Zaburi 68:21-27 NEN

Zaburi 68:21-27

68:21 Za 74:14; 110:5; Hab 3:13Hakika Mungu ataponda vichwa vya adui zake,

vichwa vya hao waendao katika njia za dhambi.

68:22 Ay 36:30; Mt 18:6Bwana alisema, “Nitawarudisha kutoka Bashani;

nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari,

68:23 Za 58:10; 1Fal 21:19; 2Fal 9:36ili uweze kuchovya miguu yako katika damu ya adui zako,

huku ndimi za mbwa wako zikiwa na fungu lake.”

68:24 Za 63:2Ee Mungu, maandamano yako yameonekana,

maandamano ya Mungu wangu, Mfalme wangu,

yakielekea patakatifu pake.

68:25 1Nya 15:16; 6:31; 2Nya 5:12; Ufu 18:22; Mwa 31:27; Isa 5:12Mbele wako waimbaji, baada yao wapiga vinanda,

pamoja nao wako wanawali wakipiga matari.

68:26 Za 22:22; Ebr 2:12; Law 19:2Msifuni Mungu katika kusanyiko kubwa,

msifuni Bwana katika kusanyiko la Israeli.

68:27 1Sam 9:21; Hes 34:21; Amu 5:18Liko kabila dogo la Benyamini likiwaongoza,

wakifuatwa na kundi kubwa la watawala wa Yuda,

hatimaye watawala wa Zabuloni na Naftali.

Read More of Zaburi 68