Zaburi 75:1-10 NEN

Zaburi 75:1-10

Zaburi 75

Mungu Ni Mwamuzi

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Zaburi ya Asafu. Wimbo.

75:1 Yos 3:5; Za 44:1; 71:16; 77:12; 105:2; 107:8, 15; 145:5, 12, 18Ee Mungu, tunakushukuru,

tunakushukuru wewe,

kwa kuwa jina lako li karibu;

watu husimulia matendo yako ya ajabu.

75:2 Kut 13:10; Za 7:11Unasema, “Ninachagua wakati maalum;

ni mimi nihukumuye kwa haki.

75:3 Ebr 1:3; Isa 24:19; 1Sam 2:8; 2Sam 22:8Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka,

ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.

75:4 Za 5:5; Zek 1:21; 1Sam 2:3Kwa wale wenye majivuno ninasema,

‘Msijisifu tena,’

kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.

75:5 Ay 15:25Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu;

msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ”

Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi

au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu.

75:7 Mwa 16:5; Ufu 18:8; 1Sam 2:7; Ay 5:11; Za 50:6; 58:11; 147:6; Eze 21:26; Dan 2:21; Lk 1:52Bali Mungu ndiye ahukumuye:

Humshusha huyu na kumkweza mwingine.

75:8 Mit 23:30; Isa 51:17; Yer 25:15; Zek 12:2; Ufu 14:10; Ay 21:20Mkononi mwa Bwana kuna kikombe

kilichojaa mvinyo unaotoka povu

uliochanganywa na vikolezo;

huumimina, nao waovu wote wa dunia

hunywa mpaka tone la mwisho.

75:9 Za 40:10; 76:6; 108:1; Mwa 24:12Bali mimi, nitatangaza hili milele;

nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo.

75:10 Za 89:17; 92:10; 112:9; 148:14Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote,

bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.

Read More of Zaburi 75