Zaburi 59:1-8 NEN

Zaburi 59:1-8

Zaburi 59

Kuomba Ulinzi Wa Mungu

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi. Wakati Sauli alipotuma wapelelezi nyumbani mwa Daudi ili wamuue.

59:1 Za 82:259:1 Za 143:9; 20:1Ee Mungu, uniokoe na adui zangu,

unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu.

59:2 Za 14:4; 36:12; 53:4; 92:7; 94:16; 26:9; 139:19; Mit 29:10Uniponye na watu watendao mabaya,

uniokoe kutokana na wamwagao damu.

59:3 Za 56:6; 1Sam 26:18Tazama wanavyonivizia!

Watu wakali wananifanyia hila,

ingawa Ee Bwana, mimi sijakosea

wala kutenda dhambi.

59:4 Za 13:3; 119:3; Mt 5:11Sijatenda kosa; hata hivyo wako tayari kunishambulia.

Inuka unisaidie, uone hali yangu mbaya!

59:5 Za 69:6; 80:4; 84:8; 44:23; 9:5; Isa 10:3; Yer 18:23; Dan 4:35Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli!

Zinduka uyaadhibu mataifa yote,

usionyeshe huruma kwa wasaliti.

59:6 Za 22:16Hurudi wakati wa jioni,

wakibweka kama mbwa,

wakiuzurura mji.

59:7 Za 55:21; 94:4; Mit 10:32; 12:23; 15:2, 28; Ay 22:13Tazama yale wanayotema kutoka vinywa vyao,

hutema upanga kutoka midomo yao,

nao husema, “Ni nani atakayetusikia?”

59:8 Za 2:4; 37:13; Mit 1:26Lakini wewe, Bwana, uwacheke;

unayadharau mataifa hayo yote.

Read More of Zaburi 59