 812:8 Kut 16:19; 23:18; 34:25; Law 7:15; Hes 9:11; Kut 13:3; Kum 16:3-7; 2Nya 35:13; 1Kor 5:8Usiku huo huo watakula nyama iliyookwa kwenye moto, pamoja na mboga chungu za majani na mikate isiyotiwa chachu. 912:9 Kut 29:13-22; Law 3:3Msile nyama mbichi wala iliyochemshwa, lakini iwe imeokwa kwenye moto, kichwa, miguu na nyama zake za ndani. 1012:10 Kut 13:7; 29:34; Law 22:30; Kum 16:4Msibakize nyama yoyote mpaka asubuhi; nazo kama zitabakia mpaka asubuhi, lazima mziteketeze kwa moto. 1112:11 Kum 16:3; Isa 48:20; 52:11; Law 23:5; Hes 9:2-4; 28:16; Kum 16:1; Yos 5:10; 2Fal 23:21-23; 2Nya 30:1; Ezr 6:19; Isa 31:5; Eze 45:21Hivi ndivyo mtakavyokula: Mtajifunga mikanda viunoni, mtakuwa mmevaa viatu vyenu miguuni na kushika fimbo zenu mkononi mwenu. Mle kwa haraka; hii ni Pasaka ya Bwana.

1212:12 Amo 5:17; Isa 10:33; 31:8; 37:36; Kut 4:23; 13:15; 15:11; 18:11; Hes 33:4; 2Nya 2:5; Za 95:3; 97:9; 135:5; Isa 19:1; Kut 11:4; Yer 43:12; 44:8; Kut 6:2“Usiku huo huo nitapita katika nchi yote ya Misri na kumuua kila mzaliwa wa kwanza, wa wanadamu na wa wanyama, nami nitaihukumu miungu yote ya Misri. Mimi ndimi Bwana. 1312:13 Ebr 11:28; Kut 8:23Damu itakuwa ishara kwa ajili yenu ya kuonyesha nyumba ambazo mtakuwamo; nami nitakapoiona damu, nitapita juu yenu. Hakuna pigo la uharibifu litakalowagusa ninyi nitakapoipiga Misri.

1412:14 Kut 13:9; 23:14; 32:5; 13:5, 10; 27:21; Law 3:17; 10:9; 16:29; 23:14; 24; 3; Hes 18:23“Siku hii itakuwa kumbukumbu kwenu, mtaiadhimisha kuwa sikukuu kwa Bwana, katika vizazi vyenu vyote: mtaishika kuwa amri ya kudumu. 1512:15 Kut 13:6-7; 23:15; 34:18; Law 23:6; Hes 28:17; Kum 16:3; 1Kor 5:7; Mwa 17:14; Hes 9:13Kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu. Katika siku ya kwanza mtaondoa chachu yote ndani ya nyumba zenu, kwa maana yeyote atakayekula chochote chenye chachu kuanzia siku ya kwanza hadi ya saba lazima akatiliwe mbali kutoka Israeli. 1612:16 Hes 29:35Katika siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu, na kusanyiko jingine katika siku ya saba. Katika siku hizo msifanye kazi kamwe isipokuwa kutayarisha chakula cha kila mmoja; hilo ndilo tu mtakalofanya.

1712:17 Kut 23:15; 34:18; Kum 16:16; 2Nya 8:13; 30:21; Ezr 6:22; Mt 26:17; Lk 22:1; Mdo 12:3; Kut 6:6, 26; 13:3; Law 19:36; 3:17“Mtaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, kwa sababu hiyo ndiyo siku ile niliyovitoa vikosi vyenu kutoka Misri. Mtaiadhimisha siku hii kwa vizazi vyenu vyote kuwa amri ya kudumu. 1812:18 Law 23:5-8; Hes 28:16-25Katika mwezi wa kwanza mtakula mikate isiyotiwa chachu, kuanzia jioni ya siku ya kumi na nne hadi jioni ya siku ya ishirini na moja. 1912:19 Mwa 17:14; Hes 9:14; 15:14; 35:15; Kum 1:16; Yos 8:33Kwa muda wa siku saba isionekane chachu yoyote katika nyumba zenu. Yeyote alaye chochote chenye chachu ndani yake, lazima akatiliwe mbali kutoka jumuiya ya Israeli, akiwa ni mgeni au mzawa. 2012:20 Law 3:17; Hes 35:29; Eze 6:6; Kut 13:6Msile chochote kilichotiwa chachu. Popote muishipo, ni lazima mle mikate isiyotiwa chachu.”

2112:21 Mk 14:12-16; Kut 12:11Ndipo Mose akawaita wazee wote wa Israeli na kuwaambia, “Nendeni mara moja mkachague wanyama kwa ajili ya jamaa zenu, mkachinje mwana-kondoo wa Pasaka. 2212:22 Law 14:4-6; Hes 19:18; Za 51:7; Ebr 11:28; Kut 12:7Chukueni kitawi cha hisopo, kichovyeni kwenye damu iliyopo kwenye sinia na kuipaka baadhi ya hiyo damu kwenye vizingiti na kwenye miimo yote miwili ya milango. Mtu yeyote asitoke nje ya mlango wa nyumba yake mpaka asubuhi. 2312:23 Isa 19:22; Ufu 7:3; Mwa 16:7; Isa 37:36; Kut 12:7, 13; Yer 6:26; 48:8; 1Kor 10:10; Ebr 11:28Bwana apitapo katika nchi yote kuwapiga Wamisri, ataiona damu juu ya vizingiti na kwenye miimo ya milango, naye atapita juu, wala hatamruhusu mwangamizi kuingia katika nyumba zenu na kuwapiga ninyi.

24“Shikeni maagizo haya yawe kanuni ya kudumu kwenu na kwa ajili ya wazao wenu. 2512:25 Mwa 15:14; Kut 3:17Mtakapoingia katika nchi Bwana atakayowapa kama alivyoahidi, shikeni desturi hii. 2612:26 Kut 10:2; 13:8; Yos 4:6Watoto wenu watakapowauliza, ‘Sikukuu hii ina maana gani kwenu?’ 2712:27 Kut 8:23; 12:11; Mwa 24:26; Kut 4:31Basi waambieni, ‘Hii ni dhabihu ya Pasaka kwa Bwana, ambaye alipita juu ya nyumba za Waisraeli katika nchi ya Misri na hakudhuru nyumba zetu alipowapiga Wamisri.’ ” Ndipo watu wa Israeli waliposujudu na kuabudu. 28Waisraeli wakafanya kama vile Bwana alivyomwagiza Mose na Aroni.

2912:29 Kut 11:4; Mwa 19:13; Kut 4:23; 9:6; Za 78:51Ilipofika usiku wa manane, Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, mrithi wa kiti cha ufalme, hadi mzaliwa wa kwanza wa mfungwa, aliyekuwa gerezani, na wazaliwa wa kwanza wa mifugo yote pia. 3012:30 Kut 11:6Farao, na maafisa wake wote, na Wamisri wote wakaamka usiku, na kulikuwa na kilio kikubwa katika nchi ya Misri, kwa kuwa haikuwepo nyumba ambayo hakufa mtu.

Kutoka

3112:31 Kut 8:8Wakati huo Farao akawaita Mose na Aroni na kuwaambia, “Ondokeni! Tokeni kwa watu wangu, ninyi pamoja na Waisraeli! Nendeni mkamwabudu Bwana kama mlivyoomba. 3212:32 Kut 10:9, 26; Mwa 27:34Chukueni makundi yenu ya kondoo na mbuzi pamoja na ngʼombe, kama mlivyosema, nanyi mwende zenu. Nanyi pia mnibariki.”

3312:33 Kut 6:1; 1Sam 6:6; Mwa 20:3; Kut 8:19; Za 105:38Wamisri wakawahimiza Waisraeli waondoke kwa haraka na kuacha nchi yao. Kwa kuwa walisema, “La sivyo, tutakufa wote!” 34Hivyo watu wakachukua donge lao la unga kabla ya kutiwa chachu, wakaweka ndani ya mabakuli ya kukandia, wakayaviringisha katika vitambaa na kuyabeba mabegani mwao. 3512:35 Kut 3:22; Mwa 24:53Waisraeli wakafanya kama Mose alivyowaelekeza, nao wakawaomba Wamisri wawapatie vitu vya fedha, dhahabu na nguo. 3612:36 Mwa 39:21; Kut 3:22Basi Bwana alikuwa amewafanya Wamisri kuwa wakarimu kwa hawa watu, wakawapatia Waisraeli vile walivyotaka kwao; kwa hiyo wakawateka nyara Wamisri.

3712:37 Mwa 47:11; Kut 13:20; Hes 33:3-5; Mwa 12:2; Kut 38:26; Hes 1:46; 2:32; 11:13-21; 26:51Waisraeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi. Walikuwepo wanaume wapatao 600,000 waendao kwa miguu bila kuhesabu wanawake na watoto. 3812:38 Hes 11:4; Yos 8:35Watu wengine wengi wakafuatana nao, pamoja na makundi makubwa ya mifugo wakiwemo kondoo, mbuzi na ngʼombe. 3912:39 Kut 3:20; 6:1; 11:1Wakatengeneza maandazi yasiyotiwa chachu kwa ule unga uliokandwa waliokuwa wameutoa Misri, donge hilo la unga halikuwa limetiwa chachu, kwa kuwa walikuwa wameondolewa Misri kwa haraka nao hawakuwa na muda wa kuandaa chakula chao.

4012:40 Mwa 15:13; Mdo 7:6; Gal 3:17Waisraeli walikuwa wameishi Misri kwa muda wa miaka 430. 4112:41 Kut 6:26; 3:10; 12:17Ilikuwa ni siku ya mwisho ya hiyo miaka 430, vikosi vyote vya Bwana vilipokuwa vimeondoka Misri. 4212:42 Kut 13:10; Law 3:17; Hes 9:3; Kum 16:1, 6Kwa sababu Bwana aliutenga usiku ule ili kuwatoa Waisraeli katika nchi ya Misri, katika usiku huu Waisraeli wote wanapaswa kuadhimisha kwa kukesha ili kumheshimu Bwana katika vizazi vijavyo.

Masharti Kwa Ajili Ya Pasaka

4312:43 Hes 9:14; 15:14; 2Nya 6:32-33; Isa 14:1; 56:3-6; 60:10; Kut 12:11Bwana akamwambia Mose na Aroni, “Haya ndiyo masharti kwa ajili ya Pasaka:

“Mgeni hataruhusiwa kula Pasaka. 4412:44 Mwa 17:12-13Mtumwa yeyote ambaye mmemnunua aweza kuila kama mmemtahiri, 4512:45 Law 22:10lakini kibarua yeyote au msafiri haruhusiwi kula.

4612:46 Hes 9:12; Za 22:14; 34:20; Mit 17:22; Yn 19:36“Sharti iliwe ndani ya nyumba; msichukue nyama yoyote nje ya nyumba hiyo. Msiuvunje mfupa wowote. 47Jumuiya yote ya Israeli ni lazima waiadhimishe Pasaka hiyo.

4812:48 Law 19:18, 34; 24:22; Hes 9:14; 10:32; Eze 44:7“Mgeni aishiye miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka ya Bwana ni lazima wanaume wote waliomo nyumbani mwake wawe wametahiriwa, ndipo aweze kushiriki kama mzawa. Mwanaume yeyote asiyetahiriwa haruhusiwi kuila. 4912:49 Law 24:22; Hes 15:15-16, 29; Kum 1; 16Sheria iyo hiyo itamuhusu mzawa na mgeni anayeishi miongoni mwenu.”

50Waisraeli wote walifanya kama vile Bwana alivyomwagiza Mose na Aroni. 5112:51 Kut 3:10; 6:6, 26; 12:41Siku ile ile Bwana akawatoa Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.