Luka 7:11-35

Yesu Amfufua Mtoto Wa Mjane

Baada ya siku hiyo, Yesu alikwenda mji mmoja uitwao Naini. Wanafunzi wake na umati wa watu waliongozana naye. Alipokaribia njia ya kuingia mjini alikutana na watu wal iobeba maiti wakitoka nje ya mji. Marehemu alikuwa mtoto wa kiume wa pekee wa mama mmoja mjane na umati wa watu wa mji ule ulikuwa pamoja na huyo mama. Bwana Yesu alipomwona yule mjane moyo wake ulijaa huruma, akamwambia, “Usilie.” Kisha akalisoge lea lile jeneza akaligusa na wale waliolibeba wakasimama. Ndipo akasema: “Kijana nakuambia, amka!” Yule aliyekuwa marehemu akaamka, akakaa na akaanza kusema! Yesu akamkabidhi kwa mama yake.

Watu wote wakajawa na hofu. Wakamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea kati yetu. Mungu amekuja kutuokoa sisi watu wake.” Habari hizi za mambo aliyofanya Yesu zikaenea Uyahudi nzima na sehemu za jirani.

Hakuna Aliye Mkuu Kuliko Yohana

Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walipomweleza Yohana habari hizi zote aliwaita wawili kati yao akawatuma wakamwulize Bwana Yesu, “Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?”

Wakati huo huo, Yesu aliwaponya wengi waliokuwa na magonjwa, maumivu na pepo wachafu. Pia akawawezesha vipofu wengi kuona. Ndipo akawajibu wale wanafunzi waliotumwa, “Nendeni mkamwambie Yohana yote mliyoyaona na kusikia: vipofu wanapata kuona, vilema wanatembea, wenye ukoma wanapona, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanasikia Habari Njema. Amebari kiwa mtu asiyepoteza imani yake kwangu.” Wanafunzi wa Yohana walipoondoka, Yesu akaanza kuwaeleza watu juu ya Yohana: “Hivi mlipokwenda nyikani mlikwenda kuona nini? Nyasi zikipeperushwa na upepo? Kama sivyo, mlikwenda kuona nini basi? Mtu aliyevaa nguo za fahari? Sidhani! Watu wanaovaa nguo za fahari na kuishi maisha ya anasa hukaa katika majumba makubwa. Sasa mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kuona nabii? Naam! Tena aliye mkuu kuliko nabii. Huyu Yohana ndiye anayezungumzwa katika Maandiko yase mayo: ‘Tazama, namtuma mjumbe wangu akutangulie, ili akuandalie njia.’ Nawaambia, kati ya binadamu wote, hakuna aliye mkuu kumzidi Yohana. Hata hivyo aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yohana. Watu wote waliosikia maneno hayo, ikiwa ni pamoja na watoza ushuru, walimtukuza Mungu kwa kuwa wao waliukubali ubatizo wa Yohana. Bali Mafarisayo na wanasheria walikataa mpango wa Mungu kwao kwa kutokukubali kubatizwa na Yohana. Yesu akawau liza, “Niseme nini juu ya watu wa kizazi hiki? Niwafananishe na nini? Wao wamefanana na watoto waliokaa sokoni wakijibizana na wenzao wakisema: ‘Tuliwaimbia nyimbo za shangwe, hamkucheza. Tuliwaimbia nyimbo za msiba, hamkuomboleza.’ Yohana Mbatizaji alikuwa akifunga na hakuonja divai maishani mwake, ninyi mkasema, ‘Ana wazimu!’ Lakini mimi nakula na kunywa, nanyi mnasema: ‘Mtazameni mlafi na mlevi! Rafiki wa watoza kodi na wenye dhambi.’ Lakini hekima ya Mungu inadhihirishwa kuwa kweli na wote wanaoipokea.”

Read More of Luka 7