Zaburi 94:1-11 NEN

Zaburi 94:1-11

Zaburi 94

Mungu Mlipiza Kisasi Kwa Ajili Ya Wenye Haki

94:1 Mwa 4:24; Za 80:1; Rum 12:19; Kum 33:2Ee Bwana, ulipizaye kisasi,

Ee Mungu ulipizaye kisasi, uangaze sasa.

94:2 Mwa 18:25; Yak 5:9; Hes 10:35; Za 31:23Ee Mhukumu wa dunia, inuka,

uwalipize wenye kiburi kama wanavyostahili.

94:3 Za 13:2; Mwa 20:3Hata lini, waovu, Ee Bwana,

hata lini waovu watashangilia?

94:4 Yer 43:2; Za 52:1; Yud 15Wanamimina maneno ya kiburi,

watenda mabaya wote wamejaa majivuno.

94:5 Za 28:9; 44:2; 74:8; Isa 3:15; Yer 8:21Ee Bwana, wanawaponda watu wako,

wanawaonea urithi wako.

94:6 Kum 10:18; 20:19; Isa 1:17Wanamchinja mjane na mgeni,

na kuwaua yatima.

94:7 Ay 22:14; Mwa 24:12Nao husema, “Bwana haoni,

Mungu wa Yakobo hafahamu.”

94:8 Kum 32:6; Za 73:22Sikizeni, enyi wajinga miongoni mwa watu;

enyi wapumbavu, lini mtakuwa na hekima?

94:9 Kut 4:11; Mit 20:12Je, aliyeweka sikio asisikie?

Aliyeumba jicho asione?

94:10 Za 39:11; Ay 35:11; Yn 6:45; Isa 2:3; 28:26; Kut 35:34Je, anayeadhibisha mataifa asiadhibu?

Je, awafundishaye wanadamu asiwe na maarifa?

94:11 Za 139:2; Mt 15:26; 9:4; 1Kor 3:20; 1:21Bwana anajua mawazo ya mwanadamu;

anajua kwamba ni ubatili.

Read More of Zaburi 94