Zaburi 48:9-14 NEN

Zaburi 48:9-14

48:9 Za 39:3; 6:4Ee Mungu, hekaluni mwako

tunatafakari upendo wako usiokoma.

48:10 Kut 6:3; Isa 11:12; 24:16; 42:10; 49:6; Yos 7:9; 1Sam 2:10; Za 22:27; 100:1; 65:5; 98:3; Mal 1:1Ee Mungu, kama jina lako lilivyo,

sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia,

mkono wako wa kuume umejazwa na haki.

48:11 Za 97:8Mlima Sayuni unashangilia,

vijiji vya Yuda vinafurahi

kwa sababu ya hukumu zako.

48:12 Neh 3:1Tembeeni katika Sayuni,

uzungukeni mji,

hesabuni minara yake;

48:13 2Sam 20:15; Isa 26:1; Mao 2:8; Hab 2:1; Za 78:6; 71:18; 109:13yatafakarini vyema maboma yake,

angalieni ngome zake,

ili mpate kusimulia habari zake

kwa kizazi kijacho.

48:14 Za 25:5; 73:24; Mit 6:22; Isa 25:9; 49:10; 57:18; 58:11Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele;

atakuwa kiongozi wetu hata mwisho.

Read More of Zaburi 48