Zaburi 73:1-14 NEN

Zaburi 73:1-14

KITABU CHA TATU

(Zaburi 73–89)

Zaburi 73

Haki Ya Mungu

Zaburi ya Asafu.

73:1 Za 24:4; 5:8Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli,

kwa wale ambao mioyo yao ni safi.

73:2 Kum 32:35; Za 69:2; Efe 4:27Bali kwangu mimi, miguu yangu ilikuwa karibu kuteleza;

nilikuwa karibu mguu wangu kuachia uliposimama.

73:3 Mit 3:31; 23:17; 24:1-2; Ay 9:24; 21:7; Yer 12:1; Mal 3:15Kwa maana niliwaonea wivu wenye kujivuna

nilipoona kufanikiwa kwa waovu.

Wao hawana taabu,73:4 Tafsiri nyingine zinasema: hawana maumivu katika kufa kwao.

miili yao ina afya na nguvu.

73:5 Za 73:12; Eze 23:42Hawapati shida zinazowataabisha watu wengine,

wala hawapati mapigo kama wanadamu wengine.

73:6 Law 26:19; Mwa 6:11; 41:42; Wim 4:9; Eze 16:11; Mit 4:17; Mhu 8:11Kwa hiyo kiburi ni mkufu wao,

wamejivika jeuri.

73:7 Za 7:10Uovu hutoka katika mioyo yao iliyokufa ganzi,

majivuno maovu kutoka mioyoni mwao hauna kikomo.

73:8 Za 10:7; 12:5; 41:5; Eze 25:15; Kol 3:8; 2Pet 2:18; Yud 16Hudhihaki na kusema kwa ukorofi,

katika majivuno yao wanatishia kutesa.

73:9 Ufu 13:6Vinywa vyao huweka madai hata kwa mbingu,

nazo ndimi zao humiliki duniani.

Kwa hiyo watu wao huwageukia

na kunywa maji tele.73:10 Au: na kupokea yote wasemayo.

73:11 Ay 22:13; Za 94:7Wanasema, “Mungu awezaje kujua?

Je, Yeye Aliye Juu Sana anayo maarifa?”

73:12 Za 73:5; 49:6Hivi ndivyo walivyo waovu:

siku zote hawajali,

wanaongezeka katika utajiri.

73:13 Ay 9:29-31; 21:15; Za 24:4; Mal 3:14; Mwa 44:16; Ebr 10:19-22Hakika nimeuweka moyo wangu safi bure,

ni bure nimenawa mikono yangu nisiwe na hatia.

73:14 Za 73:5Mchana kutwa nimetaabika,

nimeadhibiwa kila asubuhi.

Read More of Zaburi 73