以赛亚书 44 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以赛亚书 44:1-28

以色列蒙拣选

1“我的仆人雅各

我所拣选的以色列啊,

现在你要留心听。

2造你、使你在母胎中成形、

帮助你的耶和华说,

‘我的仆人雅各

我所拣选的耶书仑44:2 “耶书仑”是以色列的昵称。啊,

不要害怕。

3我要用水浇灌干渴之地,

使河流滋润干旱之土。

我要用我的灵浇灌你的后裔,

使我赐的福临到你的子孙。

4他们要滋长如青草,

又如溪旁杨柳。’

5这个说,‘我属于耶和华,’

那个说,‘我是雅各的子孙,’

还有人手上写着,‘耶和华之民,’

把自己归在以色列名下。

6“耶和华,以色列的君王和救赎主——

万军之耶和华说,

‘我是首先的,我是末后的,

除我以外再没有真神。

7谁能与我相比?让他公之于众。

让他细说自从我设立这古老民族以来的往事,

让他宣告未来将要发生的事。

8不要恐惧,不要害怕,

我不是从古时告诉过你们吗?

你们是我的证人。

除我以外还有真神吗?

没有,没有别的磐石,

一个也没有。’”

9制造偶像的真是无用,他们珍爱的偶像毫无价值。拜神像的人目盲眼瞎,愚昧无知,自找羞辱。 10制造神像、铸造无益偶像的是谁? 11看啊,拜偶像的人必羞愧,制造神像的工匠不过是人。让他们聚在一起来对质吧,他们必恐惧、羞愧。 12铁匠拿起工具在炭火上工作,用他强壮的臂膀挥动铁锤打造偶像。他饥饿时就会无力,口渴时就会疲乏。 13木匠拉线测量木料,用笔勾出轮廓,用圆规画出模样,用凿子雕成人的样子,形态逼真,放在庙宇里。 14他砍伐香柏木,或从林中选取柏木和橡木。他栽种松树,雨水使它长大。 15这树可以用来烧柴,他取一些木料生火取暖、烤饼,又制成神像来祭拜,雕成偶像来叩拜。 16他用一半木头生火烤肉,饱餐一顿,并用火取暖,说:“啊!我这里有火,真暖和。” 17他用另一半木头造了一个神明,作他的偶像,向它俯伏叩拜、祷告说:“你是我的神明,求你拯救我。” 18他们愚昧无知,因为他们的眼睛被封住以致看不见,他们的心窍被塞住以致不明白。 19他们无人思想,无人明白,无人醒悟说:“我用一半木头生火,在炭上烤饼烤肉吃,我岂能用另一半木头造可憎的神像?我岂能向一块木头叩拜?” 20他们以灰为食,心智迷糊,走入歧途,不能自救,也不会说:“我右手拿的神像岂不是假的吗?”

耶和华救赎以色列

21雅各啊,以色列啊,

要记住这些事,

因为你是我的仆人。

我造了你,你是我的仆人;

以色列啊,我必不忘记你。

22我除去了你的过犯和罪恶,

使它们如云雾消散。

归向我吧,因为我救赎了你。”

23诸天啊,歌唱吧!

因为耶和华成就了这事。

地的深处啊,欢呼吧!

众山岭和林中的树木啊,

你们都要歌唱!

因为耶和华救赎了雅各

以色列彰显了祂的荣耀。

24在母腹中造你、救赎你的耶和华说:

“我是创造万物的耶和华,

我独自铺展穹苍,开辟大地。

25我使假先知的预兆无法应验,

使占卜者丑态百出;

我颠覆智者的知识,

使之愚不可及。

26我使我仆人的话应验,

使我使者的计划成就。

我说耶路撒冷必有人居住,

我说犹大的城邑必重建起来,

从废墟中重建起来。

27我对深海说,‘枯干吧!

我要使你的河流干涸’;

28我说塞鲁士是我的牧人,

他必完成我的旨意,

他会下令重建耶路撒冷

降旨奠定圣殿的根基。

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 44:1-28

Israeli Aliyechaguliwa

144:1 Yer 30:10; Isa 41:8-10; Mwa 16:11; Isa 14:1“Lakini sasa sikiliza, ee Yakobo, mtumishi wangu,

Israeli, niliyemchagua.

244:2 Hes 23:21; Kum 32:15; Za 149:2; 139:13; Isa 41:10; Yer 30:10; 46:27Hili ndilo asemalo Bwana,

yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni,

yeye atakayekusaidia:

Usiogope, ee Yakobo, mtumishi wangu,

Yeshuruni,44:2 Yeshuruni hapa maana yake ni Yeye aliye mnyofu, yaani Israeli (ona pia Kum 32:15). niliyekuchagua.

344:3 Yn 4:10; Yoe 3:18; Isa 65:23; Yoe 2:28; Yn 7:37-39; Mit 9:5; Eze 36:27Kwa maana nitamimina maji juu ya nchi yenye kiu,

na vijito vya maji juu ya ardhi iliyokauka;

nitamimina Roho wangu juu ya watoto wako,

nayo baraka yangu juu ya wazao wako.

444:4 Law 23:40; Ay 40:22; 5:25; Za 72:16Nao watachipua kama manyasi katika shamba la majani,

kama mierezi kando ya vijito vya maji yatiririkayo.

544:5 Kut 13:9; Neh 9:38; Zek 13:9; 14:16; 8:20-22; Yer 50:5Mmoja atasema, ‘Mimi ni wa Bwana’;

mwingine atajiita kwa jina la Yakobo;

vilevile mwingine ataandika juu ya mkono wake, ‘Wa Bwana,’

na kujiita kwa jina la Israeli.

Ni Bwana, Siyo Sanamu

644:6 Ay 19:25; Isa 41:4; Ufu 22:13; Isa 43:10; 1Nya 17:20“Hili ndilo asemalo Bwana,

Mfalme wa Israeli na Mkombozi,

Bwana Mwenye Nguvu Zote:

Mimi ni wa kwanza na Mimi ni wa mwisho;

zaidi yangu hakuna Mungu.

744:7 Kum 32:39; Isa 41:22-26Ni nani basi aliye kama mimi? Yeye na atangaze.

Yeye atangaze na kuweka mbele yangu

ni kitu gani kilichotokea tangu nilipoumba watu wangu wa kale,

tena ni nini kitakachotokea:

naam, yeye na atoe unabii ni nini kitakachokuja.

844:8 Isa 43:10; Mwa 49:24; Kum 4:35; Isa 42:9Msitetemeke, msiogope.

Je, sikutangaza hili, na kutoa unabii tangu zamani?

Ninyi ni mashahidi wangu.

Je, yuko Mungu zaidi yangu mimi?

Hasha, hakuna Mwamba mwingine;

mimi simjui mwingine.”

944:9 Isa 41:24; Kum 4:28; Kut 20:4; Law 19:4; Isa 40:19; 1:29; Yer 22:22Wote wachongao sanamu ni ubatili,

navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu.

Wale ambao wanazitetea ni vipofu,

ni wajinga, nao waaibika.

1044:10 Yer 10:5; Mdo 19:24; Isa 41:29Ni nani atengenezaye mungu na kusubu sanamu,

ambayo haiwezi kumfaidia kitu chochote?

1144:11 2Fal 19:18; Isa 42:17; 37:19; 1:29Yeye pamoja na wenziwe wa aina yake wataaibishwa,

mafundi wao si kitu ila ni wanadamu tu.

Wote wakusanyike pamoja na kuwa na msimamo wao,

watashushwa chini kwa hofu na kwa fedheha.

1244:12 Isa 40:19; 54:16; Yer 10:3-5; Mdo 17:29; Isa 41:6-7; 40:28Muhunzi huchukua kifaa

na kukifanyia kazi kwenye makaa ya moto,

hutengeneza sanamu kwa nyundo,

huifanyiza kwa nguvu za mkono wake.

Huona njaa na kupoteza nguvu zake,

asipokunywa maji huzimia.

1344:13 Isa 41:7; Za 115:4-7; Amu 17:4-5Seremala hupima kwa kutumia kamba

na huuchora mstari kwa kalamu;

huchonga kwa patasi

na kutia alama kwa bikari.

Huifanyiza katika umbo la binadamu,

la mwanadamu katika utukufu wake wote,

ili iweze kukaa katika sehemu yake ya ibada ya miungu.

1444:14 Isa 41; 19Hukata miti ya mierezi,

huchukua mtiriza au mwaloni.

Huuacha ukue miongoni mwa miti ya msituni,

au hupanda msunobari, nayo mvua huufanya ukue.

1544:15 Ufu 9:20; 2Nya 25:14Ni kuni ya binadamu:

yeye huchukua baadhi yake na kuota moto,

huwasha moto na kuoka mkate.

Lakini pia huutumia kumtengeneza mungu na akamwabudu,

huitengeneza sanamu na kuisujudia.

1644:16 Isa 47:14Sehemu ya kuni huziweka motoni,

akapikia chakula chake,

hubanika nyama na kula hadi ashibe.

Huota moto na kusema,

“Aha! Ninahisi joto, ninaona moto.”

1744:17 1Fal 18:26; Amu 10:14; Isa 47:15; Kut 20:5; Isa 45:20; 46:7Mabaki yake hutengeneza mungu, sanamu yake;

yeye huisujudia na kuiabudu.

Huiomba na kusema,

“Niokoe; wewe ni mungu wangu.”

1844:18 Isa 16:12; Yer 4:22; Isa 29:10; Rum 11:8-10; Isa 6:9-10; Yer 10:8, 14-15Hawajui chochote, hawaelewi chochote,

macho yao yamefungwa hata hawawezi kuona,

akili zao zimefungwa hata hawawezi kufahamu.

1944:19 Isa 45:20; Kum 27:15; Isa 5:13; 27:11; 40:20Hakuna anayefikiri,

hakuna mwenye maarifa wala ufahamu wa kusema,

“Sehemu yake nilitumia kwa kuni;

hata pia nilioka mkate juu ya makaa yake,

nikabanika nyama na kuila.

Je, nifanye machukizo kwa kile kilichobaki?

Je, nisujudie gogo la mti?”

2044:20 Hos 4:12; Ay 15:31; 2Tim 3:13; Rum 1:25; Za 102; 9; 2The 2:11; Kum 4:28Hujilisha kwa majivu, moyo uliodanganyika humpotosha;

hawezi kujiokoa mwenyewe, au kusema,

“Je, kitu hiki kilichoko katika mkono wangu wa kuume si ni uongo?”

2144:21 Isa 46:8; Zek 10:9; Za 27:10; Yer 31:20; Isa 49:15; 27:11“Ee Yakobo, kumbuka mambo haya,

ee Israeli, kwa kuwa wewe ni mtumishi wangu.

Nimekuumba wewe, wewe ni mtumishi wangu.

Ee Israeli, sitakusahau.

2244:22 2Nya 6:21; Mdo 3:19; Mt 20:28; Mal 3:7; 2Sam 12:13; Ay 22:23; 1Kor 6:20Nimeyafuta makosa yako kama wingu,

dhambi zako kama ukungu wa asubuhi.

Nirudie mimi,

kwa kuwa nimekukomboa wewe.”

2344:23 Za 98:4; Isa 42:10; Za 98:8; Yer 30:19; Isa 12:6; 1Nya 16:31; Za 65:13; Kut 16:7Enyi mbingu, imbeni kwa furaha,

kwa maana Bwana amefanya jambo hili.

Ee vilindi vya dunia, piga kelele.

Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo,

enyi misitu na miti yenu yote,

kwa maana Bwana amemkomboa Yakobo,

ameuonyesha utukufu wake katika Israeli.

Yerusalemu Kukaliwa

2444:24 Ay 19:25; Isa 43:15; 42:5; Za 139:13“Hili ndilo asemalo Bwana,

Mkombozi wako, aliyekuumba tumboni:

“Mimi ni Bwana,

niliyeumba vitu vyote,

niliyezitanda mbingu peke yangu,

niliyeitandaza nchi mwenyewe,

2544:25 Law 19:26; Ay 5:13; 2Sam 15:31; 1Kor 1:19-20, 27; Za 33:10; 1Sam 6:2; Isa 47:13“mimi huzipinga ishara za manabii wa uongo,

na kuwatia upumbavu waaguzi,

niyapinduaye maarifa ya wenye hekima,

na kuyafanya kuwa upuzi,

2644:26 Zek 1:6; Isa 59:21; Mt 5:18; Ezr 9:9; Isa 46:10; Yer 23:20; 39:16niyathibitishaye maneno ya watumishi wake,

na kutimiza utabiri wa wajumbe wake,

“niambiaye Yerusalemu, ‘Itakaliwa na watu,’

niambiaye miji ya Yuda kuwa, ‘Itajengwa,’

na kuhusu magofu yake, ‘Mimi nitayatengeneza,’

2744:27 Isa 11:15; 19:5; Ufu 16:12niambiaye kilindi cha maji, ‘Kauka,

nami nitakausha vijito vyako,’

2844:28 2Nya 36:22-23; Ezr 1:2-4; Isa 14:32; 41:2; 28:16; 58:12nisemaye kuhusu Koreshi, ‘Yeye ni mchungaji wangu,

naye atatimiza yote yanipendezayo;

atauambia Yerusalemu, “Ukajengwe tena,”

na kuhusu Hekalu, “Misingi yake na iwekwe.” ’