2 Wakorintho 1:23

Mungu ni shahidi wangu kwamba niliacha kurudi Korintho kwa kuwahurumia.

Read More of 2 Wakorintho 1

2 Wakorintho 2:1-11

Kwa sababu hiyo, niliamua kwamba sitafanya safari nyingine kuja kuwahuzunisha. Kwa kuwa kama nawahuzunisha, ni nani ali yebaki kunifurahisha isipokuwa ninyi ambao nimewahuzunisha? Ndio sababu nikawaandikia ili nitakapokuja nisihuzunishwe na watu ambao wangenifanya nifurahi. Nilikuwa na uhakika kwenu kwamba furaha yangu ingekuwa furaha yenu nyote. Kwa maana nili waandikia katika dhiki na kutaabika moyoni na kwa machozi mengi. Shabaha yangu haikuwa kuwahuzunisha bali kuwaonyesha kina cha upendo wangu kwenu.

Msamaha Kwa Mwenye Dhambi

Basi ikiwa mtu ye yote amesababisha huzuni, kwa kiasi fulani hakunihuzunisha mimi kama alivyowahuzunisha ninyi nyote; sipendi kuweka uzito zaidi kwa upande wenu. Basi adhabu aliyop ewa na wengi inamtosha. Na sasa mnapaswa kumsamehe na kumfariji ili asikate tamaa kabisa kutokana na huzuni kubwa mno aliyo nayo. Kwa hiyo nawasihi mumhakikishie tena kwamba mnampenda. Nili waandikia kuwajaribu ili nione kama mtakuwa watii kwa kila kitu. Mtu ye yote mnayemsamehe na mimi namsamehe. Cho chote nili chosamehe, kama kulikuwa na cha kusamehe, nimesamehe kwa ajili yenu mbele ya Kristo ili shetani asije akatushinda. Kwa maana tunajua mipango yake.

Read More of 2 Wakorintho 2