Zaburi 44:1-12 NEN

Zaburi 44:1-12

Zaburi 44

Kuomba Ulinzi Wa Mungu

Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora.

44:1 2Sam 7:22; 1Nya 17:20; Yer 26:11; Amu 6:13; Kum 32:7; Ay 37:23Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu,

baba zetu wametueleza

yale uliyotenda katika siku zao,

siku za kale.

44:2 Kut 15:17; Kum 7:1; Yos 10:42; 3:10; Mdo 7:45; Isa 60:21; Amu 4:23; 2Nya 14:13; Za 80:9; Yer 32:23Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa

na ukawapanda baba zetu,

uliangamiza mataifa

na kuwastawisha baba zetu.

44:3 Yos 24:12; Kut 15:16; Za 78:54; 77:15; 79:11; 89:10, 15; Isa 40:10; 52:10; 63:5; Kum 4:37Sio kwa upanga wao waliipata nchi,

wala si mkono wao uliwapatia ushindi;

ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume,

na nuru ya uso wako,

kwa kuwa uliwapenda.

44:4 Za 24:7; 5:2; 21:5; 74:12Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu,

unayeamuru ushindi kwa Yakobo.

44:5 Yos 23:5; Za 60:12; 108:13; Dan 8:10Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu;

kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu.

44:6 Za 33:16; Hos 1:7; Mwa 48:22Siutumaini upinde wangu,

upanga wangu hauniletei ushindi;

44:7 Kum 20:4; Ay 8:2bali wewe unatupa ushindi juu ya adui zetu,

unawaaibisha watesi wetu.

44:8 1Kor 1:3; Rum 2:17; Za 34:2; 52:1; 30:12; 2Kor 10:17Katika Mungu wetu tunajivuna mchana kutwa,

nasi tutalisifu jina lako milele.

44:9 Kum 8:3; 31:17; Za 43:2; 107:39; 108:11; Isa 5:15; Yos 7:12Lakini sasa umetukataa na kutudhili,

wala huendi tena na jeshi letu.

44:10 Law 26:17; Amu 2:14; Kum 28:25Umetufanya turudi nyuma mbele ya adui,

nao watesi wetu wametuteka nyara.

44:11 Yer 12:3; 32:37; Law 26:33; Zek 2:6; Kum 4:27; Eze 6:8; Lk 21:24; Za 9:11; 60:1; 2Fal 17:6Umetuacha tutafunwe kama kondoo

na umetutawanya katika mataifa.

44:12 Kum 32:30; Isa 50:1; 52:3; Yer 15:13Umewauza watu wako kwa fedha kidogo,

wala hukupata faida yoyote kwa mauzo yao.

Read More of Zaburi 44