以西结书 30 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

以西结书 30:1-26

为埃及唱哀歌

1耶和华对我说: 2“人子啊,你要说预言,这样宣告主耶和华的话,

“‘哀号吧!你们要为那日悲伤。

3因为日子近了,耶和华的日子近了,

那是乌云密布的日子,

列国沦亡的时候。

4必有刀剑攻击埃及

埃及必尸横遍野,

古实必痛苦不堪。

敌人要掳掠埃及的财富,

摧毁她的根基。

5古实路德阿拉伯利比亚以及她的其他盟友都必与她一同死于刀下。’

6“耶和华说,

埃及的盟友都要覆灭,

埃及的傲气必荡然无存,

密夺色弗尼的居民都要丧身刀下。

这是主耶和华说的。

7埃及要变成荒地中的荒地,

她的城邑要沦为废墟中的废墟。

8我要点火烧埃及

埃及的所有盟友都要灭亡。

那时,他们就知道我是耶和华。

9“‘在那日,我要差遣使者乘船出去惊吓安逸的古实人,在埃及遭难的日子,他们必痛苦不堪。看啊,这日子快到了。’

10“主耶和华说,

“‘我要借巴比伦尼布甲尼撒的手消灭埃及的百姓。

11他和追随他的都是万民中最残暴的人。

我要差他们去毁灭埃及

大肆杀戮,

使埃及尸骨遍野。

12我要使尼罗河干涸,

把土地卖给恶人,

我要借外族人的手使地和地上的一切都荒废,

这是我耶和华说的。’

13“主耶和华说,

‘我要毁灭偶像,

铲除挪弗的神像。

埃及再没有君王,

国内到处充满恐惧。

14我要使巴特罗荒废,

放火焚烧琐安

审判底比斯

15把我的烈怒倾倒在埃及的堡垒——

消灭底比斯的百姓。

16我要放火烧埃及

要受痛苦的折磨,

底比斯要被攻破,

挪弗终日惶恐不已,

17亚文比伯实的壮丁必死于刀下,

众城都要遭受掳掠。

18我粉碎埃及势力的那天,

答比匿日月无光,

她的锐气全消。

乌云要笼罩她,

她城邑的居民要被掳去。

19我必这样审判埃及

他们就知道我是耶和华。’”

20第十一年一月七日,耶和华对我说: 21“人子啊,我打断了埃及王法老的臂膀,没有人替他敷药包扎,以致他无力拿刀。 22主耶和华说,‘我要与埃及王法老为敌,我要把他那强壮的臂膀和曾经受伤的臂膀一起打断,使刀从他手中掉落。 23我要把埃及人驱散到列国,分散到列邦。 24我要使巴比伦王的臂膀强壮有力,把我的刀交在他手中。我要打断法老的臂膀,使法老在他面前像受了致命伤的人一样呻吟。 25我要使巴比伦王的臂膀强壮有力,而法老的双臂必软弱无力。我要把我的刀交在巴比伦王手中,让他挥刀攻击埃及。那时他们就知道我是耶和华。 26我要把埃及人驱散到列国,分散到列邦,这样他们就知道我是耶和华。’”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 30:1-26

Maombolezo Kwa Ajili Ya Misri

1Neno la Bwana likanijia kusema: 230:2 Isa 13:6; Yak 5:1“Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Ombolezeni ninyi na mseme,

“Ole wa siku ile!”

330:3 Oba 1:15; Yoe 2:11; Eze 32:7; 34:12; 7:7; Yoe 1:15Kwa kuwa siku ile imekaribia,

siku ya Bwana imekaribia,

siku ya mawingu,

siku ya maangamizi kwa mataifa.

430:4 Eze 29:19; Yer 50:15; 25:19; Dan 11:43; Mwa 10:6; Eze 29:10Upanga utakuja dhidi ya Misri,

nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia.

Mauaji yatakapoangukia Misri,

utajiri wake utachukuliwa

na misingi yake itabomolewa.

530:5 Eze 27:10; Yer 25:20; 2Nya 9:14; Nah 3:9Kushi30:5 Kushi ndiyo Ethiopia. na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya30:5 Libya ndiyo Kubu. na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri.

630:6 Eze 29:10“ ‘Hili ndilo Bwana asemalo:

“ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka

na kiburi cha nguvu zake kitashindwa.

Kutoka Migdoli hadi Aswani,

watauawa ndani yake kwa upanga,

asema Bwana Mwenyezi.

730:7 Eze 29:12“ ‘Hizo nchi zitakua ukiwa

miongoni mwa nchi zilizo ukiwa,

nayo miji yao itakuwa magofu

miongoni mwa miji iliyo magofu.

830:8 Yer 49:27; Eze 39:6; Nah 1:6; Eze 29:9Ndipo watakapojua kwamba mimi ndimi Bwana,

nitakapoiwasha Misri moto

na wote wamsaidiao watapondwa.

930:9 Kum 31:6; Mt 10:28; Eze 24:3; 44:630:9 Mwa 10:6; Isa 18:1-2; 23:5; Eze 32:9-10; Sef 2:12“ ‘Siku hiyo wajumbe watatoka kwangu kwa merikebu, ili kuwatia hofu Ethiopia, wakiwa katika hali yao ya kuridhika. Maumivu makali yatawapata siku ya maangamizi ya Misri, kwa kuwa hakika itakuja.

1030:10 Yer 39:1; Eze 29:19“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Nitakomesha makundi ya wajeuri ya Misri

kwa mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli.

1130:11 Eze 28:7; 29:19Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote,

litaletwa ili kuangamiza nchi.

Watafuta panga zao dhidi ya Misri

na kuijaza nchi kwa waliouawa.

1230:12 Isa 19:6; Yer 46:8; Eze 29:9; 19:7Nitakausha vijito vya Naili

na nitaiuza nchi kwa watu waovu,

kwa mkono wa wageni,

nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu

kilichomo ndani yake.

Mimi Bwana nimenena haya.

1330:13 Yer 43:12; Isa 19:13; Eze 6:6; Zek 10:11“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Nitaangamiza sanamu

na kukomesha vinyago katika Memfisi30:13 Kiebrania ni Nofu.

Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri,

nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.

1430:14 Eze 29:14; Hes 13:22; Za 78:12; Yer 46:25Nitaifanya Pathrosi30:14 Pathrosi ni Misri ya Juu. kuwa ukiwa

na kuitia moto Soani,

nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi30:14 Thebesi kwa Kiebrania ni No (au No-Amoni), mji katika Misri.

15Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,30:15 Kiebrania ni Sini.

ngome ya Misri,

nami nitakatilia mbali

makundi ya wajeuri wa Thebesi.

1630:16 Yos 7:15; Isa 19:13Nitaitia moto nchi ya Misri;

Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu.

Thebesi itachukuliwa na tufani,

Memfisi itakuwa katika taabu daima.

1730:17 Mwa 41:45Wanaume vijana wa Oni30:17 Yaani Heliopoli (Mji wa Jua). na wa Pi-Besethi30:17 Yaani Bubasti.

wataanguka kwa upanga

nayo hiyo miji itatekwa.

1830:18 Law 26:13; Isa 9:4; Yer 2:16; 43:7Huko Tahpanhesi mchana utatiwa giza

nitakapovunja kongwa la Misri;

hapo kiburi cha nguvu zake kitakoma.

Atafunikwa na mawingu

na vijiji vyake vitatekwa.

1930:19 Eze 28:22Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu,

nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”

2030:20 Eze 26:1; 29:17; 32:1Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa kwanza, siku ya saba, neno la Bwana likanijia kusema: 2130:21 Yer 48:25; 44:30; 30:13; 46:11“Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga. 2230:22 Mwa 15:18; Yer 46:25; Za 37:17; Zek 11:17Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na Farao mfalme wa Misri. Nitavunja mikono yake yote miwili, ule mkono ulio mzima pia na ule uliovunjika na kuufanya upanga uanguke toka mkononi mwake. 2330:23 Eze 29:12Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi zote. 2430:24 Zek 10:6-12; 12:5; Eze 21:14; Sef 2:12; Yer 51:52Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli na kuutia upanga wangu mkononi mwake, lakini nitavunja mikono ya Farao, naye atalia kwa huzuni mbele yake kama mtu aliyetiwa jeraha la kumfisha. 2530:25 Kut 7:5; Za 9:16; 59:13; 1Nya 21:12; Isa 10:5; Eze 29:19Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, lakini mikono ya Farao italegea. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana, nitakapoutia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye ataunyoosha dhidi ya Misri. 2630:26 Eze 29:12Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi mbalimbali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.”