传道书 4 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

传道书 4:1-16

1于是,我又观察日光之下的一切欺压之事。我看见受欺压的泪流满面,无人安慰。因为欺压者有权有势,所以无人安慰他们。 2因此,我认为那已死的人比活着的人幸福。 3不过,比以上两种人更幸运的是那从未出生的人,他们从未见过日光之下的恶行。 4我又看见人的一切劳碌和成就原是出于争强好胜。这也是虚空,如同捕风。 5愚人游手好闲,最后只能饿死。 6拥有不多,心里安宁,胜过拥有很多,仍劳碌捕风。 7我又看见日光之下一件虚空的事: 8有一个人孤孤单单,没有儿子也没有兄弟,却终身劳碌。他虽然家道丰裕,仍不满足,从未想过:“我不停地劳碌,放弃一切享受,究竟是为了谁?”这也是虚空,是一种悲哀。

9两个人总比一个人好,因为二人劳碌同得美好的成果。 10一人跌倒,总有同伴相扶。但孤身一人、跌倒了无人相扶的真悲惨! 11还有,二人同睡会暖和,一人独睡怎能暖和呢? 12遭遇攻击,一人独自不能抵挡,二人并肩就能对付。三股拧成的绳子不容易断。 13贫穷但有智慧的青年,胜过年老、愚昧、不再纳谏的君王。 14虽然这青年在本国出身贫寒,却能从囚犯成为君王。 15我看见所有日光之下的人都起来拥护这位代替老君王的青年。 16拥护他的人不计其数,以后的世代却对他不满。这也是虚空,如同捕风。

Kiswahili Contemporary Version

Mhubiri 4:1-16

Uonevu, Taabu, Uadui

14:1 Mao 1:16; Mhu 3:16; Za 12:5Nikatazama tena nikaona uonevu wote uliokuwa unafanyika chini ya jua:

Nikaona machozi ya walioonewa,

wala hawana wa kuwafariji;

uwezo ulikuwa upande wa wale wanaowaonea,

wala hawana wa kuwafariji.

24:2 Mhu 2:17; Yer 20:17-18; 22:10; Ay 3:17; 10Nami nikasema kwamba wafu,

waliokwisha kufa,

wana furaha kuliko watu walio hai,

ambao bado wanaishi.

34:3 Mhu 6:3; Mt 24:19; Ay 3:16-22Lakini aliye bora kuliko hao wawili

ni yule ambaye hajazaliwa bado,

ambaye hajaona ule uovu

unaofanyika chini ya jua.

4Tena nikaona kuwa kazi zote na mafanikio yote huchipuka kutokana na wivu wa mtu kwa jirani yake. Hili nalo ni ubatili, ni kukimbiza upepo.

54:5 Mit 6:10Mpumbavu hukunja mikono yake

na kujiangamiza mwenyewe.

64:6 Mit 15:16-17; 16:8Afadhali konzi moja pamoja

na utulivu kuliko konzi mbili pamoja na taabu

na kukimbiza upepo.

7Tena nikaona kitu kingine kilicho ubatili chini ya jua:

84:8 Mit 27:20; Hab 2:5-6; 1Yn 2:16Kulikuwepo mwanadamu aliye peke yake,

hakuwa na mwana wala ndugu.

Hapakuwa na mwisho wa kazi yake,

hata hivyo macho yake

hayakutosheka na utajiri wake.

Aliuliza, “Ninajitaabisha hivi kwa ajili ya nani,

nami kwa nini ninajinyima kufurahia?”

Hili pia ni ubatili,

ni shughuli yenye taabu!

9Wawili ni afadhali kuliko mmoja,

kwa sababu wana malipo mazuri kwa kazi yao:

10Kama mmoja akianguka,

mwenzake atamwinua.

Lakini ni jambo la kuhuzunisha

kwa mtu yule aangukaye

naye hana wa kumwinua!

11Pia, kama wawili wakilala pamoja

watapashana joto.

Lakini ni vipi mtu aweza

kujipasha joto mwenyewe?

12Ingawa mtu mmoja aweza kushindwa,

watu wawili wanaweza

kumkabili adui na kumshinda.

Kamba ya nyuzi tatu

haikatiki kwa urahisi.

Maendeleo Ni Ubatili

13Afadhali kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu ambaye hajui tena kupokea maonyo. 14Kijana huyo angeweza kutokea gerezani akapata ufalme, au angeweza kuwa amezaliwa katika umaskini kwenye huo ufalme. 15Nikaona kwamba wote walioishi na kutembea chini ya jua walimfuata kijana, aliyepokea ufalme. 16Hapakuwa na kikomo cha watu wote aliowatawala. Lakini wale waliokuja baadaye hawakufurahia kazi ya yule aliyepokea ufalme. Hili nalo pia ni ubatili, ni kukimbiza upepo.