以斯帖记 9 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以斯帖记 9:1-32

犹太人的反击

1十二月,即亚达月十三日,是执行王谕旨的日子。那天,犹太人的仇敌原本想辖制他们,却反而被他们辖制。 2犹太人在亚哈随鲁王的各省各城聚集起来,攻击那些要害他们的人,无人能抵挡他们,因为各族都惧怕他们。 3各省的官员、总督、省长和为王办事的人因惧怕末底改,就都帮助犹太人。 4因为末底改已是王宫要员,他的名声传遍各省,权势日盛。 5犹太人用刀击杀所有敌人,任意消灭恨他们的人。 6犹太人单在书珊城就杀了五百人。 7他们还杀了巴珊大他达分亚斯帕他8坡拉他亚大利雅亚利大他9帕玛斯他亚利赛亚利代瓦耶撒他10这十人是犹太人的仇敌哈曼的儿子、哈米大他的孙子。但犹太人没有动他们的财物。

11当天,王获悉在书珊城被杀的人数, 12便对以斯帖王后说:“犹太人在书珊城杀了五百人,还杀了哈曼的十个儿子,在其余各省就更不知怎样了!现在你要什么?必赐给你。你还有何要求?必为你成全。” 13以斯帖回答说:“王若愿意,就请恩准书珊城的犹太人明天仍执行今天的谕旨,并把哈曼十个儿子的尸体吊在木架上。” 14王允准了,便在书珊城颁布谕旨,哈曼十个儿子的尸体便被吊了起来。 15亚达月十四日,书珊城的犹太人再次聚集起来,在城中杀了三百人,但没有动他们的财物。

16王其他各省的犹太人也都聚集起来自卫,得以脱离仇敌。他们杀了七万五千个仇敌,但没有动他们的财物。 17这事发生在亚达月十三日。十四日,犹太人休息,并以此日为设宴欢庆的日子。 18书珊城的犹太人在十三、十四日聚集杀敌,十五日才休息,并以此日为设宴欢庆的日子。 19因此,住在乡村的犹太人都以亚达月十四日为设宴欢庆的节日,并互赠礼物。

普珥节

20末底改把这些事记录下来,写信给亚哈随鲁王国内远近各省的犹太人, 21吩咐他们每年在亚达月十四、十五日守节期, 22设宴欢庆,互赠礼物,周济穷人,以记念犹太人在此月此日得以脱离仇敌,化忧为乐,转悲为喜。

23犹太人接受了末底改写给他们的信,同意每年庆祝这个节日。 24因为犹太人的仇敌亚甲哈米大他的儿子哈曼曾经阴谋毁灭犹太人,曾经抽普珥,即抽签,要杀戮、灭绝他们。 25但王知道这阴谋后,便降旨使哈曼谋害犹太人的恶计落到他自己头上,将他及其众子吊在木架上。 26他们借用普珥这个词,称这两天为普珥节。犹太人因这信上的一切话,又因所看见、所经历的事, 27就为自己、自己的后代和归属他们的人定下规矩:每年必按时守这两天为节日,永不废弃。 28各省各城、家家户户、世世代代都要记念、遵守这节日,使犹太人永不中断过普珥节,他们的后代也不可忘记。

29亚比孩的女儿以斯帖王后和犹太末底改以全权写第二封信,嘱咐犹太人守这普珥节, 30用和善、真诚的话写信给亚哈随鲁王国一百二十七省的所有犹太人, 31嘱咐他们照犹太末底改以斯帖王后的指示,按他们为自己和后代所规定的,按时守普珥节,禁食哀哭。 32以斯帖的命令确定了普珥节,这命令被记载下来。

Kiswahili Contemporary Version

Esta 9:1-32

Ushindi Wa Wayahudi

19:1 Yer 29:4-7; Mit 22:22-23Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari, amri iliyoagizwa na mfalme ilikuwa itekelezwe. Siku hii adui wa Wayahudi walikuwa wametumaini kuwashinda, lakini sasa mambo yaliwageukia na Wayahudi wakawashinda wale waliokuwa wanawachukia. 29:2 Mwa 22:17; Za 35:26Wayahudi walikusanyika katika miji yao, katika majimbo ya Mfalme Ahasuero kuwashambulia wale waliokuwa wanatafuta kuwaangamiza. Hakuna yeyote aliyeweza kushindana nao, kwa sababu watu wa mataifa mengine yote waliwaogopa. 3Nao wakuu wote wa majimbo, majemadari, watawala na maafisa wa mfalme wakawasaidia Wayahudi, kwa sababu walimhofu Mordekai. 49:4 Kum 25:17-19; Ezr 4:6Mordekai alikuwa mtu mashuhuri katika jumba la mfalme; sifa zake zilienea katika majimbo yote naye alipata uwezo zaidi na zaidi.

59:5 Kum 25:17-19; Ezr 4:6Wayahudi waliwaangusha adui zao wote kwa upanga wakiwaua na kuwaangamiza, nao walifanya kile walichotaka kwa wale waliowachukia. 6Katika ngome ya Shushani Wayahudi waliua na kuangamiza wanaume 500. 7Pia waliwaua Parshendatha, Dalfoni, Aspatha, 8Poratha, Adalia, Ardatha, 9Parmashta, Arisai, Aridai na Waizatha, 109:10 Es 5:11; Mwa 14:23wana kumi wa Hamani mwana wa Hamedatha, adui wa Wayahudi. Lakini hawakuchukua nyara.

11Mfalme aliarifiwa siku iyo hiyo hesabu ya waliouawa katika ngome ya Shushani. 129:12 Es 5:6; 7:2Mfalme akamwambia Malkia Esta, “Wayahudi wamewaua wanaume 500 na wana kumi wa Hamani ndani ya ngome ya Shushani. Wamefanyaje katika majimbo mengine ya mfalme yaliyobaki? Je, sasa haja yako ni nini? Nayo pia utapewa. Nalo ombi lako ni nini? Nalo utafanyiwa.”

13Esta akajibu, “Ikimpendeza mfalme, uwape ruhusa Wayahudi walioko Shushani warudie amri ya leo kesho pia, na wana wa Hamani kumi wanyongwe mahali pa kunyongea watu.”

149:14 Ezr 6:11Basi mfalme akaamuru kwamba hili litendeke. Amri ilitolewa huko Shushani, nao wakawanyonga wana kumi wa Hamani. 159:15 Mwa 14:23Wayahudi huko Shushani wakakusanyika pamoja siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, nao wakawaua wanaume 300 huko Shushani, lakini hawakuchukua nyara zao.

169:16 Kum 25:19; 1Nya 4:43Wakati ule ule, Wayahudi wengine waliokuwa kwenye majimbo ya mfalme, wakakusanyika kujilinda nao wakapata nafuu kutokana na adui zao. Waliua adui zao wapatao 75,000 lakini hawakugusa nyara zao. 179:17 1Fal 3:15Hili lilitendeka siku ya kumi na tatu ya mwezi wa Adari na siku ya kumi na nne walipumzika na kuifanya siku ya karamu na furaha.

Kusherehekea Purimu

18Wayahudi huko Shushani, hata hivyo, walikuwa wamekusanyika siku ya kumi na tatu na ya kumi na nne, pia siku ya kumi na tano walipumzika na kuifanya siku ya karamu na furaha.

199:19 Ufu 11:10Ndiyo sababu Wayahudi wanaokaa vijijini na katika miji midogo huadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kama siku ya furaha na karamu, siku ambayo wao hupeana zawadi mmoja kwa mwingine.

20Mordekai aliandika matukio haya, naye akapeleka barua kwa Wayahudi wote walioko katika majimbo ya Mfalme Ahasuero, majimbo yaliyo mbali na karibu, 21akiwataka kila mwaka washerehekee siku ya kumi na nne na ya kumi na tano ya mwezi wa Adari 229:22 Neh 8:12; Za 30:11-12kama wakati ambao Wayahudi walipata nafuu kutoka kwa adui zao na kama mwezi ambao huzuni yao iligeuzwa kuwa furaha na kuomboleza kwao kuwa siku ya kusherehekea. Aliwaandikia kushika siku hizo kama siku za karamu na za furaha na kupeana zawadi za vyakula wao kwa wao na zawadi kwa maskini.

23Hivyo Wayahudi walikubali kuendeleza sherehe walizokuwa wamezianza, wakifanya lile Mordekai alilokuwa amewaandikia. 249:24 Kut 17:8-16; Law 16:8Kwa maana Hamani mwana wa Hamedatha Mwagagi, adui wa Wayahudi wote, alikuwa amepanga hila dhidi ya Wayahudi ili kuwaangamiza, na alikuwa amepiga puri (yaani kura) kwa ajili ya maangamizi na uharibifu wao. 259:25 Za 7:16; Es 7:10Lakini wakati shauri hilo baya lilipoarifiwa kwa mfalme, alitoa amri iliyoandikwa kwamba mipango mibaya ambayo Hamani ameipanga dhidi ya Wayahudi inapasa imrudie juu ya kichwa chake mwenyewe, na kwamba yeye na wanawe waangikwe mahali pa kunyongea watu. 26(Kwa hiyo siku hizi ziliitwa Purimu, kutokana na neno puri.) Kwa sababu ya kila kitu kilichoandikwa kwenye barua hii na kwa sababu ya yale waliyoyaona na yale yaliyowatokea, 27Wayahudi wakachukua na kuifanya desturi kwamba wao na wazao wao na wote ambao walijiunga nao wangefanya bila kuacha kushika siku hizi mbili kila mwaka, kwa njia ilivyoelekezwa na kwa wakati wake. 28Siku hizi zinapasa zikumbukwe na kuadhimishwa katika kila kizazi, kila jamaa na katika kila jimbo na kila jiji. Nazo siku hizi za Purimu kamwe zisikome kusherehekewa na Wayahudi, wala kumbukumbu zake zisipotee miongoni mwa wazao wake.

29Basi Malkia Esta binti Abihaili, pamoja na Mordekai, Myahudi, waliandika kwa mamlaka yote kuthibitisha barua hii ya pili kuhusu Purimu. 309:30 Es 1:1Naye Mordekai akatuma barua kwa Wayahudi wote katika majimbo 127 ya ufalme wa Ahasuero, barua zenye maneno ya amani na matumaini, 319:31 Es 4:1-3ili kuimarisha siku hizi za Purimu katika majira yake yaliyowekwa, kama Mordekai, Myahudi na Malkia Esta walivyowaamuru, na walivyojiimarisha wenyewe na wazao wao kuhusu nyakati za kufunga na kuomboleza. 32Amri ya Esta ilithibitisha taratibu hizi kuhusu Purimu, nayo ikaandikwa katika kumbukumbu.