Warumi 1:1-17 NEN

Warumi 1:1-17

1:1 1Kor 1:1; Mdo 9:15; 1The 2:8, 9; 1Pet 4:17Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu, 1:2 Gal 3:8; Tit 1:2; Rum 16:25, 26; Mdo 26:6; 3:21; Mt 4:3Injili ambayo Mungu alitangulia kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika Maandiko Matakatifu, 1:3 Yn 1:14; Rum 9:5yaani, Injili inayomhusu Mwanawe, yeye ambaye kwa uzao wa mwili alikuwa mzao wa Daudi, 1:4 Mt 4:3; Mdo 2:24; 1Kor 1:2; Mdo 13:33na ambaye kwa uwezo wa Roho wa utakatifu alidhihirishwa kuwa Mwana wa Mungu kwa ufufuo wake kutoka kwa wafu, yaani, Yesu Kristo, Bwana wetu. 1:5 Mdo 9:15; 6:7; Rum 16:27Kwa kupitia kwake na kwa ajili ya Jina lake, tumepokea neema na utume ili kuwaita watu miongoni mwa watu wa mataifa yote, waje kwenye utii utokanao na imani. 1:6 Yud 1; Ufu 17:14Ninyi nyote pia mko miongoni mwa watu walioitwa ili mpate kuwa mali ya Yesu Kristo.

1:7 Rum 8:39; 1The 1:4; Efe 1:2; Tit 1:4Kwa wote walioko Rumi wapendwao na Mungu na kuitwa kuwa watakatifu:

Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi.

Maombi Na Shukrani

1:8 Efe 1:16; 1The 2:13; Rum 10:18; 16:19Kwanza kabisa, namshukuru Mungu wangu kwa njia ya Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inatangazwa duniani kote. 1:9 2Tim 1:1; Yer 42:5; Gal 1:20Kwa maana Mungu ninayemtumikia kwa moyo wangu wote katika kuhubiri Injili ya Mwanawe, ni shahidi wangu jinsi ninavyowakumbuka 1:10 Rum 15:32; Mdo 19:21; Rum 15:23, 32; 1Sam 12:23; Lk 18:1; Efe 1:16; Flp 1:4; Kol 1:9; 2The 1:11; 2Tim 1:3; Mdo 18:21; Rum 15:32katika maombi yangu siku zote, nami ninaomba kwamba hatimaye sasa kwa mapenzi ya Mungu, njia ipate kufunguliwa kwa ajili yangu ili nije kwenu.

1:11 Rum 15:23; 1:7; Mdo 28:31Ninatamani sana kuwaona ili nipate kuweka juu yenu karama za rohoni ili mwe imara, 1:12 2Pet 1:1; Tit 1:4au zaidi, ninyi pamoja nami tuweze kutiana moyo katika imani sisi kwa sisi. 1:13 Rum 15:22, 23; Yn 15:16; 1The 2:18; Flp 4:17; Mdo 13:23; 16:7Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba mara nyingi nimekusudia kuja kwenu (ingawa mpaka sasa nimezuiliwa), ili nipate kuvuna mavuno miongoni mwenu kama nilivyovuna miongoni mwa wengine ambao ni watu wa Mataifa wasiomjua Mungu.

1:14 1Kor 9:16Mimi ni mdeni kwa Wayunani na kwa wasio Wayunani, kwa wenye hekima na kwa wasio na hekima. 1:15 Rum 15:20Ndiyo sababu ninatamani sana kuihubiri Injili kwenu pia ninyi mlioko Rumi.

1:16 2Tim 1:8; 1Kor 1:18; Mdo 3:26; 13:26; Rum 2:9, 10Mimi siionei haya Injili ya Kristo kwa maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwanza kwa Myahudi na kwa Myunani pia. 1:17 Rum 3:21; Flp 3:9; Hab 2:4Kwa maana katika Injili haki itokayo kwa Mungu imedhihirishwa, haki ile iliyo kwa njia ya imani hadi imani. Kama ilivyoandikwa: “Mwenye haki ataishi kwa imani.”

Read More of Warumi 1