Zaburi 89:1-8 NEN

Zaburi 89:1-8

Zaburi 89

Wimbo Wakati Wa Taabu Ya Kitaifa

Utenzi wa Ethani Mwezrahi.

89:1 Za 59:16; 36:5; 40:10Nitaimba juu ya upendo mkuu wa Bwana milele;

kwa kinywa changu nitajulisha uaminifu wako

ujulikane kwa vizazi vyote.

89:2 Za 36:5Nitatangaza kuwa upendo wako unasimama imara milele

na uaminifu wako umeuthibitisha mbinguni.

89:3 Eze 34:23; Hes 3:5; Ebr 7:21; Mdo 2:30Ulisema, “Nimefanya agano na mteule wangu,

nimemwapia mtumishi wangu Daudi,

89:4 2Sam 7:12-16; Lk 1:32, 33; Mt 1:1; Isa 9:6, 7; Rum 1:3; 1Fal 9:5; 8:16; Eze 37:24, 25; Za 132:11, 12‘Nitaimarisha uzao wako milele

na kudumisha ufalme wako kwa vizazi vyote.’ ”

89:5 Za 19:1; 1:5Ee Bwana, mbingu zinayasifu maajabu yako,

uaminifu wako pia katika kusanyiko la watakatifu.

89:6 Mwa 1:26; Kut 9:14; Za 18:31; 113:5Kwa kuwa ni nani katika mbingu

anayeweza kulinganishwa na Bwana?

Ni nani miongoni mwa viumbe vya mbinguni

aliye kama Bwana?

89:7 Ay 5:1; Za 11:1; 47:2Katika kusanyiko la watakatifu, Mungu huogopwa sana,

anahofiwa kuliko wote wanaomzunguka.

89:8 Isa 6:3; Za 71:19Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote,

ni nani aliye kama wewe?

Ee Bwana, wewe ni mwenye nguvu,

na uaminifu wako unakuzunguka.

Read More of Zaburi 89