传道书 6 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

传道书 6:1-12

1我看见日光之下有一件可悲的事,重重地压在人身上: 2上帝赐给人财富、产业和尊荣,叫他拥有所渴望的一切,却使他无法享用,倒让别人享用。这是虚空,是极大的悲哀。 3人若有一百个儿子,并且长寿,但心中却从未因福乐而满足,死后又不得安葬,我看这样的人还不如流产的胎儿。 4这胎儿在虚空中来,在黑暗中去,名字隐没在黑暗中, 5没有见过天日,一无所知,然而这胎儿比那人更享安息。 6就算那人活了千年,又活千年,却不能享受福乐,又如何呢?世人最终岂不都同归一处吗? 7人人为口腹劳碌,却永不满足。 8那么,智者比愚人有什么优势呢?贫穷人即使懂得如何处世,又有什么益处呢? 9满足于眼前所有的,胜过心中贪想的。这也是虚空,如同捕风。 10一切存在的事物都已命名,人的本质也被识透;人无法与比他更强的较量。 11其实话越多,越虚空,这对人又有什么益处? 12人生短暂虚空,如影飞逝,有谁知道什么对人有益?谁能告诉人死后日光之下会发生什么事?

Kiswahili Contemporary Version

Mhubiri 6:1-12

1Nimeona ubaya mwingine chini ya jua, nao unalemea sana wanadamu: 26:2 Kum 8:7-10; Za 17:14; Amu 18:10; Mhu 5:13-19Mungu humpa mwanadamu utajiri, mali na heshima, hivyo hakukosa chochote moyo wake unachokitamani. Lakini Mungu hamwezeshi kuvifurahia, badala yake mgeni ndiye anayevifurahia. Hili ni ubatili, ni ubaya unaosikitisha.

36:3 Ay 3:3, 16; Es 7:10; Mhu 4:3Mtu anaweza kuwa na watoto mia moja naye akaishi miaka mingi, lakini haidhuru kuwa ataishi muda mrefu kiasi gani, kama hawezi kufurahia mafanikio yake na kwamba hapati mazishi ya heshima, ninasema afadhali mtoto aliyezaliwa akiwa amekufa kuliko yeye. 4Kuzaliwa kwake hakuna maana, huondokea gizani na gizani jina lake hufunikwa. 5Ingawa hakuwahi kuliona jua wala kujua kitu chochote, yeye ana pumziko zaidi kuliko mtu huyo, 66:6 Mhu 2:16Hata kama huyo mtu ataishi miaka elfu mara mbili na zaidi, lakini akashindwa kufurahia mafanikio yake, je, wote hawaendi sehemu moja?

76:7 Mit 16:26; 27:20; 1Tim 6:6-8Juhudi zote za binadamu ni kwa ajili ya kinywa chake,

hata hivyo hamu yake kamwe haitoshelezwi.

86:8 Mhu 2:15Mtu mwenye hekima ana faida gani

zaidi ya mpumbavu?

Mtu maskini anapata faida gani

kwa kujua jinsi ya kujistahi

mbele ya watu wengine?

9Ni bora kile ambacho jicho linakiona

kuliko hamu isiyotoshelezwa.

Hili nalo ni ubatili,

ni kukimbiza upepo.

106:10 Ay 9:32; Isa 45:9; Mhu 3:15Lolote lililopo limekwisha kupewa jina,

naye mwanadamu alivyo ameshajulikana;

hakuna mtu awezaye kushindana

na mwenye nguvu kuliko yeye.

11Maneno yanavyokuwa mengi,

ndivyo yanavyokosa maana,

Je, hilo linamfaidia vipi yeyote?

126:12 Yak 4:14; Ay 10:20; 20:8; 14:2; 1Nya 29:15; Za 39:6Kwa maana ni nani anayejua lililo jema kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, katika siku chache na za ubatili anazopita kama kivuli? Ni nani awezaye kumwambia yatakayotokea chini ya jua baada ya yeye kuondoka?