Zaburi 53:1-6
Zaburi 53
Uovu Wa Wanadamu
(Zaburi 14)
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi. Utenzi wa Daudi.
53:1 Za 107:17; 74:22; 10:4; Mit 10:23; Rum 3:10Mpumbavu anasema moyoni mwake,
“Hakuna Mungu.”
Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa,
hakuna hata mmoja atendaye mema.
53:2 Za 33:13; 82:5; Yer 4:22; 8:8; 2Nya 15:2Mungu anawachungulia wanadamu chini
kutoka mbinguni
aone kama wako wenye akili,
wowote wanaomtafuta Mungu.
53:3 Rum 3:10-12; Mhu 7:29Kila mmoja amegeukia mbali,
wameharibika wote pamoja,
hakuna atendaye mema.
Naam, hakuna hata mmoja!
53:4 Yer 4:22Je, watendao mabaya kamwe hawatajifunza:
wale ambao huwala watu wangu
kama watu walavyo mkate,
hao ambao hawamwiti Mungu?
53:5 Law 26:17; Eze 6:5; 2Fal 17:20; 23:14; Za 141:7; Mao 5:22; Yer 6:30; 14:19; 8:1; Ay 8:22Hapo waliingiwa na hofu kuu,
ambapo hapakuwa cha kutetemesha.
Mungu alitawanya mifupa ya wale waliokushambulia;
uliwaaibisha, kwa sababu Mungu aliwadharau.
Laiti wokovu wa Israeli ungalikuja kutoka Sayuni!
Wakati Mungu arejeshapo wafungwa wa watu wake,
Yakobo na ashangilie, Israeli na afurahi!