Zaburi 78:40-55 NEN

Zaburi 78:40-55

78:40 Kut 23:21; Za 95:8; 106:14; Efe 4:30Mara ngapi walimwasi jangwani

na kumhuzunisha nyikani!

78:41 Kut 17:2; 2Fal 19:22; Za 71:22; 89:18Walimjaribu Mungu mara kwa mara,

wakamkasirisha yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

78:42 Amu 3:7; Neh 9:17; Za 27:11Hawakukumbuka uwezo wake,

siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi,

78:43 Kut 10:1; 3:20siku aliyoonyesha ishara zake za ajabu huko Misri,

maajabu yake huko Soani.

78:44 Kut 7:20, 21; Za 105:29; 78:45Aligeuza mito yao kuwa damu,

hawakuweza kunywa maji kutoka vijito vyao.

78:45 Kut 8:2, 6, 24; Za 105Aliwapelekea makundi ya mainzi yakawala,

na vyura wakawaharibu.

78:46 Nah 3:15; Kut 10:13Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao,

mazao yao kwa nzige.

78:47 Za 105:32; 147:17; Kut 9:23Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe

na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji.

78:48 Kut 9:25Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe,

akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi.

78:49 Kut 15:7; Mwa 19:13; 1Kor 10:10; Rum 2:8Aliwafungulia hasira yake kali,

ghadhabu yake, hasira na uadui,

na kundi la malaika wa kuharibu.

Aliitengenezea njia hasira yake,

hakuwaepusha na kifo,

bali aliwaachia tauni.

78:51 Mwa 9:12; Kut 12:12; Za 135:8; 105:23; 106:22Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri,

matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu.

78:52 Ay 21:11; Za 28:9; 77:20Lakini aliwatoa watu wake kama kundi,

akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani.

78:53 Kut 14:28; 15:7; Za 106:10Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa,

bali bahari iliwameza adui zao.

78:54 Kut 15:17; Za 44:3Hivyo akawaleta hadi kwenye mpaka wa nchi yake takatifu,

hadi nchi ya vilima ambayo mkono wake wa kuume ulikuwa umeitwaa.

78:55 Za 44:2; Kum 1:38; Yos 13:7; Mdo 13:19Aliyafukuza mataifa mbele yao,

na kuwagawia nchi zao kama urithi,

aliwakalisha makabila ya Israeli katika makao yao.

Read More of Zaburi 78