以赛亚书 9 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

以赛亚书 9:1-21

未来的君王

1但那些受过痛苦的人必不再遇见黑暗。从前,耶和华使西布伦人和拿弗他利人住的地方受人藐视,日后必使这些地方,即约旦河对岸、沿海一带、外族人居住的加利利得到荣耀。

2走在黑暗中的人必看见大光,

活在死亡阴影下的人必被光照亮。

3耶和华啊,你必使以色列成为大国,

人民都喜气洋洋,

在你面前欢喜快乐,

好像丰收时那样欢喜,

如同瓜分战利品时那样快乐。

4因为你必折断他们负的轭和欺压者的棍棒,

好像昔日你毁灭米甸人一样;

5战士的靴子和染血的征袍都要被丢进火里烧掉。

6必有一个婴儿为我们诞生,

有一个孩子要赐给我们,

祂必统治我们。

祂被称为奇妙的策士、全能的上帝、永存的父、和平的君。

7祂的国必长治久安。

祂必坐在大卫的宝座上以公平和公义治国,

使国家永固。

万军之耶和华必热切地成就此事。

耶和华要审判以色列

8主已发言责备雅各家,

他的责备落在以色列

9住在以法莲撒玛利亚以色列人都知道。

他们骄傲自大地说:

10“砖墙倒塌了,

我们可以凿石重建;

桑树砍倒了,

我们可以再种香柏树。”

11因此耶和华必驱使敌人来攻击他们。

12东有亚兰人,西有非利士人,

他们必吞噬以色列

虽然如此,耶和华的怒气还没有止息,

祂的惩罚还没有停止。

13以色列人没有归向万军之耶和华,

也不寻求祂。

14因此,耶和华要在一日之间铲除以色列的头和尾。

15头是指他们的长老和首领,

尾是指教人虚谎之事的假先知。

16这些带领者使百姓步入歧途、

走向灭亡。

17他们目无上帝,

行事邪恶,口出狂言。

所以,主不喜欢他们的青年,

也不怜悯他们的孤儿寡妇。

虽然如此,耶和华的怒气还没有止息,

祂降罚的手没有收回。

18邪恶像燃烧的火焰,

焚毁荆棘和蒺藜,点燃密林,

烟柱旋转上腾。

19万军之耶和华的烈怒必如火一般烧焦大地,

人们成为烧火的柴,

甚至弟兄彼此相煎。

20他们到处抢夺食物,

仍饥饿难忍,

甚至吃自己的骨肉9:20 骨肉”或译“臂膀的肉”。

21以法莲玛拿西必自相残杀,

又联合起来攻打犹大

虽然如此,耶和华的怒气还没有止息,

祂降罚的手没有收回。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 9:1-21

Kwa Ajili Yetu Mtoto Amezaliwa

19:1 2Fal 15:29; 1Nya 5:26; Law 26:24; Ay 15:24Hata hivyo, hapatakuwepo huzuni tena kwa wale waliokuwa katika dhiki. Wakati uliopita aliidhili nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, lakini katika siku zijazo ataiheshimu Galilaya ya Mataifa, karibu na njia ya bahari, kando ya Yordani:

29:2 Mt 4:15-16; Eze 5:8; Mal 4:2; Yn 8:12; Za 82:5; 107:10-14; 36:9; Isa 8:20; Efe 5:8Watu wanaotembea katika giza

wameona nuru kuu,

wale wanaoishi katika nchi ya uvuli wa mauti,

nuru imewazukia.

39:3 Ay 12:23; Isa 25:9; Kut 15:9; Za 119:162; 4:7; Yos 22:8Umelikuza taifa,

na kuzidisha furaha yao,

wanafurahia mbele zako,

kama watu wanavyofurahia wakati wa mavuno,

kama watu wafurahivyo

wagawanyapo nyara.

49:4 Amu 7:22-25; Nah 1:13; Isa 10:26-27; Mt 11:30; Isa 60:18; Ay 34:24; Isa 37:36-38; 14:24; Yer 2:20; Za 81:6Kama vile siku ya kushindwa kwa Wamidiani,

umevunja nira iliyowalemea,

ile gongo mabegani mwao na

fimbo yake yeye aliyewaonea.

59:5 Isa 2:4Kila kiatu cha askari kilichotumiwa vitani,

na kila vazi lililovingirishwa katika damu

vitawekwa kwa ajili ya kuchomwa,

vitakuwa kuni za kuwasha moto.

69:6 Ebr 13:20; Mwa 3:15; Ay 15:8; Amu 13:18; Mt 28:18; Za 24:8; Lk 2:14; Mwa 3:15Kwa maana, kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,

tumepewa mtoto mwanaume,

nao utawala utakuwa mabegani mwake.

Naye ataitwa

Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,

Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.

79:7 Dan 2:44; Yn 12:34; Yer 23:5; 2Fal 19:31; Za 85:8; 1Kor 15:25; 2Sam 7:13Kuongezeka kwa utawala wake na amani

hakutakuwa na mwisho.

Atatawala katika kiti cha enzi cha Daudi

na juu ya ufalme wake,

akiuthibitisha na kuutegemeza

kwa haki na kwa adili,

tangu wakati huo na hata milele.

Wivu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote

utatimiza haya.

Hasira Ya Bwana Dhidi Ya Israeli

8Bwana ametuma ujumbe dhidi ya Yakobo,

utamwangukia Israeli.

99:9 Isa 7:9; Eze 2:4; Zek 7:11; Isa 2:4Watu wote watajua hili:

Efraimu na wakazi wa Samaria,

wanaosema kwa kiburi

na majivuno ya mioyo,

109:10 Mwa 11:3; Amo 7:14; Lk 19:14; 1Fal 7:2-3“Matofali yameanguka chini,

lakini tutajenga tena kwa mawe yaliyochongwa,

mitini imeangushwa,

lakini tutapanda mierezi badala yake.”

119:11 Isa 7:8Lakini Bwana amemtia nguvu adui wa Resini dhidi yao

na kuchochea watesi wao.

129:12 Za 79:7; Isa 5:25; 2Fal 16:6; Ay 40:11Waashuru kutoka upande wa mashariki

na Wafilisti kutoka upande wa magharibi

wameila Israeli kwa kinywa kilichopanuliwa.

Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,

mkono wake bado umeinuliwa juu.

139:13 Yer 5:3; Amo 4:6-10; Sef 1:16; 2Nya 28:22; Hag 2:17; Dan 9:13; Yer 50:4; Isa 17:7Lakini watu hawajamrudia yeye aliyewapiga,

wala hawajamtafuta Bwana Mwenye Nguvu Zote.

149:14 Isa 19:15; Ufu 18:8Kwa hiyo Bwana atakatilia mbali kutoka Israeli kichwa na mkia,

tawi la mtende na tete katika siku moja.

159:15 Isa 3:2-3; 5:13; 28:7; Ay 13:4; Eze 13:2, 22; Mt 24:24Wazee na watu mashuhuri ndio vichwa,

nao manabii wanaofundisha uongo ndio mkia.

169:16 Mt 15:14; 23:16, 24; Isa 3:12Wale wanaowaongoza watu hawa wanawapotosha,

nao wale wanaoongozwa wamepotoka.

179:17 Amo 8:13; Rum 3:13-14; Yer 13:14; Isa 32:6; Mik 7:2; Isa 5:25; Yer 9:21; 11:22; Isa 27:11; 5:25; Mt 12:34; Yer 48:15; 49:26Kwa hiyo Bwana hatawafurahia vijana,

wala hatawahurumia yatima na wajane,

kwa kuwa kila mmoja wao hamchi Mungu, nao ni waovu,

na kila kinywa kinanena upotovu.

Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,

mkono wake bado umeinuliwa juu.

189:18 Za 83:14; Kum 29:23; Isa 1:31; 5:6Hakika uovu huwaka kama moto;

huteketeza michongoma na miiba,

huwasha moto vichaka vya msituni,

hujiviringisha kuelekea juu kama nguzo ya moshi.

199:19 Mik 7:2-6; Isa 13:9-13; Ay 40:11; Za 97:3; Isa 1:31; Yer 17:27; Isa 3:5Kwa hasira ya Bwana Mwenye Nguvu Zote

nchi itachomwa kwa moto,

nao watu watakuwa kuni za kuchochea moto.

Hakuna mtu atakayemhurumia ndugu yake.

209:20 Law 26:26; Ay 18:12; Isa 49:26; Zek 11:9Upande wa kuume watakuwa wakitafuna,

lakini bado wataona njaa;

upande wa kushoto watakuwa wakila,

lakini hawatashiba.

Kila mmoja atajilisha kwa nyama ya mtoto wake mwenyewe:

219:21 Amu 7:22; 12:4; 2Nya 28:6; Isa 5:25Manase atamla Efraimu,

naye Efraimu atamla Manase;

nao pamoja watakuwa kinyume na Yuda.

Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,

mkono wake bado umeinuliwa juu.