Warumi 14:1-18 NEN

Warumi 14:1-18

Msiwahukumu Wengine

14:1 1Kor 8:9-12; 9:22Mkaribisheni yeye ambaye imani yake ni dhaifu, lakini si kwa kugombana na kubishana juu ya mawazo yake. 14:2 Rum 14:14; 1Kor 10:25; 1Tim 4:4; Tit 1:15Mtu mmoja imani yake inamruhusu kula kila kitu, lakini mwingine ambaye imani yake ni dhaifu, hula mboga tu. 14:3 Lk 18:9; Kol 2:16Yeye alaye kila kitu asimdharau yeye asiyekula. Wala yeye asiyekula kila kitu asimhukumu yule alaye kila kitu, kwa maana Mungu amemkubali. 14:4 Mt 7:1; Yak 4:12Wewe ni nani hata umhukumu mtumishi wa mtu mwingine? Kwa bwana wake tu anasimama au kuanguka. Naye atasimama kwa sababu Bwana anaweza kumsimamisha.

14:5 Gal 4:10; Kol 2:16Mtu mmoja anaitukuza siku fulani kuwa ni bora kuliko nyingine, na mwingine anaona kuwa siku zote ni sawa. Basi kila mmoja awe na hakika na yale anayoamini. 14:6 Mt 14:19; 1Tim 4:3, 4Yeye anayehesabu siku moja kuwa takatifu kuliko nyingine, hufanya hivyo kwa kumheshimu Bwana. Naye alaye nyama hula kwa Bwana, kwa maana humshukuru Mungu, naye akataaye kula nyama hufanya hivyo kwa Bwana na humshukuru Mungu. 14:7 2Kor 5:15; Gal 2:20Kwa kuwa hakuna hata mmoja wetu anayeishi kwa ajili yake mwenyewe, wala hakuna hata mmoja wetu afaye kwa ajili yake mwenyewe. 14:8 Flp 1:20; Gal 2:20; 1The 5:10; Lk 20:38Kama tunaishi, tunaishi kwa Bwana, nasi pia tukifa tunakufa kwa Bwana. Kwa hiyo basi, kama tukiishi au kama tukifa, sisi ni mali ya Bwana.

14:9 Ufu 1:18; 2:8; Mdo 10:42; 2Kor 5:15Kwani kwa sababu hii hasa, Kristo alikufa na akawa hai tena kusudi apate kuwa Bwana wa wote, yaani, waliokufa na walio hai. 14:10 2Kor 5:10; Mdo 17:31; Mt 25:31, 32; 7:1; 2Kor 5:10Basi kwa nini wewe wamhukumu ndugu yako? Au kwa nini wewe unamdharau ndugu yako? Kwa kuwa sote tutasimama mbele ya kiti cha Mungu cha hukumu. 14:11 Isa 45:23; Flp 2:10, 11Kwa kuwa imeandikwa:

“ ‘Kama vile niishivyo,’ asema Bwana,

‘kila goti litapigwa mbele zangu,

na kila ulimi utakiri kwa Mungu.’ ”

14:12 Mt 12:36; 1Pet 4:5Hivyo basi kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe kwa Mungu.

Usimfanye Ndugu Yako Ajikwae

14:13 Mt 7:1; Rum 14:1; 2Kor 8:9, 13Kwa hiyo tusiendelee kuhukumiana: Badala yake mtu asiweke kamwe kikwazo au kizuizi katika njia ya ndugu mwingine. 14:14 Mdo 10:15; 1Kor 8:7Ninajua tena nimehakikishiwa sana katika Bwana Yesu kwamba hakuna kitu chochote ambacho ni najisi kwa asili yake. Lakini kama mtu anakiona kitu kuwa ni najisi, basi kwake huyo kitu hicho ni najisi. 14:15 Efe 5:2; 1Kor 8:7Kama ndugu yako anahuzunishwa kwa sababu ya kile unachokula, basi huenendi tena katika upendo. Usiruhusu kile unachokula kiwe sababu ya kumwangamiza ndugu yako ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. 14:16 1Kor 10:30; Tit 2:5; Rum 12:17Usiruhusu kile ambacho unakiona kuwa chema kisemwe kuwa ni kiovu. 14:17 1Kor 8:8; Gal 5:22Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu. 14:18 Lk 2:52; Mdo 24:16Kwa sababu mtu yeyote anayemtumikia Kristo kwa jinsi hii, anampendeza Mungu na kukubaliwa na wanadamu.

Read More of Warumi 14