Warumi 9:22-33, Warumi 10:1-4 NEN

Warumi 9:22-33

9:22 Rum 2:4Iweje basi, kama Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake na kufanya uweza wake ujulikane, amevumilia kwa uvumilivu mwingi vile vyombo vya ghadhabu vilivyoandaliwa kwa uharibifu? 9:23 Rum 8:28; 8:30Iweje basi, kama yeye alitenda hivi ili kufanya wingi wa utukufu wake ujulikane kwa vile vyombo vya rehema yake, alivyotangulia kuvitengeneza kwa ajili ya utukufu wake, 9:24 Rum 8:28; 3:29yaani pamoja na sisi, ambao pia alituita, si kutoka kwa Wayahudi peke yao, bali pia kutoka kwa watu wa Mataifa?

Yote Yalitabiriwa Katika Maandiko

9:25 Hos 2:23; 1Pet 2:10Kama vile Mungu asemavyo katika Hosea:

“Nitawaita ‘watu wangu’

wale ambao si watu wangu;

nami nitamwita ‘mpenzi wangu’

yeye ambaye si mpenzi wangu,”

9:26 Hos 1:10; Mt 16:16tena,

“Itakuwa hasa mahali pale walipoambiwa,

‘Ninyi si watu wangu,’

wao wataitwa ‘wana wa Mungu aliye hai.’ ”

9:27 Mwa 22:17; Isa 10:22-23; Hos 1:10; Yoe 2:32; Rum 11:5Isaya anapiga kelele kuhusu Israeli:

“Ingawa idadi ya wana wa Israeli

ni wengi kama mchanga wa pwani,

ni mabaki yao tu watakaookolewa.

Kwa kuwa Bwana ataitekeleza

hukumu yake duniani kwa haraka

na kwa ukamilifu.”

9:29 Yak 5:4; Isa 1:9; 13:19; Yer 50; 40Ni kama vile alivyotabiri Isaya akisema:

“Kama Bwana Mwenye Nguvu Zote

asingelituachia uzao,

tungelikuwa kama Sodoma,

tungelifanana na Gomora.”

Kutokuamini Kwa Israeli

9:30 Flp 3:9; Ebr 11:17Kwa hiyo tuseme nini basi? Kwamba watu wa Mataifa ambao hawakutafuta haki, wamepata haki ile iliyo kwa njia ya imani. 9:31 Isa 51:11; Rum 11:7; Gal 5:4Lakini Israeli, ambao walijitahidi kupata haki kwa njia ya sheria, hawakuipata. 9:32 1Pet 2:8Kwa nini? Kwa sababu hawakuitafuta kwa njia ya imani bali kwa njia ya matendo. Wakajikwaa kwenye lile “jiwe la kukwaza.” 9:33 Isa 8:14; 1Pet 2:6, 8Kama ilivyoandikwa:

“Tazama naweka katika Sayuni jiwe la kukwaza watu

na mwamba wa kuwaangusha.

Yeyote atakayemwamini

hataaibika kamwe.”

Read More of Warumi 9

Warumi 10:1-4

10:1 Za 20:4; Mdo 22:23Ndugu zangu, shauku ya moyo wangu na maombi yangu kwa Mungu ni kwa ajili ya Waisraeli, kwamba waokolewe. 10:2 Mdo 21:20; 22:3; Gal 1:14; 4:17; Rum 9:32Kwa maana ninaweza nikashuhudia wazi kwamba wao wana juhudi kubwa kwa ajili ya Mungu, lakini juhudi yao haina maarifa. 10:3 Rum 1:17; 9:31; Flp 3:9Kwa kuwa hawakuijua haki itokayo kwa Mungu, wakatafuta kuweka haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. Kwa maana Kristo ni ukomo wa sheria ili kuwe na haki kwa kila mtu aaminiye.

Read More of Warumi 10