La Bibbia della Gioia

Giovanni 15

La vera vite

1Poi Gesù disse: «Io sono la vera vite, e mio Padre è il contadino. È lui che recide ogni ramo che è in me e non dà frutti, mentre pota i rami fertili, perché producano ancora di più. Voi siete già puri grazie al Vangelo che vi ho annunciato. Restate uniti a me, ed io resterò unito a voi, perché, se un tralcio non può dar frutti quando è staccato dalla vite, neppure voi potete darne se non siete uniti a me.

Proprio così: io sono la vite, voi i tralci. Chi rimane unito a me ed io a lui, produce molti frutti. Senza di me, invece, non potete far nulla. Se uno si separa da me, viene gettato via come un tralcio reciso, che si secca, poi viene raccolto e gettato nel fuoco a bruciare. Ma se restate uniti a me e ubbidite ai miei comandamenti, potete chiedere tutto ciò che volete e vi sarà dato. Ecco che cosa glorifica mio Padre: che voi produciate frutti in abbondanza e siate così miei discepoli.

Vi ho amato, proprio come mio Padre ha amato me. Rimanete nel mio amore! 10 Se metterete in pratica i miei comandamenti, vivrete nel mio amore, come io ho messo in pratica i comandamenti di mio Padre e vivo nel suo amore. 11 Vi ho detto questo, perché siate pieni della mia gioia e la vostra felicità sia completa! 12 Questo è il mio comandamento: amatevi a vicenda, come vi ho amati io. 13 Ecco la misura dellʼamore: nessuno dimostra amore più grande di chi dà la propria vita per gli amici. 14 Se mi ubbidite, voi siete miei amici. 15 Non vi chiamo più servi, perché i servi non sanno che cosa fa il loro padrone. Ora siete miei amici, perché vi ho detto tutto ciò che ho udito dal Padre.

16 Non siete stati voi che avete scelto me, ma io che ho scelto voi, perché andiate e produciate frutto, un frutto duraturo, perché qualsiasi cosa chiediate al Padre nel mio nome, egli ve la conceda. 17 Questo vi ordino: di amarvi a vicenda. 18 Se il mondo vi odia, sappiate che, prima di voi, ha odiato me. 19 Il mondo vi amerebbe se foste suoi; ma non lo siete, perché scegliendovi, io vi ho fatto uscire dal mondo. Per questo il mondo vi odia. 20 Vi ricordate ciò che vi dissi? Un servo non è più importante del suo padrone. Perciò, se hanno perseguitato me, perseguiteranno anche voi. Se hanno ascoltato me, ascolteranno anche voi. 21 La gente del mondo vi perseguiterà, perché siete miei e perché non conosce Dio che mi ha mandato.

22 Certo, se non fossi venuto e non li avessi informati non avrebbero colpa; ma ora non hanno più scuse per i loro peccati. 23 Chi odia me, odia anche mio Padre. 24 Se non avessi compiuto davanti ai loro occhi quei miracoli che nessun altro ha mai fatto non avrebbero colpa. Invece, anche dopo aver visto questi miracoli, hanno odiato me e mio Padre. 25 Si è così avverato ciò che è scritto nella loro Legge: “Mi hanno odiato senza ragione”.

26 Ma quando sarò col Padre, vi manderò il Consolatore, lo Spirito Santo, Spirito di verità che proviene dal Padre stesso. Egli verrà da voi e testimonierà sul mio conto.

27 Anche voi parlerete di me con tutti, perché siete stati con me sin dal principio.

Neno: Bibilia Takatifu

Yohana 15

Mzabibu Wa Kweli

1‘Mimi ni mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata; na kila tawi lizaalo, yeye hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya mafundisho nili yowapa. Kaeni ndani yangu nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda pasipo kuwa sehemu ya mzabibu, vivyo hivyo, ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kufanya lo lote. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; anayekaa ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa matunda mengi sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea. Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lo lote mtakalo nanyi mtatendewa. Mnapozaa matunda kwa wingi Baba yangu anatukuzwa, na hivyo mnadhihirisha kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.

“Kama Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivy owapenda ninyi; dumuni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu mtakaa ndani ya pendo langu kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

11 “Nimewaambia haya kusudi furaha yangu iwe ndani yenu, nanyi mpate kuwa na furaha iliyokamilika.

12 “Amri yangu ni hii: pendaneni kama nilivyowapenda. 13 Hakuna mtu mwenye upendo unaozidi ule wa mtu anayejitoa afe kwa ajili ya rafiki zake. 14 Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafa nya ninayowaagiza. 15 Siwaiti ninyi watumishi tena kwa sababu mtumishi haelewi shughuli za bwana wake; bali nimewaita rafiki, kwa maana mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu nimewa fahamisha. 16 Hamkunichagua, bali mimi nimewachagua ninyi na nimewatuma mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu, ili lo lote mtakalomwomba Baba katika jina langu, awatimizie. 17 Hii ndio amri yangu: pendaneni.

18 “Kama ulimwengu ukiwachukia, fahamuni kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi. 19 Kama mngekuwa watu wa ulim wengu huu, ulimwengu ungeliwapenda. Ulimwengu unawachukia kwa sababu ninyi si wa ulimwengu huu na mimi nimewachagua kutoka katika ulimwengu.

20 “Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi na ninyi pia watawatesa; kama wamelishika neno langu na neno lenu watalishika pia. 21 Lakini yote haya watawatendea kwa ajili yangu kwa sababu hawamfahamu Baba yangu ambaye amenituma. 22 Kama sikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia. Lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi zao. 23 Mtu ye yote anayenichukia mimi anamchukia na Baba yangu. 24 Kama nilikuwa sikuwafanyia miujiza ambayo haijapata kufanywa na mtu mwingine ye yote, wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini wameona miujiza hii na bado wakatuchukia mimi na Baba yangu. 25 “Hali hii imetokea kama ilivyoandikwa katika Sheria kwamba, ‘Walinichukia pasipo sababu.’ 26 Lakini atakapokuja yule Msaidizi nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, yaani yule Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi. 27 Na ninyi pia ni mashahidi wangu kwa maana tangu mwanzo mmekuwa pamoja nami.”