Marko 5:21-43

Yesu Amponya Mama Aliyetokwa Damu

Yesu alipokwisha vuka tena na kufika ng’ambo ya pili, umati mkubwa wa watu ukamzunguka, yeye akiwa kando ya ziwa. Kisha kiongozi mmoja wa sinagogi aliyeitwa Yairo akamjia Yesu akapiga magoti miguuni pake, akamsihi, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa mahututi. Tafadhali njoo umguse kwa mikono yako apate kupona na kuishi.” Basi Yesu akaongozana naye. Umati mkubwa wa watu waliomfuata wakawa wanamsonga.

Na alikuwepo mama mmoja aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili. Mama huyu alikuwa amehangaika sana, akiwa ametibiwa na waganga wa kila aina na kutumia fedha yake yote kwa waganga lakini hakupata nafuu. Hali yake ilizidi kuwa mbaya. Alikuwa amesikia habari za Yesu kwa hiyo alimfuata kwa nyuma, akapenyeza kati ya watu, akaligusa vazi lake. Maana alisema moyoni mwake, “Nikiligusa vazi lake tu, nitapona.” Mara damu iliyokuwa inamtoka ikakauka; akajisikia amepona kabisa.

Yesu akafahamu kuwa nguvu zimemtoka. Akageuka, akawauliza wale watu, “Ni nani amenigusa?”

Wanafunzi wake wakamjibu, “Mbona unauliza ni nani ameku gusa? Huoni umati huu ulivyokusonga?” Lakini Yesu alizidi kutazama aone ni nani aliyemgusa. Kisha yule mwanamke, akijua kilichomtokea, akaja, akaanguka miguuni kwake akitetemeka kwa hofu, akamweleza ukweli wote. Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani, upone kabisa ugonjwa wako.”

Yesu Amfufua Binti Yairo

Alipokuwa akiongea, watu wakafika kutoka nyumbani kwa Yairo wakamwambia, “Usimsumbue tena mwalimu, binti yako amefar iki. ” Lakini Yesu hakuyatilia maanani maneno hayo, akamwam bia Yairo, “Usiogope, bali amini tu.”

Hakumruhusu mtu mwingine amfuate isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, nduguye Yakobo.

Walipofika nyumbani kwa yule kiongozi wa sinagogi, Yesu aliona vurugu na watu wengi wakilia na kuomboleza kwa nguvu. Alipoingia ndani, aliwaambia, “Kwa nini mnafanya vurugu na kuomboleza? Mtoto hakufariki bali amelala.” Wale watu wakam cheka kwa dharau. Lakini yeye akawatoa wote nje, akawachukua baba na mama wa yule mtoto pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao, wakaenda pale alipokuwa yule mtoto. Akamwinua mtoto akamwam bia, “Talitha kumi!” Maana yake, “Binti mdogo, nakwambia amka!’ ’

Mara yule mtoto akasimama, akaanza kutembea. Alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili. Walipoona haya, walistaajabu sana. Yesu akawaamuru wasimweleze mtu jambo hili, na akawaambia wampe yule mtoto chakula.

Read More of Marko 5

Marko 6:1-6

Watu Wa Nazareti Wamkataa Yesu

Yesu akaondoka mahali hapo, akaenda mji wa kwao, akifu atana na wanafunzi wake. Ilipofika siku ya sabato, alianza ku fundisha katika sinagogi na wengi waliomsikia walishangaa. Wakasema, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya? Amepataje kuwa na hekima ya namna hii? Amepata wapi uwezo wa kutenda miujiza ya namna hii? Huyu si yule seremala mtoto wa Mariamu? Na ndugu zake si Yakobo, Yose, Yuda na Simoni? Dada zake si tuko nao hapa?” Basi hawakumwamini.

Yesu akawaambia, ‘ ‘Nabii huheshimiwa kila mahali isipokuwa katika mji wake na kati ya jamaa na ndugu zake.” Hakufanya miujiza yo yote huko isipokuwa kuwagusa wagonjwa wachache na kuwaponya. Alishangazwa sana na jinsi walivyokuwa hawana imani.

Read More of Marko 6