以西结书 10 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以西结书 10:1-22

耶和华的荣耀离开圣殿

1我观看,只见基路伯天使头顶上的穹苍之中好像有一个蓝宝石宝座。 2耶和华对那穿细麻衣的人说:“你到基路伯天使下边旋转的轮子中间,双手捧满火炭,撒在城上。”我见他进去了。

3当他进去的时候,基路伯天使站在殿的南边,内院充满了云彩。 4耶和华的荣耀从基路伯天使的上面升起,停在殿的门口,殿里充满了云彩,院子也充满了耶和华荣耀的光辉。 5基路伯天使展翅的响声好像全能上帝说话的声音,在外院也可以听见。

6祂对那穿细麻衣的人说:“你要从基路伯天使下面旋转的轮子中取火。”那人便进去,站在一个轮子旁边。 7有一个基路伯天使伸手到他们中间的火里,取了些火放在那穿细麻衣的人手里,那人就拿了出去。 8基路伯天使的翅膀下仿佛有人的手。

9我又看见四个基路伯天使旁各有一个闪耀如绿宝石的轮子。 10四个轮子结构一样,好像轮套轮。 11基路伯天使移动时,不必转身就可以向四方移动。前轮朝哪个方向移动,其他轮子也朝哪个方向移动,不必转向。 12这四个基路伯天使的手、背、翅膀及全身都布满了眼睛,包括他们的四个轮子。 13我听见他们称这些轮子为“旋转轮”。 14每一个基路伯天使都有四张脸:第一张是基路伯天使的脸,第二张是人的脸,第三张是狮子的脸,第四张是鹰的脸。

15然后,这些基路伯天使都向上升去,他们就是我在迦巴鲁河边所见的活物。 16基路伯天使移动,轮子也随之移动;基路伯天使展翅飞离地面,轮子也随之离开地面,不离他们旁边; 17基路伯天使停住,轮子也随之停住;基路伯天使上升,轮子也随之上升。因为活物的灵在轮子中。

18那时,耶和华的荣耀离开了殿的门口,停在基路伯天使上面。 19我正观看时,基路伯天使展翅飞离地面,他们旁边的轮子也随之飞离。他们停在耶和华殿的东门口,以色列上帝的荣耀在他们上面。 20这些是我在迦巴鲁河边所看见的活物,他们在以色列上帝的下面。我知道他们是基路伯天使。 21他们各有四张脸,两对翅膀,翅膀下仿佛有人的手, 22他们的面貌和我在迦巴鲁河边所见的一样,每一个都向前直走。

Kiswahili Contemporary Version

Ezekieli 10:1-22

Utukufu Unaondoka Hekaluni

110:1 Kut 23:10; Eze 1:22; Ufu 4:2-3; Mwa 3:24Nikatazama, nikaona juu ya ile nafasi iliyokuwa juu ya vichwa vya wale makerubi kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha enzi cha yakuti samawi. 210:2 Eze 1:15; 9:2; Ufu 8:5; 2Sam 22:9Bwana akamwambia mtu yule aliyekuwa amevaa nguo ya kitani, “Ingia katikati ya yale Magurudumu yaliyo chini ya makerubi. Ukaijaze mikono yako makaa ya mawe ya moto kutoka katikati ya makerubi na uyatawanye juu ya mji.” Nilipokuwa nikiangalia, akaingia ndani.

3Basi wale makerubi walikuwa wamesimama upande wa kusini wa Hekalu wakati yule mtu alipoingia ndani, wingu likaujaza ule ukumbi wa ndani. 410:4 Kut 24:16; Eze 44:4; 1:28Kisha utukufu wa Bwana ukainuka kutoka juu ya wale makerubi ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Wingu likajaza Hekalu, nao ukumbi ukajawa na mngʼao wa utukufu wa Bwana. 510:5 Ay 40:9; Eze 1:24; 3:15Sauti ya mabawa ya wale makerubi ingeweza kusikika mpaka kwenye ukumbi wa nje, kama sauti ya Mungu Mwenyezi10:5 Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote). wakati anapoongea.

610:6 Dan 7:9Bwana alipomwamuru yule mtu aliyevaa nguo za kitani akisema, “Chukua moto toka katikati ya magurudumu, kutoka katikati ya makerubi,” yule mtu aliingia ndani akasimama pembeni mwa gurudumu. 710:7 Eze 5:4Ndipo mmoja wa wale makerubi akanyoosha mkono wake kwenye moto uliokuwa katikati yao. Akachukua baadhi ya moto na kuutia mikononi mwa yule mtu aliyevaa mavazi ya kitani, naye akaupokea akatoka nje. 810:8 Eze 1:8(Chini ya mabawa ya makerubi paliweza kuonekana kitu kilichofanana na mikono ya mwanadamu.)

910:9 Kut 28:20; Eze 1:15-21; 24:6Nikatazama, nikaona magurudumu manne kando ya makerubi, moja kando ya kila kerubi. Magurudumu hayo yalimetameta kama kito cha zabarajadi. 10Kule kuonekana kwake, yote manne yalifanana kila gurudumu lilikuwa kama linazunguka ndani ya lingine. 1110:11 Eze 1:17Yalipozunguka, yalikwenda kokote katika pande nne walikoelekea wale makerubi. Magurudumu hayakugeuka wakati makerubi yalipokwenda. Makerubi walikwenda upande wowote kichwa kilikoelekea pasipo kugeuka walipokuwa wakienda. 1210:12 Ufu 4:6-8; Eze 1:15-21; 24:6Miili yao yote, pamoja na migongo yao, mikono na mabawa yao yote yalikuwa yamejaa macho kabisa kama yalivyokuwa yale magurudumu yao manne. 13Nikasikia magurudumu yakiitwa, “Magurudumu ya kisulisuli.” 1410:14 1Fal 7:36; Eze 41:19; Dan 9:21; Ufu 4:7Kila mmoja wa wale makerubi alikuwa na nyuso nne: Uso mmoja ulikuwa kama vile wa kerubi, uso wa pili ulikuwa wa mwanadamu, uso wa tatu ulikuwa wa simba na uso wa nne ulikuwa wa tai.

1510:15 Isa 6:2; Eze 1:3-5; Za 137:1Kisha makerubi wakapaa juu. Hawa ndio wale viumbe walio hai niliowaona kando ya Mto Kebari. 1610:16 Eze 1:19Wakati makerubi walipokwenda, magurudumu yaliyoko kando yao yalikwenda na wakati makerubi walipotanda mabawa yao wapate kupaa juu kutoka ardhi, magurudumu yale hayakuondoka pembeni mwao. 1710:17 Eze 1:20-21; 3:13Makerubi yaliposimama kimya, nayo pia yalitulia kimya, nao makerubi yalipoinuka juu, magurudumu nayo yaliinuka juu pamoja nao, kwa sababu roho ya vile viumbe hai ilikuwa ndani yake.

1810:18 Za 78:60; 18:10; Eze 7:20-22; 1Sam 4:21Kisha utukufu wa Bwana ukaondoka pale kwenye kizingiti cha Hekalu na kusimama juu ya wale makerubi. 1910:19 Eze 11:1-22; 43:4Nilipokuwa nikitazama, makerubi yakatanda mabawa yao na kuinuka kutoka ardhini, nao walipokuwa wakienda, yale magurudumu yakaenda pamoja nao. Wakasimama kwenye ingilio la lango la mashariki la nyumba ya Bwana, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ukawa juu yao.

2010:20 Eze 1:1-8Hawa walikuwa ndio viumbe hai niliokuwa nimewaona chini ya Mungu wa Israeli kando ya Mto Kebari, nami nikatambua ya kuwa hao walikuwa makerubi. 2110:21 Eze 1:6, 8Kila mmoja alikuwa na nyuso nne, mabawa manne, chini ya mabawa yao kulikuwa na kile kilichoonekana kama mikono ya mwanadamu. 2210:22 Eze 1:10, 12Nyuso zao zilifanana kama zile nilizokuwa nimeziona kando ya Mto Kebari. Kila mmoja alikwenda mbele moja kwa moja.