Zaburi 40:1-8 NEN

Zaburi 40:1-8

Zaburi 40

Wimbo Wa Sifa

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

40:1 Za 37:7; 116:1; 6:9; 31:22; 34:15; 7:15; 145:19Nilimngoja Bwana kwa saburi,

naye akaniinamia, akasikia kilio changu.

40:2 Ay 9:31; 30:19; Za 7:15; 69:14; 31:8; 27:5Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu,

kutoka matope na utelezi;

akaiweka miguu yangu juu ya mwamba

na kunipa mahali imara pa kusimama.

40:3 Za 28:7; 52:6; 64:9; Ufu 5:9; Kut 14:31Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu,

wimbo wa sifa kwa Mungu wetu.

Wengi wataona na kuogopa

na kuweka tumaini lao kwa Bwana.

40:4 Za 2:12; 34:8; 84:12; 101:5; 4:2; 138:6; Kum 31:20; Mit 3:34; 16:5; Isa 65:5; 1Pet 5:5Heri mtu yule amfanyaye Bwana kuwa tumaini lake,

asiyewategemea wenye kiburi,

wale wenye kugeukia miungu ya uongo.

40:5 Kum 4:34; Isa 55:8; Za 75:1; 105:5; 136:4; 139:18; 71:15; 139:15Ee Bwana Mungu wangu,

umefanya mambo mengi ya ajabu.

Mambo uliyopanga kwa ajili yetu

hakuna awezaye kukuhesabia;

kama ningesema na kuyaelezea,

yangekuwa mengi mno kuyaelezea.

40:6 1Sam 15:22; Isa 1:11; Hos 6:6; Yer 6:20; Mt 9:13; Amo 5:22; Kut 21:6; Za 50:8; 51:16Dhabihu na sadaka hukuvitaka,

lakini umefungua masikio yangu;40:6 Au: bali mwili uliniandalia.

sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi

hukuzihitaji.

40:7 Ay 19:23; Yn 5:39; Yer 36:2; 45:1; Eze 2:9; Lk 24:44; Mdo 10:43; Ebr 10:7Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja:

imeandikwa kunihusu katika kitabu.

40:8 Mt 26:39; Yn 4:34; Ebr 10:5-7; Kum 6:6; Yer 15:16; Rum 7:22; Ay 22:22; 23:12Ee Mungu wangu,

natamani kuyafanya mapenzi yako;

sheria yako iko ndani ya moyo wangu.”

Read More of Zaburi 40