Zaburi 42:1-6 NEN

Zaburi 42:1-6

KITABU CHA PILI

(Zaburi 42–72)

Zaburi 42

Maombi Ya Mtu Aliye Uhamishoni

Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora.

42:1 Ay 19:27; Yoe 1:20; Za 18:33; 119:131; Kum 10:7Kama vile ayala aoneavyo shauku vijito vya maji,

ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu.

42:2 Za 43:4; 143:6; 84:7; 63:1; Yos 3:10; 1The 1:9; Yn 7:37; Rum 9:26; 1Sam 14:19; Mt 16:16; 9:26Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai.

Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu?

42:3 Ay 3:24; Mik 7:10; Za 79:10; 115:2; Yoe 2:17Machozi yangu yamekuwa chakula changu

usiku na mchana,

huku watu wakiniambia mchana kutwa,

“Yuko wapi Mungu wako?”

42:4 1Sam 1:15; Isa 2:2; 30:29; Yon 2:9; Ezr 3:13; Yos 6:5; Za 35:18; 109:30; 55:14; 122:1; 95:2; 100:4; 147:7Mambo haya nayakumbuka

ninapoimimina nafsi yangu:

Jinsi nilivyokuwa nikienda na umati wa watu,

nikiongoza maandamano kuelekea kwenye nyumba ya Mungu,

kwa kelele za shangwe na za shukrani

katikati ya umati uliosherehekea.

42:5 Mao 3:20; Mt 26:38; Za 9:1; 38:6; 77:3; 25:5; 71:14; 56:3, 11; 18:46; Ay 20:2; Isa 50:10Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?

Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?

Weka tumaini lako kwa Mungu,

kwa sababu bado nitamsifu,

Mwokozi wangu na 42:6 Za 43:5; 63:6; 7:11; Mwa 13:10; Hes 13:29; Kum 3:8; 4:48Mungu wangu.

Nafsi yangu inasononeka ndani yangu;

kwa hiyo nitakukumbuka

kutoka nchi ya Yordani,

katika vilele vya Hermoni,

kutoka Mlima Mizari.

Read More of Zaburi 42