以西结书 4 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以西结书 4:1-17

耶路撒冷被困的预兆

1“人子啊,你去拿一块砖放在自己面前,把耶路撒冷城画在上面。 2然后围困这城,建垒筑台,扎营围攻,四面架起撞城锤。 3拿一个铁盘当作铁墙放在你和城中间。你要面向这城,围困攻击这城。这是给以色列人的一个征兆。

4“你要向左侧卧,担当以色列人的罪恶。要用你向左侧卧的天数担当以色列人的罪恶。 5他们犯罪多少年,我要让你侧卧多少天。你要担当以色列人的罪恶三百九十天。 6然后,你再向右侧卧,担当犹大的罪恶四十天。你侧卧的天数代表他们犯罪的年数。 7你要面向被围困的耶路撒冷,光着臂膀说预言斥责这城。 8我要用绳索捆绑你,使你不能翻身,直到你围城的日子期满。

9“你要拿小麦、大麦、豆、扁豆、小米和粗麦,装在一个器皿中用来为自己做饼。你在三百九十天侧卧期间要吃这饼。 10你每天要按时按量吃二百克, 11每天要按时按量喝六百毫升水。 12你要像吃大麦饼一样吃这些饼,要在众人面前用人粪来烤饼。” 13耶和华说:“我把以色列人驱逐到各国的时候,他们也要这样在那里吃不洁净的食物。”

14我说:“唉,主耶和华啊!我从来没有玷污过自己,我自幼至今从未吃过自然死去的或被野兽撕碎的动物,不洁净的肉从未入过我的口。” 15于是祂对我说:“好吧,我容许你用牛粪代替人粪来烤饼。” 16祂又说:“人子啊,我要断绝耶路撒冷的粮源,叫他们怀着焦虑限量吃饼,怀着恐惧限量喝水。 17他们必缺粮少水,绝望地面面相觑,因自己的罪恶而灭亡。”

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 4:1-17

Kuzingirwa Kwa Yerusalemu Kwaonyeshwa Kwa Mfano

1“Mwanadamu, sasa chukua tofali, uliweke mbele yako na uchore juu yake ramani ya mji wa Yerusalemu. 24:2 Yer 6:6; Dan 11:15; Eze 21:22; Yer 33:4; Eze 17:17Kisha uuzingire: Simamisha askari dhidi yake kuuzunguka, uzunguke kwa majeshi, weka kambi dhidi yake pande zote pamoja na magogo ya kubomolea boma vitani. 34:3 Eze 20:3; Yer 13:1-7; 39:1; Isa 8:18; Law 2:5; Eze 20:46; 12:3-6Kisha chukua bamba la chuma, ukalisimamishe liwe kama ukuta wa chuma kati yako na huo mji, nawe uuelekeze uso wako. Huo mji utakuwa katika hali ya kuzingirwa, nawe utauzingira. Hii itakuwa ishara kwa nyumba ya Israeli.

4“Kisha ulale kwa upande wako wa kushoto na uweke dhambi za nyumba ya Israeli juu yake. Utazibeba dhambi zao kwa idadi ya siku utakazolala kwa huo upande mmoja. 54:5 Hes 14:34Nimekupangia idadi ya siku kama miaka ya dhambi yao. Kwa hiyo kwa siku 390 utabeba dhambi za nyumba ya Israeli.

64:6 Hes 14:34; Dan 12:11-12; 9:24-26; Kut 28:38“Baada ya kumaliza hili, lala chini tena, wakati huu ulale chini kwa upande wa kuume, uchukue dhambi za nyumba ya Yuda. Nimekupangia siku arobaini, siku moja kwa kila mwaka mmoja. 74:7 Eze 6:2; 13:17Geuza uso wako uelekeze kwenye kuzingirwa kwa Yerusalemu na mkono wako ambao haukuvikwa nguo tabiri dhidi yake. 84:8 Eze 3:25Nitakufunga kwa kamba ili usiweze kugeuka kutoka upande mmoja hadi upande mwingine, mpaka hapo utakapokuwa umetimiza siku za kuzingirwa kwako.

94:9 Isa 28:25“Chukua ngano na shayiri, maharagwe na dengu, mtama na mawele, uviweke na kuvihifadhi vyote kwenye gudulia la kuhifadhia, na uvitumie kujitengenezea mkate. Utaula mkate huo kwa hizo siku 390 utakazokuwa umelala kwa upande mmoja. 104:10 Kut 30:13Pima shekeli ishirini4:10 Shekeli 20 ni sawa na gramu 200. za chakula utakachokula kwa kila siku, nawe utakula kwa wakati uliopangwa. 114:11 Eze 4:16Pia pima maji moja ya sita ya hini,4:11 Moja ya sita ya hini ni sawa na mililita (ml) 600. nawe utakunywa kwa wakati uliopangwa. 124:12 Isa 36:12Nawe utakula chakula kama vile ambavyo ungekula mkate wa shayiri, uoke mkate mbele ya macho ya watu, ukitumia kinyesi cha mwanadamu.” 134:13 Hos 9:3; Amo 7:17Bwana akasema, “Hivi ndivyo watu wa Israeli watakavyokula chakula kilicho najisi miongoni mwa mataifa ninakowapeleka.”

144:14 Eze 20:49; Law 11:39; Dan 1:8; Mdo 10:14; Kum 14:3; Hos 9:3-4; Eze 20:49Ndipo nikasema, “Sivyo Bwana Mwenyezi! Kamwe mimi sijajitia unajisi. Tangu ujana wangu hadi sasa sijala kamwe kitu chochote kilichokufa au kilichoraruliwa na wanyama wa mwituni. Hakuna nyama yeyote najisi iliyoingia kinywani mwangu.”

15Akasema, “Vema sana, basi nitakuruhusu uoke mkate wako kwa kutumia kinyesi cha ngʼombe badala ya kinyesi cha mwanadamu.”

164:16 Za 105:16; Eze 5:16; Law 26:26; Isa 3:1; Eze 12:19Ndipo Mungu akaniambia, “Mwanadamu, mimi nitakatilia mbali upatikanaji wa chakula katika Yerusalemu. Watu watakula chakula cha kupimwa kwa wasiwasi pamoja na maji ya kupimiwa kwa kukata tamaa, 174:17 Law 26:39; Eze 33:10; 24:23; 5:16; 12:18-19; Amo 4:8kwa kuwa chakula na maji vitakuwa adimu. Watastajabiana kila mmoja, nao watadhoofika kwa sababu ya dhambi yao.