以西结书 18 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以西结书 18:1-32

犯罪者必灭亡

1耶和华对我说: 2“你们谈论以色列地时为什么说‘父亲吃了酸葡萄,儿子的牙酸倒了’这句俗语呢? 3主耶和华说,我凭我的永恒起誓,你们在以色列必不再用这句俗语。 4因为所有的生命都属于我,父和子都属于我。谁犯罪,谁死亡。

5“倘若有义人秉公行义, 6不在山上的庙宇里吃祭物,不拜以色列人的偶像,不玷污别人的妻子,不亲近经期中的妇女; 7不欺压人,反而退还债户的抵押品;不抢夺财物,反而给饥饿的人食物吃,给赤身露体的人衣服穿; 8不放债取利,不犯罪作恶,反而公平待人, 9遵守我的律例,切实遵行我的典章——这样的人是义人,必能活着。这是主耶和华说的。

10“倘若这人生的儿子凶残暴戾,嗜杀成性,无恶不作, 11常在山上的庙宇吃祭偶像之物,玷污别人的妻子, 12欺压贫穷困苦的人,抢夺财物,扣留债户的抵押品,祭拜偶像,行可憎之事, 13放债取利,这样的人还能活着吗?他必不能活。他多行可憎之事,必自取灭亡,自害己命。

14“倘若这不肖子有一个好儿子,他看见父亲的所作所为,不愿步父亲的后尘。 15他不在山上吃祭偶像之物,不拜以色列人的偶像,不玷污别人的妻子, 16不欺压他人,不扣留抵押品,不抢夺财物,反而给饥饿的人食物吃,给赤身露体的人衣服穿, 17不压榨贫穷的人,不放债取利,反而遵守我的典章,顺从我的律例,这人必不因父亲的罪恶而死亡,他必活着。 18他父亲因肆意欺诈,掠夺同胞,多行不义,必死于自己的罪恶。

19“你们会问,‘儿子为什么不用承担父亲的罪恶呢?’这是因为儿子秉公行义,谨遵我的律例,所以他必活着。 20谁犯罪,谁死亡,儿子不用承担父亲的罪恶,父亲也不用承担儿子的罪恶。义人的义必归自己,恶人的恶也必归自己。

21“恶人若肯改邪归正,遵守我的律例,秉公行义,就必活着,不致死亡。 22他犯的一切罪过不会被追究,他必因行事正直而活着。 23主耶和华说,我难道喜欢恶人死亡吗?我岂不是更愿他们改邪归正并活着吗? 24义人若弃善行恶,与恶人同流合污,这人岂能活着?他从前的义行不会被记念,他必因自己的背信和罪恶而死亡。

25“你们说,‘主行事不公平。’以色列人啊,你们听着,是我行事不公平呢?还是你们行事不公平呢? 26义人若离义行恶,必因恶行而死。 27恶人若改邪归正、秉公行义,必保全性命。 28因为他醒悟过来,改邪归正,必能活着,不致死亡。 29以色列人却说,‘主行事不公平!’以色列人啊,是我行事不公平呢?还是你们行事不公平呢?

30“所以主耶和华说,‘以色列人啊,我必按你们各人的行为审判你们。你们要悔改,改邪归正,免得死在罪中。 31你们要离弃从前所有的罪恶,洗心革面。以色列人啊!你们何必走向灭亡呢?’ 32主耶和华说,‘我断不喜欢任何人死亡,你们要悔改,便得存活。’”

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 18:1-32

Roho Itendayo Dhambi Itakufa

1Neno la Bwana likanijia kusema: 218:2 Isa 3:15; Mao 5:7; Ay 21:19; Yer 31:29“Je, ninyi watu mna maana gani kutumia mithali hii inayohusu nchi ya Israeli:

“ ‘Baba wamekula zabibu zenye chachu,

nayo meno ya watoto yametiwa ganzi’?

318:3 Za 49:4“Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hamtatumia tena mithali hii katika Israeli. 418:4 Mwa 18:32; Rum 6:23; Ebr 12:9; 2Fal 14:6; Mit 13:21; Kut 17:14; Ay 21:20; Isa 42:5; Eze 33:8Kwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa.

5“Mtu aweza kuwa ni mwenye haki

atendaye yaliyo haki na sawa.

618:6 Eze 6:2; 22:9; Kum 4:19; Amo 5:26; Ebr 13:4; Eze 6:13; Law 15:24Hakula katika mahali pa ibada za miungu

kwenye milima

wala hakuziinulia macho sanamu

za nyumba ya Israeli.

Hakumtia unajisi mke wa jirani yake,

wala hakukutana kimwili na mwanamke

wakati wa siku zake za hedhi.

718:7 Yak 5:4; Kut 22:26; Kum 24:12; 24:12; 15:11; Lk 3:11; Kut 20:15; Ay 22:7Hamwonei mtu yeyote,

bali hurudisha kilichowekwa rehani kwake.

Hanyangʼanyi, bali huwapa wenye njaa chakula chake

na huwapa nguo walio uchi.

818:8 Zek 8:16; Kut 18:21; Kum 23:19-20; Yer 22:3; Kut 22:25; Law 25:35-37Hakopeshi kwa riba

wala hajipatii faida ya ziada.

Huuzuia mkono wake usifanye mabaya,

naye huhukumu kwa haki kati ya mtu na mtu.

918:9 Hab 2:4; Law 18:5; Amo 5:4; Law 19:37; Eze 11:12; 20:11Huzifuata amri zangu

na kuzishika sheria zangu kwa uaminifu.

Huyo mtu ni mwenye haki;

hakika ataishi,

asema Bwana Mwenyezi.

1018:10 Kut 21:12; Eze 22:6“Aweza kuwa ana mwana jeuri, amwagaye damu au atendaye mojawapo ya mambo haya 1118:11 Kut 22:22; Ay 24:9; Isa 54:9; 59:6-7; Hab 2:6; Kut 22:17; Eze 16:49(ingawa baba yake hakufanya mojawapo ya haya):

“Hula katika mahali pa ibada za miungu kwenye milima.

Humtia unajisi mke wa jirani yake.

1218:12 Kut 22:22; 22:27; Ay 24:9; Amo 4:1; 2Fal 21:11Huwaonea maskini na wahitaji.

Hunyangʼanyana.

Harudishi kile kilichowekwa rehani kwake.

Huziinulia sanamu macho.

Hufanya mambo ya machukizo.

1318:13 Kut 22:25; Law 20:9; Hos 12:14; Eze 33:4-5Hukopesha kwa riba na kutafuta faida ya ziada.

Je, mtu wa namna hii ataishi? Hapana, hataishi! Kwa sababu amefanya mambo haya yote ya machukizo, hakika atauawa na damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.

1418:14 2Nya 34:21; Mit 23:24“Lakini yawezekana mwana huyo ana mwana aonaye dhambi hizi zote anazofanya baba yake, naye ingawa anaziona, yeye hafanyi mabaya kama haya:

1518:15 Eze 22:9; Za 24:4“Hakula katika mahali pa ibada za miungu

kwenye milima,

wala hainulii macho sanamu

za nyumba ya Israeli.

Hakumtia unajisi

mke wa jirani yake.

1618:16 Kut 22:27; Ay 22:7; Mit 22:9; Za 41:1; Eze 16:49; Isa 7:10Hakumwonea mtu yeyote

wala hakutaka rehani kwa ajili ya mkopo.

Hanyangʼanyi,

bali huwapa wenye njaa chakula chake

na huwapa nguo walio uchi.

1718:17 Za 1:2Huuzuia mkono wake usitende dhambi,

hakopeshi kwa riba

wala hajipatii faida ya ziada.

Huzishika amri zangu

na kuzifuata sheria zangu.

Hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake; hakika ataishi. 1818:18 Eze 3:18Lakini baba yake atakufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe, kwa sababu alitoza bei isiyo halali kwa nguvu, akamnyangʼanya ndugu yake na kufanya yaliyo mabaya miongoni mwa watu wake.

1918:19 Kut 20:5; Kum 5:9; Yer 15:4; Zek 1:3-6“Lakini mnauliza, ‘Kwa nini mwana asiadhibiwe kwa uovu wa baba yake?’ Kwa vile mwana ametenda yaliyo haki na sawa na amekuwa mwangalifu kuzishika amri zangu zote, hakika ataishi. 2018:20 Kum 24:16; Rum 2:9; Isa 3:10; Hes 15:31; 1Fal 8:32; 2Fal 14:6; Eze 7:27; Mt 16:27Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. Mwana hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya baba yake, wala baba hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya mwanawe. Haki ya mtu mwenye haki itahesabiwa juu yake na uovu wa mtu mwovu utalipizwa juu yake.

2118:21 Eze 13:22; 33:12-19; Yer 18:8; Mwa 26:5“Lakini mtu mwovu akiacha dhambi zake zote alizozitenda na kushika amri zangu zote na kufanya lililo haki na sawa, hakika ataishi, hatakufa. 2218:22 Dan 4:27; Mik 7:19; Mit 18:20-24; Isa 43:25Hakuna kosa lolote alilotenda litakalokumbukwa juu yake. Kwa ajili ya mambo ya haki aliyoyatenda, ataishi. 2318:23 Mao 3:33; 2Pet 3:9; 1Tim 2:4; Za 147:11; Ay 37:23; Eze 16:6; Mik 7:18Je, mimi ninafurahia kifo cha mtu mwovu? Asema Bwana Mwenyezi. Je, si mimi ninafurahi wanapogeuka kutoka njia zao mbaya na kuishi?

2418:24 Ay 35:8; 2Pet 2:20-22; Ebr 10:38; Yer 34:6; Eze 15:8; 1Sam 15:11; 2Nya 24:17-20“Lakini kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi na kufanya mambo ya machukizo ambayo mtu mwovu hufanya, Je, ataishi? Hakuna hata mojawapo ya matendo ya haki aliyotenda litakalokumbukwa. Kwa sababu ya kukosa uaminifu kwake anayo hatia na kwa sababu ya dhambi alizozitenda, atakufa.

2518:25 Sef 3:5; Mal 3:1-17; Mwa 18:25; Yer 2:29; Eze 33:17; Mal 2:17“Lakini mnasema, ‘Njia ya Bwana si ya haki.’ Sikia, ee nyumba ya Israeli: Njia yangu siyo iliyo ya haki? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki? 2618:26 Eze 18:24Kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi, atakufa kwa ajili ya dhambi yake, kwa sababu ya dhambi alizotenda, atakufa. 2718:27 Isa 1:18; Eze 13:22Lakini mtu mwovu akigeuka kutoka maovu aliyoyatenda na kufanya yaliyo haki na sawa, ataokoa maisha yake. 2818:28 Eze 18:14; Isa 55:7Kwa kuwa anayafikiria na kugeuka kutoka makosa yake yote aliyoyatenda na kuyaacha, hakika ataishi, hatakufa. 29Lakini nyumba ya Israeli inasema, ‘Njia za Bwana si haki.’ Je, njia zangu si za haki, ee nyumba ya Israeli? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki?”

3018:30 Yer 35:15; Eze 7:13; Mt 3:2; Hos 12:6; 1Pet 1:17; Isa 27“Kwa hiyo, ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu, kila mmoja sawasawa na njia zake, asema Bwana Mwenyezi. Tubuni! Geukeni kutoka makosa yenu yote, ndipo dhambi haitakuwa anguko lenu. 3118:31 Za 51:10; Isa 1:16-17; Eze 36:26; Efe 4:22; Amu 6:8; Yer 27:13; Eze 11:19Tupilieni mbali makosa yenu yote mliyoyatenda, nanyi mpate moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, ee nyumba ya Israeli? 3218:32 2Nya 7:14; Ay 37:23; Eze 33:11; Ay 22:23; Isa 55:7; Mal 3:7; Eze 16:6Kwa maana sifurahii kifo cha mtu awaye yote afaye katika uovu, asema Bwana Mwenyezi. Tubuni basi, mkaishi!